Ukiwa na tabia hizi, jiandae kuwa middle class na kuteseka ki uchumi!

Hapana mkuu nyumba ni asset, asset is anything with economic value to the owner and that can be converted to cash however cash itself is an asset. Hata kama nyumba unaishi mwenyewe still is an asset coz it has value and can be converted to cash at future. Hata ukinunua kiwanja ukakiacha usifanyie shughul yoyote ile ni asset, coz land has economic value and you can expect cash flow at future, soma hapa: http://m.investorwords.com/273/asset.html

(i stand to be corrected)
 
Akili yangu ipo wazi sana lakini kuna watu wanataka kutuambia kuwa kujenga ni kuzika pesa kama walivyokaambiwa na Robert kiyosaki ni hapo tu ndipo napopinga,usafiri binafsi pia ni muhimu ktk kukuwezesha kufuatilia biz zako

mkuu saba7 nadhani hujamuelewa mleta mada haujakatazwa kujenga nyumba wala kununua gari ila inatakiwa ujue position yko kiuchumi kwa wakat huo huo km Una mil 12 hlf zote unatka ujengee nyumba hpo ndyo cyo sawa! kwanini hzo mil 12 usifungue mirad km mitatu tofauti uizungushe hyo hela ndani ya mwaka ifike mil 40 then baada ya hpo ndyo unaanza kujenga nyumba yko very comfortable...kwa mfano mini km nilivyokupa mfano hpo juu ningesema hyo mil 1.5 ni ndogo nikanunua pikipiki kwa ajili ya luxury leo hii ningekuwa WP???
 
Ndugu maisha hayana formula maalumu.Gali na nyumba vina u muhimu wake,lita tano za mafuta zinaweza kunipeleka mbali.Sio muda wote hutahitaji daladala,zipo dharura za haraka zita hitaji taxii,kama taxii ningelipa Tsh.10,000 mafuta nitaweka ya sh.5,000 tu,kama uta nunua gari nzima basi gharama za lazima ni ku service gali yako,bima na Load licence hivi viwili kwa mwaka,service kila Km. 3,000 na kuendelea na pia inategemea aina ya oil uliyo nunua sababu ya BP inaenda hadi Km.5,000.Pia huokoa muda wazungu husema "Time is money".

Nyumba ukijenga unatulia na ina dhamana hata kwa mikopo,tena mikopo mingine haihitaji hati bora mali isiyo hamishika hasa kwa baadhi ya benki binafsi.Wapo matajiri walio kopa waka endelea na wapo waliokopa wakafirisika au kufirisiwa no formula hata biashara zilizo fanyiwa resarch kabla ya kuanza huweza kufirisika mfano word adams na hata viwanda vingi wanaendesha wenye mitaji.Biashara hiyo hiyo ukishindwa mwenzio anaweza kuianzisha eneo hilo hilo na ikawepo.Hakuna formula.Maisha kila mtu ana tengeneza Formula yake hakuna kuigana,hata ukiiga baadae uliye muiga anaweza kubadilisha je utamuiga tena?
 

Wonderful comment...key word MAISHA HAYANA FORMULA..nimekubali naunga mkono hoja...Nyumba wawezaitumia kwa mkopo au dhamana mahakamani nk
 
Wakuu nimewasoma wote vizuri sana basi hebu na mie nitupia machache tuu...maisha ni malengo!!!mtu unatakiwa uwe na malengo yako ili mradi uje uishi vizuri wewe na familia yako...kwa sababu sio wote wamezaliwa wawe wafanyabiashara au waajiriwa.Mie nilivyomaliza college nilifanya kazi kidogo hapo Dar lakini malengo niliojiwekea ili nitoke kimaisha ilikua ni lazima niondoke bongo,kwa hio nilikichanga, pesa ilipotosha nikalipa chuo nikakimbilia kwa Obama...nikafika nikala shule nikasave nikashusha mijengo miwili bongo na nikaoa mmbongo na nina familia maisha yanaenda ingawa nw niko kwa pele bado nakichanga na familia iko kwa obama poa... na kila mwaka lazima nije vacation na familia bongo.kwa hio basi maisha ni malengo tu na sio biashara tu ndio inayoweza kukutoa.,tuige mataifa mengine, kama hizo za kusafiri kwenda ughaibuni kusaka life wakenya na waganda wanafanya sana na wengi wao shule ziko vizuri na wana mafanikio sana...kingine lazima tuweke moyo wa kutokata tamaa pindi hali inapokua sivyo kwasababu "winners never quit", na unaweza kuanza na gari au nyumba ukawin kuliko hata huyo aliwekeza kwa biashara...malengo ni muhimu sana.
nawakilisha.
 
