Ukiwa umefulia ni kitu gani chako cha thamani uliwahi kukiuza ambacho leo ukikumbuka nafsi inakuuma?

Tulipanga na demu wangu akajilengesha mshikaji kajichanganya nikafumania na wajeda kwa kuogopa status yake jamaa kapiga ofisini chapu tukala milioni 5.5 ila kwa kuchelewa ilishakuwa imeliwa round moja si wajua tena wazee wa bao la kuku dakika tano nyingi ikawa imeenda
 
Siku moja nilikamatwa na shida haswa nikauza pete yangu ya engegement niliyoitunza miaka zaidi ya 6 baada ya uchumba kuvunjika. Huwa najuta kuiuza sababu hata shida haikutatulika vizuri
 
Nilikua na mgonjwa nyumbani nikaamua kuuza jogoo wangu mkubwa ninunue dawa, nikaenda center kutafuta mnunuzi jamaa nilie mpata akasema yupo busy kwasasa atakuja home badae amuone jogoo ila Cha kunisaidia akanipa 5000/= kwanza ninunue dawa ili badae akija home tuelewane na ataongeza kiasi kingine. Mimi nikachukua Ile Hela nkanunulia dawa yote. Jioni jamaa akaja aisee jogoo ni mkubwa bi mkubwa alinambia nimuuze si chini ya 12000/= lakini mwamba akakaza ELFU 7 tu. Kama sitaki nimrudishie 5000/=. Jogoo alichukuliwa Kwa bei rahisi Kwa vile nilikosa namna ya kufanya. Ni miaka mingi imepita ila tukio hilo Huwa nikikumbuka naumia sana. Ilikua mwaka 2005. Umaskini bro usikie tu Kwa watu wengine
 
Mimi ni kama nilitumia ujanja kuuza vifaa vyangu chakavu vya ndani.

Nilimtuma mke wangu akakope(kiwango nakificha) mimi nikiwa mdhamini wake kwenye makampuni ya kopesha, wanaita kausha damu.

Yalipoanza marejesho, akarejesha mara moja halafu nikamsafirisha mkoa ili mi nilimalize soo kwa raha.

Vifaa walivyokuja kuvikagua kama dhamana kabla ya kuidhinisha mkopo vilikuwa ni vile nilivyoviselect kuviondoa kwa matumizia ya nyumbani kwangu.

Kulikuwa na Tv old model ya kichogo, jiko kubwa la umeme, friza, vifaa hivyo vilikuwa vinatumia umeme mwingi nishavichoka.

Siku ya marejesho ilipofika nikapokea simu namba ngeni wakajitambulisha na kumuulizia mke wangu, maana hawampati kwenye simu.

Nikawajibu kuwa alipata dharula na kasafiri vijijini ndanindani hawawezi kumpata.

Nikawa nimewapandisha hasira, kumbe sikujua kuwa wakopaji huundishwa kikundi na kulazimishwa kudhaminiana wao kikundi kizima na kama mmoja wao kwa sababu yoyote hatarejesha, kundi zima linatakiwa kumchangia ama mdhamini wake awajibike.

Nikashitukia kundi kubwa la kinamama hata siwajui wakatinga nyumbani kwa bashasha kuja kufanya kitu wao wanaita kufirisi.

Walipofika wakadai nimlipie mdaiwa niliye mdhamini, nikawaaambia pesa sina, wamsubiri mwenzao atakaporudi atawapelekea rejesho lake.

Ebanaee!
... 'Hatukubali na hatuondoki mpaka ulipe rejesho ama sivyo tunaondoka na vifaa alivyoviandikisha dhamana'.

Nikajiulizisha, ... 'Kwani kitu gani aliandikisha'?...

Wakavitaja, nikawaambia piteni ndani mchukue, mi sina hela.

Wakaingia wakakusanya vifaa hivyo wakaondoka navyo tukawa tumemalizana nao.

Walivyoondoka nikachana mabox ya vifaa vipya nilivyokuwa tayari nishaviandaa siku nyingi nikavipachika.

Kwa hiyo vifaa vyangu chakavu niliviuza kwa njia hiyo ya kisomi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…