Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Nami ilishanikuta na sasa nina maamuzi kama yako ya kutokopesha zaidi ya elfu 20.

Ila mimi niliwakomalia sana mpaka wakalipa
 
Inatia hasira lakini cha kujifunza Mimi kwa Sasa mtu simkopeshi, ukinililia huna Pesa ya kula bora nikununulie kiroba cha unga na kilo kadhaa za dagaa Nikuongeze na elfu kumi sikudai

Ukinijia unalia Pesa ya rejesho kwa kweli Sina

Sijui watoto wamefukuzwa shule nikopeshe Ada jibu ni Sina.

Kama unamgonjwa nitajua namna ya kukusaidia.

Ila sikopeshi Wala sidhamini mtu awe ndugu, Jirani Wala rafiki.
 
Rafiki yangu mmoja nilimkopa Laki Sita May 2017. Alikuwa nje ya mji na mkewe akapata emergency, akihitaji hiyo pesa. Kwa kuthamini urafiki wetu, nilimtumia fasta, na elfu kumi juu ya ''kutolea''. Huyu hajalipa mpaka leo. Mwingine alikuwa staff member na akaomba nimkope Laki Nane kwa kuwa alikuwa na shida ya kutoa kagari kake kapya bandarini. Ilikuwa June mwaka jana. Hajalipa mpaka leo.

Jambo la ajabu sasa, naona kama urafiki wetu umetetereka pakubwa sana kwa wote wawili. Sio kwamba nawasumbua kwa kuwadai, la hasha. Naona mmoja yeye hata nikichat nae, ule ukaribu wetu wa zamani haupo tena. Sasa hivi simuoni kabisa WhatsApp na nimeambiwa kabadilisha namba. Huyu wa Laki nane zaidi ya mara mbili amepokea simu zangu na kusema ''nipo busy/meeting mkuu, ntakucheki baadae buddaaa...''. Hakunicheki mpaka kesho kutwa. Last time nilitaka kumpa mchongo wa kazi moja hivi lakini alivyoyeyusha, deal nimempa mwingine.

Anyway, kopa mtu fedha at your own risk. Kwa kuwa ninathamimi sana urafiki, mwaka huu sintomkopa fedha mtu au rafiki yangu yeyote. Kama ni fedha kidogo na nimesukumwa na shida ya mtu, nitatoa msaada bure na halitakuwa deni. As for the two gentlemen, nimeshawasamehe moyoni ila sitawaambia na itakaa iwatese tu.

Kamwe usiazime ama kukopa fedha kwa mtu ambaye huhitaji kukosana naye ama kupoteza urafiki na ukaribu naye kabisa.Kama una uhakika hutoweza kupoteza urafiki na ukaribu naye basi unaweza kufanya hivyo.Kumbuka nyakati kama hizi deni linaweza kuzaa uadui wa kizazi na kizazi!!
 
Mm kuna rafiki na ndugu zangu nimewakopesha... Mimi mtu alikuwa akija kwa lengo la kukopa ninampa aijalishi ni shilingi ngapi so Nina list ndefu kuanzia 10,000/= hadi 2m. Ilipofika January 5 mwaka uhuu nilijitathimini nikakuta pesa ambayo siwezi kuipata niliyokopesha ni zaidi ya 2.5m. Nilichukua kalamu na kufuta majina ambayo wahusika wameshayumba kiuchumi na awawezi kurudi Leo au kesho kwenye line...... Ninachomshukuru Mungu mm mipango yangu inazidi kunyooka Ila walionikopa na kunitapeli wanazidi kusambaratika kiuchumi Alafu kwa sababu walishaharibu awapati ujasiri wa kuniazima pesa hata kunipigia simu awawezi wanaogopa ninawacheka kimoyomoyo...... Kuna rafiki yangu alinikopa laki Tano may 2017 alikuwa yupo vizuri kiuchumi Sana.... Lakin Sasa hiv had Gari ameuza anasaga soli tu.....
 
Back
Top Bottom