True kabisa tena umenyuka suite yako ya kazi na heels unakimbilia daladala usiombe mvua inyeshe weweee ,kamata vitz kula kiyoyozi saafii

chamsingi unapoamua kufanya kitu chochote fanya kikiwa kweli kina umuhimu wa kukifanya kwa wakati huo na sio ilimradi unafanya kama kuionyesha jamii, kama wabongo wengi wanavyofanya
 

salute
 
Jaman investment ni perception on how will you generate income. Nyumba sio lazima uijenge kisha ukakuishi .Inaweza kupangishwa kwa waindi kama wanavyofanya Arusha, then na ww umepanga uswahilini real estate business guys msichanganyikiwe just think every thing can be invested.good night
 
Kaka ulishaanza biashara bila kujua kwamba umeanza biashara.Hiyo nyumba ndio mtaji wako. usingejenga bro ukaingia kwenye business wakati ukiwa kazini ungepoteza sana hasa kwenye nchi ambayo waaminifu wanahesabika? lakini iliweka store fedha yako kwa thamani ya nyumba. you can do it again and you will gate more than 25mill
 

you are very right mkuu...
 
Nyumba ni Mtaji...kama una hati zako za umiliki ukifika Benki pale wanakuona km Mungu..ila kwenye suala la kununua gari nakuunga mkono mtoa mada..
 
Nyumba ni Mtaji...kama una hati zako za umiliki ukifika Benki pale wanakuona km Mungu..ila kwenye suala la kununua gari nakuunga mkono mtoa mada..

I wish hiyo hati ingekuwa inapatikana kwa urahisi unaosema, binafsi nilishakata tamaa na hati, anayefahamu jinsi ya kuipata anaweza kutoa maelezo, or else inaweza ikachukua miaka.
 
Inawezekana ni kweli mkuu..mimi naweza kuwa mhanga wa kuwekeza ktk vitu visivyozalisha.mwisho wa siku vyote nimeshindwa kuvikamilisha..
Pole mkuu hata mie ni mhanga kwa mbaliiiii ila wakati mwingine family background na makosa waliyoyafanya wazee wetu plus kodi ya nyumba pia ni ya kunyanyasana kiasi kwamba mtu anaamua kufanya maamuzi ya namna hii, hoja za jamaa zina msingi sana ila kwa mtu ambae ni muajiriwa na muda mwingi yupo kazini huo muda wa ku-invest ataupata wapi wakati amekubali ku-invest elimu yake kuwatajirisha wengine na ndio maana kuna ambao wanaamua kuanza na mjengo kwa kuwa investment yoyote unahitaji kuwa nayo karibu na ukisema umwachie mtu on your behalf unaweza ukapata kichaa maana hela anazitafuna na nyumba unakuta huna. By the way ushauri wake ni mzuri sana ila tunaangalia mazingira na aina ya kazi tunazofanya unless kama mtu amebahatika kuwa mfanya biashara moja kwa moja bila kuajiriwa sehemu though mtu anaweza kuanza na nyumba kwa lengo la kuitumia kama dhamana pindi anapoona mambo ya ajira hayaendi na kuamua kujikita kwenye biashara
 
