Ukiwa nje usiwaamini ndugu Bongo, ndoto ya kurudi nyumbani mazima imefifia kutokana na ujenzi hafifu

Ukiwa nje usiwaamini ndugu Bongo, ndoto ya kurudi nyumbani mazima imefifia kutokana na ujenzi hafifu

mleta mada nilichojifunza ni kwamba unatutangazia kua unaendelea na ujenzi tumeshajua.
Huwez ukawa ulishajenga na unajua gharama za ujenzi alaf uulize nyumba finishing itaweza malizika ndani ya mwezi hapo unaniacha na maswali kwamba huenda ni stori tu.
Nipende kusema ukiwa na pesa utahamisha bahari sembuse hako kanyumba kukapiga makeup chapchap kkae mkao.
ILA NI KAMA UNA HELA
 
Basi nikajua kwa malalamiko haya utakuwa mjengo wa kisasa hadi nitamani kuzamia Ughaibuni.
Sio mbaya, hiyo nyumba haina uzio yaani ukuta na naona finishing bado sidhani kama kwa muda huo unatosha.
Watu mnaopata bahati kwenda nje na mkaamua kufanya uenzi wa makazi bora muwa mnajenga kwa kutumia makampuni badala ya ndugu zenu, mnakwepa makampuni ya ujenzi ila ndugu mnaowaamini wanawapiga pesa nyingi kuliko mngezolipa ktk kampuni.
Sinza hapa nilikuwa nafanya nami vimichakato vyangu, kuna jirani yangu alinunua nyumba mbli kupata moja, bei alioambiwa na ndugu zake alipigwa zaidi ya mil 28, kwenye ujenzi ni balaa tupu hadi roho inaniuma. Kuna kibustani mbele ya nyumba kidogo ndugu yake kwamwambia kinahitaji mil 3 ili kikae mkao duuu.
Haya nimekusikia dangote.
 
Unavyoona watu wengi wa hapa duniani wanapata majuto makubwa na kuanguka ni kutokana na watu wa karibu especially ndugu hawana uaminifu sometime mtu baki kama rafiki anaweza kuplay fair kuliko ndugu...better kumuamini mke kama mshazaa na mna familia kuliko kwa sasa Tamaa ni nyingi mno mbele ya pesa
Mungu akubariki kwa ushaur mzuri uliotoa mkuu.
 
Mkuu tupe connection huko kaburu, passport zipo tayari. Niandae kiasi gani ili niweze kufika nakusaka tonge huko?
Mkuu kaburu kwa nyie mnaokuja sasa hivi kuna changamoto zake. Sisi wengine tunatusua kwa sababu kitambo mno maisha mabovu haya, afu tunazijua kona zote za kusakia tonge.
So tunapatia tonge letu kutokana na uzoefu wetu.
 
Ishu kama hizi unatenga tu muda kama ni mwezi mmoja unakuja unasimamia mafundi mpaka sehemu fulani unasimama ukipata tena nafasi unarudi
Kweli mkuu, dah najilaumu sana kwa kuwamini ndugu mazima.
 
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.

Ndugu wanajamii forum wenzangu, unapokuwa nje ya nchi mara nyingi unakumbana na changamoto nyingi kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki uliyowaacha nyumbani.

Hii ni kutokana na wao kuona, au kuamini kwamba unao uwezo wa kufanya kila kitu kwao. Na kibaya zaidi hata utapojaribu kufanya baadhi ya vile unavyoweza kufanya bado utaendelea kubebeshwa lawama tu, ili mradi wahakikishe kuwa wew hauwezi ukaishi bila lawama zao.

Mwaka 2019 before corona nilikwenda bongo nikanunua kiji eneo maeneo ya salasala. Mpaka hapo tayari nilikuwa na eneo langu lingine ambalo tayari nimeshajenga kule Kigamboni, sehemu fulan inaitwa yebo yebo. Ila mimi binafsi nilipojaribu kupalinganisha Kigamboni na Salasala maeneo niliyonunua mimi, niliona kwamba Salasala ndio panafaa kuwa makazi yang ya kudumu pindi ntaporudi kuishi bongo mpaka pale muumba ataponichukua.

Kwahiyo nilivyorudi kaburu ikabidi nianze jitihada za ujenzi kule Salasala ili nishushe mjengo nitakaoishi mimi na familia yangu afu ile nyumba ya Kigamboni nitaipangisha. Kwa sasa kule yebo yebo Kigamboni anaishi brother wangu ambae na yey ana kiwanja chake huko huko Kigamboni anajenga, kwahiyo wakati namalizia mjengo wangu wa Kigamboni aliniomba akae kwanza kwa muda ili awe karibu na shughuli yake ya ujenzi afu nyumba yake ikishaisha ndo atapohama na kuniachia nyumba yangu nipangishe, nkasema haina noma bro.

