KERO Ukosefu wa huduma muhimu ya maji na intaneti hosteli za UDSM za wanafunzi wa Masters na PhD ni mateso makubwa

KERO Ukosefu wa huduma muhimu ya maji na intaneti hosteli za UDSM za wanafunzi wa Masters na PhD ni mateso makubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Masters na Phd unawezaje kutegemea Wi-fi ya chuo na kukaa Hostel? Au elimu ya kibongo imekuwa ya kijinga
 
Hostel ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam tawi la Ubungo kuna matatizo mengi yanawakumba wanafunzi.

Moja kati ya matatizo hayo ni upatikanaji wa maji. Hostel ya Ubungo licha ya kukaa zaidi wanafunzi wa master na PhD lakini tatizo la upatikanaji wa maji unasumbua sana.

Maji yanayopatikana hapo ni ya Serikali ambapo yanatoka kwa wiki siku 2 au siku 3 jambo ambalo wanaoishi hapo wanaishi kwa shida.

Matanki ya kuhifadhia maji ni madogo mno na yanawafanya wakazi wa hapo kutembea na ndoo wanapokwenda na kurudi vyooni kama wakazi Kinyangara ya juu huko Tabora.

Vyoo ni vichafu sana na vinanuka sana kwa sababu hakuna maji. Jambo la kufanya ni kuchimbwa kisima ili maji masaa 24 katika mabomba ya vyooni yanapatikana na sio kama hivi sasa ukienda chooni ubebee ndoo.

Jambo la pili ni internet. Jengo halina internet kabisa na wanafunzi wanaoishi hapa wanafanya tafiti na wengine na wanataka kujisomea.

Jengo limekosa kabisa huduma hiyo ambapo maisha yamekuwa magumu. Makazi haya hayapo Iringa milimani, yapo mjini kabisa karibu kabisa na Ubungo Plaza.

Kwa leo ni hayo tu
1. Humo ndani Kuna kisima na pump, imekuaje?
2. Mataqo baa bado upo?
3. Humo ndani tulikua tunaingiza Malaya Hadi walinzi wanaanza kituzuia,
4. Bila maji Hadi game hau-enjoy.
 
Hahaaaaa, siku hizi hata kuchakata data zenu mnazozipika imekuwa rahisi sana. 😀😃😄😁 kila kitu kinafanyika mtandaoni.

Ukishamaliza kupika data za uongo na kuokoteza material mtandaoni na kupewa cheti chako cha Master's njoo kwenye "utendaji ni zero". Master's inatakiwa ireflect utendaji wako ila hadi huruma. Mtu ana Master's ila kujieleza kiswahili hawezi wala kiingereza hawezi. Mtu ana Master's ila kuandika taarifa na reports za hata page 1 hawezi. Tunao maofisini, tunao mitaani inasikitisha sana. Mungu awasaidie.
Seriously unawabeza kwa kutumia mtandao? Mtandao sio tu unapanua wigo wa data na knowledge unayoweza kutumia katika research yako. Mtandao unakupa uwezo wa kuongeza ujuzi katika nyanja yako bila kuingia darasani. Mtandao unakuwezesha kujua nani mwingine anafanya research katika eneo lako na hivyo kukuwezesha kushirikiana nae. Plagiarism enzi hizi za mtandao ni ngumu kwa sababu kuna app kibao ambazo zimejikita katika kupanda nao. Aidha, ukichukua sehemu ambayo mtu ameandika ukaitafuta mtandaoni, kama kuna mwengine aliyewahi kuiandika utajua tu. Hii ni tofauti na ule wakati ambapo mlikuwa mnaandika thesis zenu kwa mkono.
Kitu kingine ni gharama ya vitabu. Hapo zamani watu walikuwa wanapewa vitabu bure. Siku hizi wanapaswa kununua vya second hand kwa bei mbaya. Ukiwa na mtandao, unaweza kupata e-books nyingi kwa bei nafuu. Ili kuvi download unahitaji mtandao uliokaa vizuri.

Badala ya kuwabeza kuwa wasomi wa siku hizi hawawezi kuandika report, zibeze shule zilizowaelimisha ambako bila shaka utakuta maprofesa wake nao walisomea slide rule. Shida ni mfumo wetu wa elimu,vsio wanafunzi.

Tuwe gracious katika kukosoa. Tusitake watoto wetu wasivae viatu kwa vile sisi hatukuvaa.

Amandla...
 
Zinasaidia nini kwenye masomo hizo huduma za internet. Mbona sisi tuliosoma Msc kipindi hiko SUA wakati hakukuwa na internet tulisoma vizuri tu.

Internet zinawadumaza nkuwafanya wawe vilaza hao wanafunzi wa kisasa. Wanashindwa kununua bundle binafsi? Hizo WiFi ndio wanatumia kuangalia video za ngono na kudownload movie tu hakuna lolote.
Ulimwengu kiganjani 22nd century
 
PhD anakaa hostel!?mbona mnadeka sana PhD
PhD na masters inatakiwa unakaa mahali kwenye ka apartment hata ka laki na nusu mahali ila hostel tena hapa mjini hapana.
Anyway ushauri wako wa kuchimba kisima ni mzuri
Acha kukariri kwaiyo wewe unaona Masters ni issue kubwa sanaa ambao hawez kukaa hostel.
 
Back
Top Bottom