Uko tayari? Dar es Salaam mpya inakuja. Serikali kutwaa eneo la mita za mraba 233,000. Maeneo ya Sinza, jirani na Mlimani City, Boko, SIMU2000 kuguswa

Uko tayari? Dar es Salaam mpya inakuja. Serikali kutwaa eneo la mita za mraba 233,000. Maeneo ya Sinza, jirani na Mlimani City, Boko, SIMU2000 kuguswa

Serikali ya ccm ni ya kijinga sana.Imeshindwa kuipanga Nchi lakini inasubiri watu wabanane na wafanye uwekezaji mkubwa ndiyo ianze kuwafukuza na kujifanya inataka kuendeleza?Ukizunguka Nchi nzima mipango miji ni ya hovyohovyo tu Huku wapangaji wa miji na wizara ya ardhi yanatumbua Kodi zetu.
 
Wala sababu sio rent. Wapo wanalipa rent kubwa chini kuliko ambayo ipo kwenye hizo sky scrappers.

Maghorofa yapo mengi posta na hayana watu, Hilo la demand na supply na kuleta unafuu wa rent mbona bado hakuna watu?

Ukiwa unazungumza haya unapaswa kujua unazungumzia Tanzania ambayo 50% ya population cant afford three meals.

Hilo la government subsidies liondoe maana ni wazo ambao uhalisia wake haupo. NHC wamefanya projects na husema wanaweka subsidies gharama nafuu but still two bedrooms apartment inacosr around mil 200. Nani wa ku afford kulipa mil 200 kwa room mbili?
Huwa nashangaa sana vile vibanda vya NHC kuuzwa kwa bei hizo! Sijui walijenga kwa ajili ya kuuza kwa Wawekezaji wageni! Inashangaza sana.
 
Ni kweli lakini mabadiliko huwa lazima yaanzie mahali, tuwapongeze wote wanahusika kwa nia njema hii! Eka 47 sio mradi mdogo kwa nchi maskini kwa viwango vya namna yoyote mkuu! Nchi yetu ilishakuwa na kimachinga sana. Residential areas zote ni kama slums na hamna miundombinu hata ya fire tu, then kila kona zimejengwa frames tu hamna hata discipline wala mwongozo wowote! Najua wengi sana wataathirika ila pia italeta tabia ya watu kununua maeneo yaliyopimwa sasa sio mashamba pori
Kwani wakjnunua hayo maeneo unayoyaita mashamba pori ni makosa kisheria!? Au ndio uwezo wao ulipoishia!?
 
Ume assume mengi sana ambayo sijasema.

Ume assume nimesema kila mwekezaji wa dunia nzima aje kupewa ardhi hapo. Sijasema hili.

Ume assume nataka wananchi waondolewe hapo. Sijasema hilo.

Ume assume nataka walipwe fidia isiyo market value. Sijasema hilo.

Ume assume sijui kuwa kuna masuala mengine ya uchumi yanayotakiwa kufanyiwa kazi. Sijasema hilo.

Kote humo ume assume wrong.

Mimi Bibi yangu alikuwa na nyumba hapo Sinza si mbali na Mlimani City. Kuna mjomba wangu karithi yupo mpaka leo.

Ukivunja nyumba kama zile tano na kujenga ghorofa 25, halafu pale chini ghorofa ya chini kabisa kukawa na nyumba tano za wale uliowavunjia nyumba wabaki palepale, ukawalipa fidia ya kuvunja nyumba zao (ya sentimental value)halafu uwaache wawe pale ghorofa ya chini wapangishe watu au kutumia kama nyumba au biashara, hapo unahitaji kuwahamisha waende wapi tena?

Huoni kwamba kuwa hapo si tu hujawahamisha, bali pia umewaongezea value sehemu hiyo itakuwa inavutia biashara zaidi, wanaweza kuzidisha rent na wakiamua kufanya biashara wanaweza kufanya biashara kubwa zaidi?
Wilaya ya Kigamboni inazidi kusahaulika kwenye miradi hii mikubwa.
 
