Ambition plus
JF-Expert Member
- Feb 23, 2018
- 6,101
- 11,381
Kaka umefunga PM yako?Nileteee..una kiasi gani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kaka umefunga PM yako?Nileteee..una kiasi gani?
Mtu alieachiwa kuuza nimetoka kula nae dona mda sio mrefuHiyo biashara ni ngumu ina mzunguko mrefu je una uhakika aliyekupa ishu ni mmiliki mwenyewe? Maana kuna zile 2 za mwezi uliopita watu wamepigwa sana
Hata likiwa limechanika kabisa bora liwe linaitwa tu tairi.. Bei ni kwa kiloShukrani bro soon ntakupa feedback, na je hizo tairi unanunua kwa kilo au kwa mfumo upi? na kuna vigezo vyovyote kwenye ubora wa tairi? au ilimradi tu ziwe tairi used
Nb: Tujifunze kujaribu vitu na tusichague kazi[emoji1545][emoji1545][emoji1545]Biashara ya taka Mali ukiiangalia Kwa nje unaweza hisi watu wanapoteza muda, lakn binafsi imenifanya nikabadili mindset yangu Kwa muda mfupi sana.
Changamoto zipo tena sana lakini zinakuwa solved mapema ukilinganisha na zile za leseni na tin namba.
Vyuma chakavu ni biashara inayohitaji mtaji na connection pia mana hio inatolewa macho sana na serikali, kuswekwa ndani kama mhujumu uchumi ni kufumba na kufumbua.
Plastic, chupa, pamoja na mifuko ni salama zaidi.
Hivi ukiwa na mtaji kidogo unaweza kuanza changamoto yake ni ukuaji wa mtaji unachukua mda mrefu kulingana na upatikanaji wa material, cost za usafiri.
Nb: Tujifunze kujaribu vitu na tusichague kazi.
Sasa picha nakutumiaje pm umefungaNaomba picha zake tafadhali
400 kwa lita nahitaji kama lita laki 2 au tatu unayo?Kaka oil chafu na matairi mabovu bei gani unanunua nipe bei kama hutojali.. nipo mwanza
Ukiwa mtulivu na maono baada ya mwezi utajikuta umetengeneza faida kubwa kuliko hata aliyeajiriwa...!
Ni biashara imewatajirisha watu waliowahi kuanza kuifanya nchini Tanzania.Wandugu utu uzima dawa.. Hebu tushauriane kitu kwenye hili la mishe za kutafuta shilingi
Ajira hakuna na changamoto za maisha ni nyingi sana.. Kila kitu ni hela hasa kwa sisi tunaoishi mijini.. Hata kikombe cha maji ni pesa achilia mbali chakula.. Mjini hakuna cha bure! Sasa hata kama hakuna ajira lakini ajira ndogondogo za kujiajiri na kupata chochote hazikosekani...! Ajira zisizohitaji leseni, chumba cha biashara wala kodi ya mwezi na msaidizi..!
Natambua wengi wamekata tamaa na biashara ama wanaogopa kuingia huko kutokana na mlolongo mrefu wa nyaraka na tozo na kodi za kila aina.. Yaani kwa sasa ukiwa na million moja hiyo pesa inaweza kuishia kwenye hayo mambo..sasa ufanyeje ili pesa yako ya msingi ibaki na izalishe chochote?
Mchawi wa hilo uko kwenye 'WASTE' kuanzia
Mifuko ya kila aina
Chuma cha kila aina
Plastiki za kila aina
Mabox ya kila aina
Makaratasi ya kila aina
Chupa za kila aina
Matairi ya kila aina
Oil chafu za kila aina nknk
Kuna pesa huku kwenye waste.. Na unaweza kufika mahali ikawa ni ajira yako rasmi...kuna biashara ya chapchap na pesa yake ni hapo hapo.. Uwekezajia ni mdogo kulingana na uwezoa lakini faida unaiona hapo hapo
Unachotakiwa kufanya ninini?
Wakati wako wa kujiajiri ni sasa..! Mwenzako anapodamka kwenda kuomba kazi sehemu mbali mbali... Wewe damka upite kwenye masoko makubwa wanakopokea na kusafirisha bidhaa sehemu mbali mbali za nchi.. Huko angalia vifungashio tuu, bei zake na upatikanaji wake .. Ziara hii ifanye kwa siku nzima
Siku ya pili damka nenda maeneo ulikoambiwa vufungashio vipatatikana.. Cheki bei zake na upatikanaji wake..hii ziara ya siku ya pili ifanye kwa siku nzima pia
Siku ya tatu damka nenda viwandani .. Angalia wanatengeneza nini na wanatupa nini.. Huko dili na watu wa 'waste' tuuu.. Watakwambia kitu gani kinauzwa wapi na wateja ni akina nani... Hii unaweza kuifanya kwa siku tatu hivi
Kwa siku tano za wiki ikifika Ijumaa jioni utajikuta sio wewe uliyeanza wiki ukiwa hujui hayo yote..hii inaitwa elimu mitaani.com.. Kuanzia hapo anza kutafuta oda ndogondogo kwa mtaji wako.. Ukiwa mtulivu na maono baada ya mwezi utajikuta umetengeneza faida kubwa kuliko hata aliyeajiriwa...!
Hakuna mkuu .. Waajiriwa wengi almost asilimia 90 hasa wa serikali ni watumwa wa mishahara.. Hawawazi zaidi ya hapo.. Na anajua hata akitega namna gsni mwisho wa mwezi anadaka kama kawaMkuu kwanini walioajiriwa huwa wanakuwa kama reference ili kuwapa hamasa ambao wanatakiwa kujiajiri....
Hakuna motivation nyingine ya kuwapa tofauti na kuwalinganisha na walioajiriwa?
Wastani wa kilo 1 ni bei gani mkuu?.Hata likiwa limechanika kabisa bora liwe linaitwa tu tairi.. Bei ni kwa kilo
Je ni lazima liwe tairi la gari au yute mpaka ya baiskeli?.Hata likiwa limechanika kabisa bora liwe linaitwa tu tairi.. Bei ni kwa kilo