Wakuu
Kufulia kusikie tu kwa jirani.kuna kipindi kama miaka minne imepita,niliwahi kufulia kiasi kwamba nilikosa hata mia mbovu mfukoni.nikaona mambo yasiwe mengi nikauza zangu laptop yangu ilikua mpya kabisa aina ya HP kwa bei sawa na bure ili mambo yaende,ebana nikikumbukaga hii issue najihisi kuumia sana.
Kuna yeyote aliwahi kukumbwa na majanga kama haya?
Mimi ni kama nilitumia ujanja kuuza vifaa vyangu chakavu vya ndani.
Nilimtuma mke wangu akakope(kiwango nakificha) mimi nikiwa mdhamini wake kwenye makampuni ya kopesha, wanaita kausha damu.
Yalipoanza marejesho, akarejesha mara moja halafu nikamsafirisha mkoa ili mi nilimalize soo kwa raha.
Vifaa walivyokuja kuvikagua kama dhamana kabla ya kuidhinisha mkopo vilikuwa ni vile nilivyoviselect kuviondoa kwa matumizia ya nyumbani kwangu.
Kulikuwa na Tv old model ya kichogo, jiko kubwa la umeme, friza, vifaa hivyo vilikuwa vinatumia umeme mwingi nishavichoka.
Siku ya marejesho ilipofika nikapokea simu namba ngeni wakajitambulisha na kumuulizia mke wangu, maana hawampati kwenye simu.
Nikawajibu kuwa alipata dharula na kasafiri vijijini ndanindani hawawezi kumpata.
Nikawa nimewapandisha hasira, kumbe sikujua kuwa wakopaji huundishwa kikundi na kulazimishwa kudhaminiana wao kikundi kizima na kama mmoja wao kwa sababu yoyote hatarejesha, kundi zima linatakiwa kumchangia ama mdhamini wake awajibike.
Nikashitukia kundi kubwa la kinamama hata siwajui wakatinga nyumbani kwa bashasha kuja kufanya kitu wao wanaita kufirisi.
Walipofika wakadai nimlipie mdaiwa niliye mdhamini, nikawaaambia pesa sina, wamsubiri mwenzao atakaporudi atawapelekea rejesho lake.
Ebanaee!
... 'Hatukubali na hatuondoki mpaka ulipe rejesho ama sivyo tunaondoka na vifaa alivyoviandikisha dhamana'.
Nikajiulizisha, ... 'Kwani kitu gani aliandikisha'?...
Wakavitaja, nikawaambia piteni ndani mchukue, mi sina hela.
Wakaingia wakakusanya vifaa hivyo wakaondoka navyo tukawa tumemalizana nao.
Walivyoondoka nikachana mabox ya vifaa vipya nilivyokuwa tayari nishaviandaa siku nyingi nikavipachika.
Kwa hiyo vifaa vyangu chakavu niliviuza kwa njia hiyo ya kisomi.