Sasa basi ujenzi wa Salasala niliuanza mwaka 2020 nikitarajia kuwa katikati ya mwaka huu wa 2022 niwe nimeshamaliza afu ikiwezekana mwezi wa 12 nikienda bongo likizo iwe ndo kimoja nisirudi tena Kaburu. Cha kushangaza pamoja na jitihada zote nlizofanya lkn wanaosimamia mjengo wangu ndio wananikwamisha. Nyumba inaenda kimdondo sana mpaka inanikatisha tamaa kama ninaweza kuihamia mwishoni mwa mwaka huu.

Kabla ya kuanza ujenzi huu kuna watu walinishauri kwamba ni bora nimtume mama watoto aende kukaa bongo ili awe anasimamia shughuli za ujenzi kuliko kuwaamini ndugu tu pekee, mimi nikakaidi kwa kuona kuwa kamwe siwezi kumuweka mke wangu mbele ya ndugu zangu.

Sasa matokeo yake majuto ni mjukuu. Na mimi kuhamia Kigamboni staki naona kumenikalia kushoto sana aisee. Wana JF wenzangu mnaonaje, hivi mjengo huu unaweza kuisha kwa mwezi mmoja uliobaki kweli?

Maanake kuishi mbali na nyumbani kwa muda mrefu nako kunachosha.

View attachment 2400496View attachment 2400497
Nipe hiyo kazi. Ndani ya mwezi itaisha. Hata Kama ukihitaji fensi, itakamilika ndani ya mda huo
 
Huyo atakuwa mhaya

Tena aweza kuwa kupiga picha nyumba ya jirani yake Profesa Rwarubisi Ndizi Bukoba anayefundisha chuo kikuu wanachosoma maraisi wa dunia akiwemo Joe Biden yeye akiwa ndie mkuu wa hicho chuo!!
Ukabila unatoka wapi mkuu, afu kama haunijuagi vizuri humu mimi ni wa kaskazini. Hao wahaya unaosema wew wengi wao ni choka mbaya, ila wako vizuri shuleni.
 
Kuna idadi ya kutosha ya watu waliolizwa na wake zao.

Mimi kuna Mshikaji alikuwa Marekani amemtumia mshikaji tu wa mtaani kusimamia nyumba yake mpaka imeisha na jamaa akaendelea kukaa kuilinda nyumba, mshkaji yupo hapa Sasa hivi amekuja likizo amemnunulia jamaa zawadi ya gari IST afanye uber.

Na nyumba iliyojengwa INA standard zote mpaka Rangi zake ni viwango, kwenye hili Mimi naona ni jinsi ya mtu kujipanga siku hizi kuna video call unaona vitu kwa uhalisia.
Washikaji kama hao wamebaki wachache sana, ni rahisi kushinda bahati nasibu kuliko kupata waaminifu kama hao
 
Nilitaka kusema mshukuru Mungu hata kama wameweza kuifikisha hapo

Halafu akili nyingine ikaniambia aah wewe unaamini ndugu kama ni mapicha ya nyumba ya watu wengine na wewe unazugwa tu mjengo wako huo?

Ila mimi ndugu zangu hawakuniangusha kwa sababu wako vizuri sana kimaisha
 
Hiyo mbona imeshaisha unaweza kuhamia. Watu wanahamia kwenye nyumba hazijapigwa hata plaster. Na nimeona kama kuna nguo zimeanikwa.
Yaani wewe hamia tu hata leo, utamalizia ukiwa hapohapo
 
Ni vile tu pesa ni za shida ila ukiingia mkataba na kampuni za ujenzi huwa stress zinapungua sana.
 
Huyo atakuwa mhaya

Tena aweza kuwa kupiga picha nyumba ya jirani yake Profesa Rwarubisi Ndizi Bukoba anayefundisha chuo kikuu wanachosoma maraisi wa dunia akiwemo Joe Biden yeye akiwa ndie mkuu wa hicho chuo!!
Ukabila unatoka wapi mkuu, afu kama haunijuagi vizuri humu mimi ni wa kaskazini. Hao wahaya unaosema sisi tumeaacha mbali kimaendeleo
Wenyewe hawataki wageni, mtaelewa lini hili somo?

Hata ufanye kazi miaka 20 South Africa kwa mshahara wa deiwaka hutoki, wanaofanikiwa na kufanya mambo Bongo hawatokaa wakwambie siri ya mafanikio yao.
Huu ndio ukweli mchungu mkuu 😂😂😂
 
Back
Top Bottom