Ukiwa nje usiwaamini ndugu Bongo, ndoto ya kurudi nyumbani mazima imefifia kutokana na ujenzi hafifu

Anza sehemu muhimu kama chumba na choo kuweka sawa, unahamia. sehemu nyingine unamalizia ukiwa humo humo ndani taratibu bila stress.
Asanteni mkuu kwa ushauri murua kabisa.
 
Msaidiane na mke wako kuisimamia, project kama hiyo kumpa ndugu ni kutafutiana lawama tuu labda awe milionea na awe na muda, mtu pekee katika ndugu naweza kumuamini ni mama yangu tuu na hata akila inaweza isiniume sana
Ushauri wako ni mzuri na uliloongea ni kweli. Mtu pekee ambae hata akila hela yako hautakuuma sana na mara nyingi huwa hawali ni wazazi tu, ila waliobaki uaminifu ni mdogo mno.

Mi nimeshajifunza tayari.
 
Mtu anaeamini ndugu zaidi ya ubavu wake anaolala nao na kuamka nao, ukiumwa hoi anakuogesha uchi aiseee lazima kikukute kitu. Hivyo we kazana tu na ujenz wako
Dah mkuu maneno yako yamenigusa sana, utafikiri ni mke wang ndio alienambia hivyo.

Hata hivyo nimeshajifunza kutokana na makosa, na kamwe sintorudia kosa.
 
Kwakuwa ulisha nunua kiwanja ungechagua kati ya:
1. Kujenga kwa kutumia mkandarasi ambaye mnasaini mkataba na mnalipana kwa hatua ya ujenzi ulipofika. Hii ni nzuiri haina usumbufu wa kina fundi maiko ila ina gharama zaidi.

2. Ukusanye fedha uweke kwenye akaunti ukirudi upange maeneo jirani na site yako usimamie ujenzi mwenyewe ukiwa umesharudi tayari. Nyumba utakayoishi inauhitaji wa ww kuisimamia na kufanya maaumuzi.

3. Mkeo asimamie kama ulivyosema.

Fedha haina undugu sana sana utagombana na nduguzo kwa kuwapima imani ya kuwapa fedha za ujenzi.

Sijui kwanini tanzania hakuna developers wengi wa nyumba kama nchi nyingine ambapo suala la mtu mmoja mmoja kujenga halipo sana bali ni kununua tu nyumba au apartment iliyokamilika.
 
Ya ulichoongea ni ukweli mtupu mkuu, ila umbali na mishe zetu ndo zinanishinda kuja kusimamia.

Ndugu ndio watu wanaoongoza kwa kurudishana nyuma, hata ukiwa mwema kiasi gani.
Nadhani sio ndugu na sio ndugo wote ila wengi wao hata marafiki japo nao sio wote lakini wengi tu, Tz shida kubwa maneno matamu kama asali ila wao huwa wanafikiria kwanza nitapigaje hapa nifaidike huwa maslahi yao wanaweka mbele lakini angalizo tu ukiona rafiki au ndugu au yoyote anatumia nguvu nyingi za ushawishi juu yako basi kimbia haraka ogopa mimi nakushauri ukitaka kufanya kwa haraka tumia fundi unayemuamini aweke gharama za umaliziaji na za kazi yake halafu wewe simamia manunuzi mbona siku hizi Mobile pesa zipo unaweza kufanya hata huko uliko kama step by step hili utaepuka kugombana na ndugu au marafiki bora ugombane na mafundi.
 
Ukisimamia mwenyewe ndo hautajiibia hata wake wanawaibia waume zao, mara nyingi nimeona wake wakiwadalalia waume zao bei za materials

Ni bora upigwe pesa kuliko kwenye materials maana unaweza kuletewa materials zilizo na ubora wa chini baada ya miaka michache nyumba yako usiitamani tena

Kama kibunda kipo wengine wanatafuta likizo hata ya mwezi mmoja wanasimamia ujenzi mpaka wanamaliza

Ni Salasala eneo gani mkuu?
 
Nimekuja hapa kupata ushauri na kupunguza stress baada ya kutuma zingine afu mabadiliko ya ujenzi au muendelezo ni zero.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]nacheka kama mazuri.

Sasa nguvu ya kuwatumia zingine unaitoa wapi?

Au ndio mambo ya damu nzito.....
 
Salasala ukanunua 'kijiji' ukaanza 'mjengo'. We jamaa lazima ni Mhaya. Ila hongera unapambana. Ila kama mjengo wenyewe ndo huo hapo kwa picha mimi naona kama hao ndugu hata kwenye design walizingua.

Hako ni kanyumba siyo mjengo. Kuta fupi sana yaani headroom ndogo sana. Vibaraza vimeminywa, fundi kaezeka kama nyumba ya kuku. Halafu it seems ujenzi ulisimama long time. Dah aise kweli ndugu noma. Anyway, all the best mkuu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]nacheka kama mazuri.

Sasa nguvu ya kuwatumia zingine unaitoa wapi?

Au ndio mambo ya damu nzito.....
Ndg nao wanaloga sana siku hizi! Utatumaa tu hata ukilalamika uko pembeni!!
 
Dah ningekuwa na mawazo kama haya ya kwako, wala yasingenipata haya yalionipata.

Naweza kusema kwamba nimekumbuka shuka asubuhi. Ila kwa sasa nimepanga kumtanguliza mke akasimamie pale palipobaki, maana ndugu sina tena haja ya kuwaamini tena.
 
Siku nyingine ujenge ukiwa likizo, utapata kichaa bure, hivi hiyo design ndo uliichagua? Mbona bati hilo kama litapauka? Anyway polee
Yan mambo mengi yamekwenda ndivyo sivyo. Ila sasa nimejifunza kutokana na makosa best angu.
 
Kweli mkuu ushauri wako mzuri sana. Na kwa vile nimeshajua wapi nilipokosea, basi siwezi tena kurudia kosa.
 
Ndugu zako wapo poa tu mbona!,mimi nilituma pesa miaka mitatu nakuta msingi tu wa nyumba tena ushaanza kubomoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…