Hakuna jibu la maana ulilopewa hadi sasa. Ukweli ni kwamba ukiweka gari full tank utatumia mafuta zaidi katika kuendesha gari kadiri yafuta yalivyo mengi, kwa sababu mafuta yanakuwa sehemu ya mzigo katika gari kwa hiyo injini inabidi ifanye kazi ya ziada kubeba mzigo wa mafuta.
Kihesabu tunasema fuel consumption is directly proportional to fuel level in the tank; C = kL, where C = fuel consumption rate, k = constant of proportionality, na L ni fuel level in the tank. Hiyo "k" ni assumption kwamba factors nyingine hazibadiliki, mfano idadi ya abiria ndani ya gari. Au kwa njia rahisi ni kwamba, rate ya consumption ya mafuta iko directly proportional na uzito wa gari. Kwa hiyo kadiri unavyojaza tank ndivyo unavyoongeza uzito wa gari na ndivyo gari itakula mafuta zaidi. Ulaji wa mafuta utapungua kadiri mafuta kwenye tank yanavyopungua, au kadiri uzito wa gari (load) unavyopungua.
Hiyo pia ndio sababu ndege haziweki full tank zinaporuka kwenda safari fulani, wanaweka mafuta yatakayotosha kuwafikisha wanapokwenda, na ziada kidogo ya emergency
Ndio maana unashauriwa usiweke vitu usivyohitaji kwenye buti ya gari kwa kuwa inafanya gari itumie mafuta zaidi. Utakuwa umesikia watu wakisema magari ya siku hizi ni karatasi sana tofauti na ya zamani - ni kweli na hilo lilifanyika ili kupunguza uzito wa gari ili lisitumie mafuta kwa wingi.