Ukokotoaji wa bei ya petroli kwa mwezi June baada ya ruzuku ya Sh 100 billion huu hapa: Bei inapaswa kupungua kwa zaidi ya asilimia 60%

Ukokotoaji wa bei ya petroli kwa mwezi June baada ya ruzuku ya Sh 100 billion huu hapa: Bei inapaswa kupungua kwa zaidi ya asilimia 60%

Boss,Hizi hesabu mnazopiga zote zinachukulia kuwa hiyo ruzuku ya 100bn ni kwa mwezi June tuu.Kama hivyo ni sahihi maana yake kuanzia July tutarudi kwenye bei za kawaida bila ruzuku!?
Ndo hivyo?
Bunge la bajeti ya mwaka unaoanzia Julai mosi 2022 hadi 30 June 2023 litapanga hizo pesa za ruzuku na kiasi chake.
 
Kama umenisoma vizuri,retail price haitazidi TSh 1,500 kwa nchi nzima.
Hizi tofauti za bei za mkoa kwa mkoa huwa ni ndogo sana. Kwa mfano kama DSM diesel inauzwa Sh 3,200, kwa Mwanza itauzwa Sh 3,360. Tofauti hizi EWURA wangaliweza kuziondoa kwa kutafuta wastani wa bei kwa sehemu zote za nchi kama yanavyofanya makampuni ya bia na ya soda. Bei ya bia DSM na Morogoro ni ile ile.

Pia reli ingalitumika kusafirisha bidhaa hii muhimu badala ya malori ya tankers. Usafirishaji wa kutumia malori kwa bidhaa hii ni wa hatari sana, EWURA inapaswa kuupiga marufuku. Hii kwanza itaimarisha shirika letu la reli kiuchumi. Tatizo malori haya mengine ni ya vigogo serikalini, mama anapaswa kusimama imara. Usafirishaji kwa njia ya reli ni rahisi mara dufu ukilinganisha na wa barabara na SGR itakapokamilika, ni usafiri wa haraka zaidi kuliko wa barabara. SGR ya kutoka DSM hadi Morogoro itakapokamilika hivi punde. Hatutarajii hata kidogo kuona bidhaa hii ikisafirishwa kwa barabara kwenda Morogoro kutoka DSM baada ya hapo.
Kwa maroli ajira watch out
 
Back
Top Bottom