Dar inapangwa upya, Sinza inasukwa upya, maeneo jirani na Mlimani City yanasukwa upya. Serikali inaenda kutwaa eneo la ukubwa wa mita za mraba 233,000 na kulipanga upya.

Maeneo kama Sinza yana viwanja vya 20/20, na maeneo hayo kwa sasa ndio ujenzi mkubwa wa maghorofa unakuja. Ni vyema serikali imeyatwaa maeneo hayo ili iyamiliki, ifute ramani ya eneo hilo, ifidie, kisha ilipange upya, na kugawa viwanja vikubwa kwa uwekezaji mkubwa.

Kama ujenzi ungeendelea kwa hali ilivyo, maeneo hayo yangekuwa hayana mvuto, na yenye msongamano.

Hii iende mpaka Tandale kwa awamu, tuipate Dar tunayoitaka.
View attachment 3171283

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI:

View attachment 3171960
Hawa jamaa waache mzaha. Pale Ubungo zamani "Stendi ya Mkoa" wanajenga uchafu TU wa kuuzia takataka za Mchina, Wakati lilikuwa eneo sahihi la kuweka karakana ya mwendo_kasi ile iliyohamishwa Toka bondeni Jangwani. Hii nchi ina ujinga mwingi sana wa viongozi.
 
Dar inapangwa upya, Sinza inasukwa upya, maeneo jirani na Mlimani City yanasukwa upya. Serikali inaenda kutwaa eneo la ukubwa wa mita za mraba 233,000 na kulipanga upya.

Maeneo kama Sinza yana viwanja vya 20/20, na maeneo hayo kwa sasa ndio ujenzi mkubwa wa maghorofa unakuja. Ni vyema serikali imeyatwaa maeneo hayo ili iyamiliki, ifute ramani ya eneo hilo, ifidie, kisha ilipange upya, na kugawa viwanja vikubwa kwa uwekezaji mkubwa.

Kama ujenzi ungeendelea kwa hali ilivyo, maeneo hayo yangekuwa hayana mvuto, na yenye msongamano.

Hii iende mpaka Tandale kwa awamu, tuipate Dar tunayoitaka.

View attachment 3171283

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI:

View attachment 3171960
Yaani serikali is the biggest bully na dhulumati number moja

"maslahi ya umma" which is nonsense hayawezi chukua haki yangu mimi mtu mmoja

yaani haki ya wengi ya kunidhulumu mali yangu halali haiwezi kua halali kuninyang'anya haki yangu

Kwanza wenye viwanja na nyumba zao hapo msihame,fungueni kesi isimamieni mahakamani na uamuzi utatoka baada ya 20years

Nchi hii CCM ikizengua kesi yenu nendeni United Nations

Sio rahisi kuibia watu mali zao eti sababu wewe ni serikali eti "una mradi wa kimkakati",thats nonsense,mradi wako wa kimkakati haukupi jeuri ya kuvamia na kudhulumu watu ardhi zao eti sababu wewe ni serikali halafu eti una "maslahi ya umma"

Huu ni us3ng3 wa ajabu sana

Huwezi watoa wananchi kirahisi hivyo...hapo itakua ni kuvurugana miaka 30 hawahami na sio kirahisi hivyo kwa vi-press release vya hovyo hivi

Ndio maana I really HATE GOVERNMENT!
 
safi sana! Dar ndio New York ya Tanzania.
Kwa wewe kutaka Dar iwe New York hakukupi haki ya kudhulumu watu ardhi zao

Watu wahame kwa hiyari kwa fidia wanazotaka wao,huu ujinga wa hii nchi kua na serikali inayojiamulia maamuzi ya kunyang'anya watu mali zao kwa sababu yeyote ile ikome
 
Wakifanikiwa kuipanga upya kimakazi Dar! Na baadae kufanya haya nchi nzima! Hili linaweza kuwa jambo kubwa zaidi la kimaendeleo kuwahi kufanywa katika nchi hii.

