Ukizielewa Siasa za Tanzania huwezi kupata tabu. Hongera Rais Samia kwa kuzielewa vyema Siasa za Tanzania, nasema kazi iendelee

Ukweli kabisa! Watu wana hali mbaya sana za kimaisha, huduma duni za kijamii na miondombinu mibovu. Linapokuja suala la watu hawa kukombolewa ili watolewe huko na wawe na maisha mazuri yenye hadhi ya kibinadamu haswa watu hao hao wanaanza propaganda chafu za kupinga hivyo vitu huku wao na vizazi vyao wakizidi kuangamia kwa maisha magumu.

Mama Samia amefanikiwa sana kuzigundua hizi akili mfu za watanzania maana bila kuzigundua mapema angeishia pabaya sana!
 
Mfuasi wa jiwe uliyezoea kuwa brainwashed na Jiwe lazima uwe na ukakasi linapokuja suala la Mama Samia. Hata ujitahidi vipi lazima unajionesha tu kuwa una ukakasi nae.
 
Siasa za kuchukia matajiri muhasisi mkuu ni magufuli na misukule yake ya sukuma gang aliyoiacha
Wana maisha mabaya, duni na hovyo kupindukia, watoto/ ndugu zao hawana ajira kila siku kuhangaika mtaani na bahasha za kaki alafu muda wote wanakalia kukataa Sera Nzuri zinazofanya nchi iwe na uchumi mzuri kwa faida yao na vizazi vyao.

Tatizo waliamini huyo Magufuli na Mungu wakati alikuwa ni mjinga ambaye wala hakustahili kuwa Raisi wa nchi yetu kwa namna alivyoturudisha nyuma.
 
Mama amekomaa sana kisiasa
Mungu amuweke kwa kweli
Nnachompendea kelele za mitandaoni hazimbabaishi
 
Mama amekomaa sana kisiasa
Mungu amuweke kwa kweli
Nnachompendea kelele za mitandaoni hazimbabaishi
Ukiendekeza siasa za watanzania, utaishia kusifiwa na viongizi wa dini kuwa Hakuna kama wewe, huku vijana wakikosa ajira na kurundikana kwenye kukusifu na kukuabudu ili uwape uteuzi huku maelfu ya wananchi wakiwa wachuuzi wasiolipa kodi na kujiita machinga wanaofunga barabara zote kwa utaratibu mbovu wa kufanya biashara na kuharibu mipango miji.
 
Alafu wanalipa kodi 20000 ya kitambulisho yule anayelipa kodi ya millioni amezibiwa biashara akiuliza anaambiwa yeye ni beberu nchi ilifika pabaya hii tajiri alionekana kama mtenda dhambi na mdhulumaji maskini akidhani amewin kumbe tajiri akifilisika hali inakua mbaya zaidi kwa maskini
watu wamemaliza chuo mishe hamna basi hata kama serikali ilishindwa kuajiri basi private sector iajiri sasa matajiri wamekimbia
Alafu wanatokea wapumbav wachache wanasifia ule udhalimu kisa wao either walikua wanafaidika au waliojaa roho mbaya na chuki
mama asingeenda kenya sijui mahindi yetu tungeuza wapi
 
Mfuasi wa jiwe uliyezoea kuwa brainwashed na Jiwe lazima uwe na ukakasi linapokuja suala la Mama Samia. Hata ujitahidi vipi lazima unajionesha tu kuwa una ukakasi nae.
Mimi ni tofauti na wewe unayeongea na dhamira potofu kwa mlengo wa kisiasa. Hakuna mahali nimekuwa na ukakasi zaidi ya kuchangia mada au kuanzisha katika muktadha wa kitaifa.

Kuhusu Rais SSH, sina shaka naye kwa kuwa ana maono sahihi ya maendeleo ya nchi hii kulingana na Ilani ya Uchaguzi ya Chama chake Tawala. Naamini pia ana utashi wa kisiasa, ambao viongozi wengi wakisiasa hawana
 
Hii nchi ilikuwa inapelekwa pabaya sana ndugu yangu. Acha tu Mungu ametuokoa maana angeendelea ndani ya muda mfupi uchumi unge collapse kabisa na tungekuwa Kama venezuela
 
Haujiulizi kwanini uzi wako una comments ishirini tu ndani ya siku mbili? — ambazo kati ya hizo, za kwako tu ni zaidi ya kumi.

Niulize nikujuze.
 

Mkuu hongera kwa bandiko zuri. Je mkuu unakubaliana na masharti Wachina waliyoyatoa ili kujenga bandari ya Bagamoyo?

Ahsante
 
Nina amani sana ninapoona siongozwi na kiongozi wa Malaika waasi
 
Naona wewe ni cha matusi uko mini siko 🚿
 
Mkuu Lord denning Asante Sana kwa andiko zuri linalo elimisha. Watanzania walikuwa wanapata habari za upande mmoja baada ya vyombo vya habari kutishiwa kufutwa au kufungiwa kwa kuandika habari ambayo Mwendazake alikuwa haipendi.

Sisi tuendelee kuwapa elimu ya bure maana wamekuwa indoctrinated na propaganda za UWONGO kwa miaka 5 non stop.

I wish CCM mwaka 2015 wangemsimamisha SSH kama mgombea na Jiwe ndiyo angekuwa Mgombea Mwenza, Leo tungekuwa mbali Sana kiuchumi.
Mama amekomaa sana kisiasa
Mungu amuweke kwa kweli
Nnachompendea kelele za mitandaoni hazimbabaishi
 
Samia nenda Rais wangu usiangalie nyuma, kwani ndege muoga hawezi kupaa kamwe.
Tumekuwa makinda yaliyo lemaa kwa muda mrefu, tukimuogopa kila anaepaa kwa uoga wetu wa kujifunza kuruka, kama hao ndege wengine warukao.Tuchukue tupeleke angani na utuachie usituonee huruma tuache tupambane kwa ajiri yetu.
Bomoa kila kitu kilicholenga kutulinda tusiuone mwanga,kutulinda tusijifunze kuruka kama ndege wengine,bomoa hicho kiota cha uoga kiondoke katikati yetu,ili kila mtu ajue anapaswa kuruka,usiwasikilize watakao ficha mbawa zao ipo siku watauona umhimu wa kuruka na kuiona dunia.
tunawaogopa hata tusio stahili kuwaogopa wakenya wakenya!!!!! nashangaa hata wao siku hizi wameanza kutuogopa nimewasikia majuzi ulipo bisha hodi,oh wanakuja kwa spidi kubwa sana,ila sisi tofauti na wao hawaogopi kushirikiana nao! maajabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…