I wish hiyo hati ingekuwa inapatikana kwa urahisi unaosema, binafsi nilishakata tamaa na hati, anayefahamu jinsi ya kuipata anaweza kutoa maelezo, or else inaweza ikachukua miaka.
Hati inapatikana bila zengwe kama utaamua kuifuatilia pia inategemea na upo eneo gani, kwa uzoefu kwa Dar kidogo inakuwa shida hasa kwa wale ambao wanakaa maeneo ambayo hayajapimwa though huwa wanapewa leseni ya makazi ambayo pia unaweza kuombea mkopo. Kwa mikoa mingine including Rock City hati inapatikana hata kama unaishi eneo ambalo halijapimwa kikubwa eneo uliopo uwe umejenga nyumba pia liwe kwenye master plan ya mji kama eneo la makazi na si viwanda au lilitengwa kwa shughuli zingine
 
Wazo la jamaa ni bomba mno ila pia kuna limitation ambayo ni hiyo uliyoielezea maana huwezi kuwatumikia mabwana wawali yaani huku mwajiriwa na huku mfanya biashara mwisho wa siku hela ikikata na nyumba huna na kazi huna itakuaje hapa? maana mie naona nyumba inaweza baadae ikatumika kama dhamana na kuitumia kupata mkopo then unaanza kufanya biashara

Kwa point yake Nkobe inatupa changamoto kwamba kama unapata hela ya kutosha na ajira yako inakupa muda wa kutosha wa kufanya mambo mengine ni vizuri badala ya kukomaa na nyumba unaweza kufikiria ku-invest ili ujiweke vizuri kiuchumi then unaendelea na masuala ya ujenzi, kwa case yako kama ulivyochangia wakati mwingine ndio changamoto zinazowafanya watu wakomae na mjengo kwanza pia bado hakijaharibika kitu maana unaweza kuitumia nyumba kama dhamana ya mkopo.
 
Last edited by a moderator:


Usipotoshe watu,sio lazima kuanza kama walivo anza wahindi.
Naweza nunua gari ya 10m,lakini siwezi jenga nyumba (yoyote ile)ya 10m.

Kama uwezo wangu ni 10m kwa sasa,na nahitaji gari kwanini nisinunue gari huku nikijipanga na mengine hayo?

Hivi ndivo nilivo anza,na i promise you sita struggle kama unavo taka watu waamini.

1.Nikiwa chuo nikanunua shamba ekari8 kwa 1.3m mkuranga.
2. Nika graduate 2012 na nikanunua gari 2013, (hili lilinisaidia kutembelea shamba kirahisi zaidi,point: Fanya kile unacho weza kufanya kwa wakati huo,don't stretch beyond your limit kwa kukimbilia kujenga afu unaacha nyumba ikiwa kwenye msingi kwa 10 years)

3. Etc etc etc,najua ujenzi jinsi ulivo na gharama zake,ukibebesha mtu mawazo ya JENGA KWANZA kabla ya chochote,tena unasema JENGA NYUMBA YA BIASHARA. Nadhani hauwi realistic,au haujui unacho kiongea in terms ya gharama halisi na maisha halisi ya mwajiriwa wa kitanzania.

Good day.
 

Hivi ukiwa na 50m,ni nyumba gani ya biashara utakayo jenga? Guest house au?
Kila mtu akijenga hiyo mitaa itakuaje? Acheni kupotosha watu.
 
sidhani kama kuna ukweli, maisha ni kujipanga na kupanga ni kuchagua. nyumba na gari nayo ni mahitaji ya msingi sana tu ya kuanza nayo kama hukuwa navyo na haijalishi ununue vya kwanza au vya mwisho, jitihada binafsi ndio muhimu zaidi

Wewe unayajua maisha,sio hawa wanao andika mambo walio jifunza darasani
 
For your information! The richest investor in the world Warren Buffet alianza kujenga nyumba yake before hajaanza biashara alikuwa ameajiliwa wakati huo.
Nawashauri vijana in their 20's to build their career rather than entering into debts.

That is realistic
 

Tuna tofautiana vipaumbele,lakini yote maisha na lazima kutoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…