Uko tayari? Dar es Salaam mpya inakuja. Serikali kutwaa eneo la mita za mraba 233,000. Maeneo ya Sinza, jirani na Mlimani City, Boko, SIMU2000 kuguswa

Hili tangazo nkajua ni fake.
 
Unaweza kupanua mji kujenga nje kidogo nje ya ya mji kama kibaha, Morogoro. SGR inafika.
 
umesahau kuwa ardh ina term miaka 33 au 99 serikal ikiamua inasitisha mkataba wako na wao. hati ni just paper na unaambiwa siku rais akiitaka kwa maslah ya umma inachukuliwa. wakaishi wap kwan hakuna pa kuish. hiv u a milion 200 mfukon unaambiwa pisha tujenge kwanza kisha utarud utakosa pa kwenda. ? au unapenda kuona tandale inakaa kwenye maji ya choo maisha yote ukipita pale kwa bi nyau unaziba pua. afadhal afazal alipokuwa makonda alisimamia ule mto upanuz ndio hapo harufu imepu gua
 
Iweke na miundo mbinu itayo wapa wazo watu kuhamia nnje ya mji, mfano ujenzi wa express way dar moro na mengine
 
Soma mtiririko ujue kwa nn nimekuuliza hivyo. Hao wote hawakujua huyu aliyeleta mada hakujua alichoandika
Ttzo sio kutokujua mleta mada, ttzo ni kusoma na kuelewa andiko.....andiko liliainisha kabisa kuwa hizo sqmts zaidi ya laki 2 zinapatikana kwenye maeneo manne tofauti ila wewe sasa ndo ukawa unalazimisha au kuuliza hizo sqmts laki 2 pale sinza zipo wapi!!!!


Kuna wengi hawatolipwa hata hiyo fidia Kwa sababu maeneo waliyojenga ni ya serikali ndo wamiliki na sio Ile kikatiba kuwa ardhi yoote ni Mali ya serikali bali wamiliki ni idara na wizara za serikali



Mfano kule Basihaya ni eneo lililokuwa linamilikiwa na wizara ya maji kipitia idara ya maji .......kule kunduchi ni eneo lililokuwa linamilikiwa na MECCO km unaikumbuka hiyo kampuni lkn pia kwakuwa pale ilikuwa ni vitalu vya madini ,Sheria inaeleza wazi ukimaliza kuyachimba basi eneo linarudi Kwa serikali na sio wewe kuliuza...........Kwa hapo Sinza eneo kubwa pia lipo chini ya Ttcl kupitia wizara husika




Sijajua kuhusu hilo eneo la mkabala na Mlimani city kutokea kule kilipo chuo Cha ardhi km sijakosea ndo lile eneo la survey
 
Iweke na miundo mbinu itayo wapa wazo watu kuhamia nnje ya mji, mfano ujenzi wa express way dar moro na mengine
Dar inatakiwa kuwa na satellite cities kama tano hivi zinatanuka.

Huku mwisho Kigamboni, huku mwisho Vikindimu kama unaenda Mkuranga, huku Kisarawe, hapo Kibaha unapanua zaidi kutoka barabarani, na kuunganisha Bagamoyo na Dar.

Unapeleka shughuli zote huko watu wengi mpaka wanakosa haja ya kuja mjini Dar, wanakuja mara moja kwa miezi 6 wasiusahau mji tu.

Halafu watu wanaofanya kazi za computer hao unawapa internet ya uhakika tu wanaweza kufanyia kazi kutoka nyumbani hawana hata haja ya kuja ofisini kila siku. Kazi zinaenda kwa email na Project Manager anafuatikia kuhakikisha kila mtu anafanya kazi yake inavyotakiwa. Ukiwa na mtandao wa uhakika na umeme wa kueleweka hiki kinakata sehemu kubwa ya watu wanaohitaji kwenda kazini ohysicalky.

Ila basi watu wanaona haya mambo ya Ulaya na Marekani tu, sisi hatuwezi.
 