Ila kama kupanga na kuijenga upya waanze na maeneo yaliyojengwa vibaya zaidi kama Manzese, Kigogo, Mbagala, Mabibo na kwingneko. Then ndo waende hayo maeneo mengine.
Mkuu

Ardhi inanyang'anywa wanapewa matajiri na wala serikali haina uwezo wa kufanya lolote maana haina fedha yeyote

Na kudhulumu mali ya wananchi sio kazi ndogo,hapo kesi itaunguruma miaka 30 uamuzi ndio utoke

Huwezi jiamulia eti unaamka asubuhi unataka kuchukua maeneo ya watu kisa eti unataka pawe New York sijui blah blah...huu udhulumati unaofanywa na serikali UISHE
 
Tanzania haikuumbwa kwa ajili ya kila mwekezaji dunia nzima kuja kupewa ardhi hapa.

Hao wananchi unaoshabikia wanyang'anywe ardhi zao uelewe maisha yao ya kiuchumi na kijamii yamefungamanishwa na mahali hapo wanapotaka kuhamishwa. Hivyo kitendo cha kuwaondoa hapo tu hata kama wanalipwa fidia kwanza hiyo fidia sio market value na haiwawezeshi kupata naeneo mengine yenye hadhi sawa na hapo hivyo watarudishwa nyuma kiuchumi na mfumo wao wa maisha utavurugika. Mtu aliyekuwa anapangisha nyumba yake sinza na kuingiza kipato tayari anerudi katika umaskini mkubwa.

Pili hao watu wanaohamishwq wanaenda wapi na kwa gharama za nani?

Kinachofanya makazi yawe duni ni hali za kiuchumi za wananchi hivyo hata majengo ya kisasa, yakijengwa bado kama mtu hana kipato kikubwa hataweza kupanga na kuishi.

Hii sheria ya ardhi inayoruhusu mwananchi kunyang'anywa ardhi yake kwa manufaa ya umma ilipaswa kubadilishwa.
Ukihamishwa na serikali huwez rudi nyuma kiuchumi, hata siku moja
 
Dar inatakiwa kuwa na satellite cities kama tano hivi zinatanuka.

Huku mwisho Kigamboni, huku mwisho Vikindimu kama unaenda Mkuranga, huku Kisarawe, hapo Kibaha unapanua zaidi kutoka barabarani, na kuunganisha Bagamoyo na Dar.

Unapeleka shughuli zote huko watu wengi mpaka wanakosa haja ya kuja mjini Dar, wanakuja mara moja kwa miezi 6 wasiusahau mji tu.

Halafu watu wanaofanya kazi za computer hao unawapa internet ya uhakika tu wanaweza kufanyia kazi kutoka nyumbani hawana hata haja ya kuja ofisini kila siku. Kazi zinaenda kwa email na Project Manager anafuatikia kuhakikisha kila mtu anafanya kazi yake inavyotakiwa. Ukiwa na mtandao wa uhakika na umeme wa kueleweka hiki kinakata sehemu kubwa ya watu wanaohitaji kwenda kazini ohysicalky.

Ila basi watu wanaona haya mambo ya Ulaya na Marekani tu, sisi hatuwezi.
Mtogo mtodo tu, ujue ukienda kijini flan hapao karibu na dar, ukachongo barabara ukaweka lami, maji, na umeme mwezi mmoja tu viwwanja vinanunuliwa vyote na kuna jaa,
Shida selikari yetu inaamini inchi itajegwa na wawekezaji kutoka njee kumbe si kweli, kukuwa kwa mji selikali lazima itie mikono hasa miundo mbinu, barara nzuri, umeme, na maji mengi, na internet
 
Mtogo mtodo tu, ujue ukienda kijini flan hapao karibu na dar, ukachongo barabara ukaweka lami, maji, na umeme mwezi mmoja tu viwwanja vinanunuliwa vyote na kuna jaa,
Shida selikari yetu inaamini inchi itajegwa na wawekezaji kutoka njee kumbe si kweli, kukuwa kwa mji selikali lazima itie mikono hasa miundo mbinu, barara nzuri, umeme, na maji mengi, na internet
Naam.

Ukiangalia miji mikubwa utaona kuna sehemu zinaonekana mbali na mji hapo Dar, kumbe kiuhalisia ni suburbs za Dar tu.
 
Back
Top Bottom