Ile ngazi waliyoitumia wazungu kupandia juu waliko kiuchumi wameiondoa na kuificha na pengine wameichoma moto kabisa.
Kiuchumi wazungu walifika pale walipo kwa kufunja haki za binadamu na kwa kukanyaga sheria na demokrasia. Walikusanya mitaji ya uwekezaji kwa kutumia njia zisizokubalika kama vile kupora makoloni, kufanyakazi kwa masaa mengi bila kujali umri kwa ujira mdogo, walitumia watumwa bure na kukanyaga demokrasia na usalama pahala pa kazi. Hawakuwa na malipo ya ajali kazini au pension.
Walipohakikisha kuwa wao tayari wana uhakika wa mitaji na masoko duniani wakatulazimisha sisi wadogo kabisa tujali haki za binadamu, demokrasia, usalama kazini, malipo ya ajali kazini, uhuru wa kuabudu, mifuko ya kijamii ya pension, kulipia huduma za kijamii kama shule, hospitali, maji, nk. Nchi zetu hizi changa haziwezi kupiga hatua kimaendeleo kama zitakumbatia uhuru wa sheria, democrasia, usalama kazini, utunzaji wa mazingira, haki za binadamu, uhuru wa kuandamana, vyama vingi, uchaguzi kila miaka 5, nk. Tutatumia muda na rasilimali nyingi sana Afrika kuhangaikia mambo hayo.
Nchi kama za China, N Korea, Asia ya kati, Asia ya mbali, Rwanda, nk zinapiga hatua kiuchumi kwa kuachana na mambo ya haki za binadamu, utawala wa sheria, democrasia, nk. China ina watu zaidi ya 1 bn, kama wakiruhusu demokrasia haitatawalika na watashindwa kuwalisha.
Kenya ni taifa dogo sana, demokrasia, sheria, haki za binadamu, malipo halali kwa wafanyakazi, nk ni ghali sana to undertake kwenye ulimwengu ambao masoko yote yanadhibitiwa na wazungu. Utapata wapi fedha za kuendeshea mfumo wa vyama vingi, sheria, bunge, na serikali?. Jaji anasema uchaguzi ufutwe maana yake taifa litumie hela na muda tena kurudia uchaguzi huku wananchi hawana maji, umeme, madawati shuleni, chakula, madawa, barabara, madawati. Hatuwezi kuendelea milele, na hii sio kwa bahati mbaya bali tulitegeshewa na wakoloni ili tusiende mbele.