Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Ukiwa unampa sana mama yako pesa, anahisi kuwa wewe unazo sana. Hata kama umejitoa tu ili mama yako asipate shida, kuna namna anaamini kuwa huyu mtoto wangu anacho tu!
Hivyo, mara nyingi anachukua matatizo ya ndugu wengine na kukuletea! Ndiyo maana ndugu wengi sana watamfuata kumuomba msaada wakijua atakuomba wewe na wao kufaidi, bila kujali kama mambo yako yanaendelea vizuri au la!
Hivyo, kama unampenda mama yako kweli, kabla ya kumpa pesa, hebu jiulize: je, hiki kitu anakihitaji kweli? Je, kiasi hiki cha pesa na matumizi yake ni sahihi?
Ndugu hawataki kukuomba wewe moja kwa moja wakijua utakataa kwa sababu vitu wanavyoomba ni vya kijinga au si vyalazima.
Mfano, anataka kumalizia nyumba wakati wewe huna hata kiwanja, anamwomba mama yako akijifanya anaumwa ili mama yako akuombe umpe pesa.
Ukweli ni kwamba, hata ukitoa, bado watakuona una roho mbaya. Kuwa na kipimo!