Ni ujuaji au ni ubishi aliojipa toka enzi hizo...hakuna kinachoshindikana ......wale wa pale Magomeni kota walifanyiwa hivyo na serikali na leo wamerudi na wanaishi kwenye yale maghorofa


Ikiwa mtu mmoja anaweza kumudu kununua nyumba moja pale kkoo Kwa Tshs billion 6 atashindwa kununua nyumba 26-30 zenye thamani ya mills 200 !!!???


Kuna matajiri wananunua na wanaendelea kununua nyumba maeneo ya Kurasini na baadhi ya maeneo ya vijibweni na darajani kule kata ya Kigamboni wa ajili ya maegesho tuu ndo washindwe kununua maeneo ya Buguruni

Kupanga ni kuchagua ila sio kusema kuwa haiwezekani kutoa hizo pesa kununua maeneo Kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya nyumba za kupangisha
 
Hilo eneo la Survey ni mali ya serikali. Walishalipwa fidia miaka mingi iliyopita. Kulikuwa na ule mradi wa reli kutoka kiwanda cha saruji Wazo Hill mpaka Ubungo. Sijui uliishia wapi.
 
Hii mipango siyo Dar pekee,bali ni nchi Nzima. Tunajenga vichuguu bila mpangilio halafu tunasema tuna nyumba.
Kwa hili la mipango miji, lisiwe la Dar pekee, liwe ni swala la muda mrefu na liwe la nchi nzima. Nchi nzima iwe planned, halafu utekelezaji ufuate taratibu. Na hili lisiwe la CHAMA fulani, bali uwe ni mpango wa kitaifa, kwasababu vyama vinaweza kutoka na vikaja vingine.

Nitasubiri nione, wata excute vipi plan hii, fidia zitalipwaje, na wataondolewaje, watapewa muda gani kuondoka baada ya fidia. Na je watapewa maeneo mapya au watajitafutia baada ya fidia?

Wanaweza kutumia ubabe na ikawa, maana hii ni Tangantika.
 
Hii movie gani unaangalia!?
 
Ongezeko la idadi ya watu, mara mbili kila miaka kumi baada ya 2012 sensa, haliendani na upanuzi wa barabara za Dar ambako sote tunajazana.

Kinachotakiwa kwa Tanroads, kila barabara kubwa mf Morogoro road na Ally Hassan Mwinyi au Mwai Kibaki na kuelekea Mbagala, Kawawa na Mandela na Nyerere Road hadi Chanika inahitaji juu yake kuwe na barabara mbili au tatu zaidi , yaani ngazi tatu mfano wa ubungo interchange iwe kwa njia nzima sio flyover za kwenye junctions tu.

Foleni za Dar hazifai na hatutakiwi kuona ni kitu cha kawaida sababu zinachelewesha sana watu kwenda makazini na kurudisha uchumi nyuma , ajali ni nyingi hasa boda boda na pia foleni zinapunguza wawekezaji wa nje kuja bongo.

Ikifika 2050 nchi ya bongo inaweza kuwa na idadi ya watu milioni 130 na magari yatajaa barabarani Dar bila kusogea maana barabara ni hizi hizi tangu uhuru na watu wenye hali ngumu wanakuja Dar toka bush na wengine hasa huko bush wanazaana kama panya na wengine kununua magari kwa sifa!!

Africa akili zetu zilienda na wakoloni.
 
Umetoa point za maana sana, hongera, lakini Fahamu,
Mapinga pinga chadomo yataanza kuzua maneno ya SHOMBO, ccm songa mbele!...
Katika operation zao wafikirie pia kuitwa VINGUNGUTI.
Mjinga hukimbiiia kutaja vyama badala ya kuelimishwa. Ardhi haina mbadala. Maswali ya msingi lazima yajibiwe. Wamiliki waliopo wanaenda wapi., wanalipwa vipi, je wanabakia hapo kama wabia wa mradi au wanaporwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…