KERO Ukosefu wa huduma muhimu ya maji na intaneti hosteli za UDSM za wanafunzi wa Masters na PhD ni mateso makubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

JOKA ZEE

New Member
Joined
Jul 5, 2024
Posts
1
Reaction score
8
Hostel ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam tawi la Ubungo kuna matatizo mengi yanawakumba wanafunzi.

Moja kati ya matatizo hayo ni upatikanaji wa maji. Hostel ya Ubungo licha ya kukaa zaidi wanafunzi wa master na PhD lakini tatizo la upatikanaji wa maji unasumbua sana.

Maji yanayopatikana hapo ni ya Serikali ambapo yanatoka kwa wiki siku 2 au siku 3 jambo ambalo wanaoishi hapo wanaishi kwa shida.

Matanki ya kuhifadhia maji ni madogo mno na yanawafanya wakazi wa hapo kutembea na ndoo wanapokwenda na kurudi vyooni kama wakazi Kinyangara ya juu huko Tabora.

Vyoo ni vichafu sana na vinanuka sana kwa sababu hakuna maji. Jambo la kufanya ni kuchimbwa kisima ili maji masaa 24 katika mabomba ya vyooni yanapatikana na sio kama hivi sasa ukienda chooni ubebee ndoo.

Jambo la pili ni internet. Jengo halina internet kabisa na wanafunzi wanaoishi hapa wanafanya tafiti na wengine na wanataka kujisomea.

Jengo limekosa kabisa huduma hiyo ambapo maisha yamekuwa magumu. Makazi haya hayapo Iringa milimani, yapo mjini kabisa karibu kabisa na Ubungo Plaza.

Kwa leo ni hayo tu
 
Wewe ni masters au Phd ?
Tuanzie hapo kabla ya tatzo lenyewe...
 
Hamien nit
 
Nimekaa hapo nilipokuwa nafanya masters yangu,uongozi wa hicho chuo ni zero kabisa.
Sijui hicho chuo kinashindwa nini kuandikia kwenye bajeti wapatiwe fedha za kuchimba visima katika hostel za Wanafunzi.
 
Sikuwahi kujua ya kwamba mwanafunzi wa PHD anakaa hosteli za chuo! Mshamba Mimi!!!!
 
Kwanini unaandika kwa kutudharau na kutukashfu sasa isi wakazi wa Tabora na wa Iringa Milimani. Nawe ndio msomi wa Master's au PhD kama usemavyo unashindwa kuwasilisha hoja zako bila kashfa. Endeleeni kunya kwenye vifungashio hapo UDSM na hatutaleta maji sasa.

Unasoma Master's au PhD alafu unalilia internent. Unashindwa kununua bundle hata la jero utafute material mtandaoni. Wenzako tulisoma na kufanya research zetu kwa kutumia four figure we unadowload kila kitu mtandaoni.

Kilaza mkubwa.
 
Acha ujuaji, jadili mada ambayo inafikirisha sana. Hawapaswi kabisa kukosa huduma ya internet.
Zinasaidia nini kwenye masomo hizo huduma za internet. Mbona sisi tuliosoma Msc kipindi hiko SUA wakati hakukuwa na internet tulisoma vizuri tu.

Internet zinawadumaza nkuwafanya wawe vilaza hao wanafunzi wa kisasa. Wanashindwa kununua bundle binafsi? Hizo WiFi ndio wanatumia kuangalia video za ngono na kudownload movie tu hakuna lolote.
 
 
Bado hizo huduma za uhakika za internet zinahitajika sana kwenye hizi taasis za elimu. Inawezekana mtoa mada amekukera kwa maneno yake lakini serikali imefeli sana kwenye uwekezaji kwenye software infrastructure.
 
Four figure tables na slide rules - Muuza madafu wa Ikulu utakuwa babu kama mimi!
 
Bado hizo huduma za uhakika za internet zinahitajika sana kwenye hizi taasis za elimu
Mkuu unafeli sana kushindwa kuona kuwa dunia ilishatoka huko ulikosomea wewe. Huwezi kuikwepa internet kwenye ulimwengu wa sasa. Kama kuna watu wanatumia WiFi kuangalia ngono bado haiondoi umuhimu wa kipekee wa huduma hiyo kwenye ulimwengu wa sasa. Hii ni dunia ya internet kwenye kila sekta, Afrika bado tunambwela mbwela.
 
Four figure tables na slide rules - wewe utakuwa babu kama mimi!
Hahaaaaa sasa wanalilia Internet mkuu. Kila kitu kinakuwa copied toka mtandaoni.

Juzi kuna mmoja kaja ofisini kwangu akaomba anihoji kama mzimamizi wa Ofisi anafanya utafiti wake, akaniambia "research title yake" nikamwambia mbona hii Tittle yako kuna mmoja alishakuja hapa na Title hii hii na akanihoji toka chuo fulani na akanihoji maswali kama haya yako na aligraduate mwaka jana? Akajingatangata nikamuonea huruma na kumruhusu anihoji atajua mwenyewe huko.

Wakija maofisini mbwembwe nyingiiii nina Master's na blah blah ila mwambie asimame ajielezee. Utaona aibu.
 
Hahaaaaa, siku hizi hata kuchakata data zenu mnazozipika imekuwa rahisi sana. πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜ kila kitu kinafanyika mtandaoni.

Ukishamaliza kupika data za uongo na kuokoteza material mtandaoni na kupewa cheti chako cha Master's njoo kwenye "utendaji ni zero". Master's inatakiwa ireflect utendaji wako ila hadi huruma. Mtu ana Master's ila kujieleza kiswahili hawezi wala kiingereza hawezi. Mtu ana Master's ila kuandika taarifa na reports za hata page 1 hawezi. Tunao maofisini, tunao mitaani inasikitisha sana. Mungu awasaidie.
 
Internet si wote wanaitumia kwa matumizi chanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…