KERO Ukosefu wa huduma muhimu ya maji na intaneti hosteli za UDSM za wanafunzi wa Masters na PhD ni mateso makubwa

KERO Ukosefu wa huduma muhimu ya maji na intaneti hosteli za UDSM za wanafunzi wa Masters na PhD ni mateso makubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hayo labda ndo matumizi yako ukipata internet.
Kwa Dunia ya sasa hata hostel za undergraduate zilifaa ziwe na internet.
Kuitumia kujijenga au kujibomoa ni maamuzi ya mtu binafsi.
Nyie mnaoshindia kubet mna nini zaidi ha kuangalia ngono. Kama mnapewa Boom mna betia, hiyo internet mtaangalia nini la maana? Pathetic and idiotic generation
 
Nyie mnaoshindia kubet mna nini zaidi ha kuangalia ngono. Kama mnapewa Boom mna betia, hiyo internet mtaangalia nini la maana? Pathetic and idiotic generation
Hunijui hata chembe ila unaandika kama vile unanifahamu.
Kama unashindwa kutambua umuhimu wa internet kwa ngazi ya postgraduate basi hata uwezo wako wa kuja na mawazo chanya ni mdogo.
 
Hahaaaaa sasa wanalilia Internet mkuu. Kila kitu kinakuwa copied toka mtandaoni.

Juzi kuna mmoja kaja ofisini kwangu akaomba anihoji kama mzimamizi wa Ofisi anafanya utafiti wake, akaniambia "research title yake" nikamwambia mbona hii Tittle yako kuna mmoja alishakuja hapa na Title hii hii na akanihoji toka chuo fulani na akanihoji maswali kama haya yako na aligraduate mwaka jana? Akajingatangata nikamuonea huruma na kumruhusu anihoji atajua mwenyewe huko.

Wakija maofisini mbwembwe nyingiiii nina Master's na blah blah ila mwambie asimame ajielezee. Utaona aibu.
Kwa mwandiko huu? Una ofisi ya kufuatwa na mtu wa PhD?
Shikamoo jf 🙌
 
Internet si wote wanaitumia kwa matumizi chanya
Kutumika kwa Uranium kutengenezea silaha za maangamizi hakuwezi kuhalalisha kufungwa kwa migodi yake. Na ndo imefanya baadhi ya nchi kufuta mawazo ya kukosa umeme kwa wanachi wao.
Kutumia nyenzo yoyote kwa uzuri au ubaya ni maamuzi ya mtumiaji mwenyewe. Internet nayo ni hivyo hivyo. Unaweza kuitumia utakavyo, ila it's one of the greatest inventions of our time. Trillions of dollars revolve around it.
 
PhD bado unalia shida ya makazi na unataka internet ya bure? kazi ipo hapo jalalani..Waziri anataka internet ya bure

Inasikitisha. Ukiwamaliza HAMAS akina Malaria 2 njoo uwamalize hawa wenye PhD za mchongo akina Mama Abdul😀😃😄😁
Wewe umeshia std 7 , umetoka kijijini umeenda mjini kuuza machungwa unajifanya una mdomo. HAMAS ni wanaume wanapigana na USA, NATO na wengine. sio kama nyinyi chadema mpira wa baskeli ukipasuka tu mnakimbilia mvunguni
 
Hostel ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam tawi la Ubungo kuna matatizo mengi yanawakumba wanafunzi.

Moja kati ya matatizo hayo ni upatikanaji wa maji. Hostel ya Ubungo licha ya kukaa zaidi wanafunzi wa master na PhD lakini tatizo la upatikanaji wa maji unasumbua sana.

Maji yanayopatikana hapo ni ya Serikali ambapo yanatoka kwa wiki siku 2 au siku 3 jambo ambalo wanaoishi hapo wanaishi kwa shida.

Matanki ya kuhifadhia maji ni madogo mno na yanawafanya wakazi wa hapo kutembea na ndoo wanapokwenda na kurudi vyooni kama wakazi Kinyangara ya juu huko Tabora.

Vyoo ni vichafu sana na vinanuka sana kwa sababu hakuna maji. Jambo la kufanya ni kuchimbwa kisima ili maji masaa 24 katika mabomba ya vyooni yanapatikana na sio kama hivi sasa ukienda chooni ubebee ndoo.

Jambo la pili ni internet. Jengo halina internet kabisa na wanafunzi wanaoishi hapa wanafanya tafiti na wengine na wanataka kujisomea.

Jengo limekosa kabisa huduma hiyo ambapo maisha yamekuwa magumu. Makazi haya hayapo Iringa milimani, yapo mjini kabisa karibu kabisa na Ubungo Plaza.

Kwa leo ni hayo tu
dah
 
Intaneti? Kuna Mbu sana uko Daslam eeh mpaka na hiyo iwe huduma Muhimu kiiasi iko?
 
Jengo limekosa kabisa huduma hiyo ambapo maisha yamekuwa magumu. Makazi haya hayapo Iringa milimani, yapo mjini kabisa karibu kabisa na Ubungo Plaza.
Billion 900 zimetengwa kwa ajili ya Magari yao nyinyi mnaishi MJINI mnakunya vichakani ndoo Mkononi hakuna Maji km mpo Bariadi huko ndanindani mnakunya vichakani kumbe ni Ubungo MJINI kabisa hapo na idara ya Maji haipo mbali na hapo, huu ni uzembe wa uongozi wa Chuo au uzembe wa nani? Au ndio maana yule Bwana alipaita JALALANI? Sasa pamegeuka CHOONI vyoo vinanuka?

Nitakushauri Jambo usijitambulishe hata Jina hao mamwehu wakikujua huna Chuo watakufukuzisha Chuo
 
Kwanini unaandika kwa kutudharau na kutukashfu sasa isi wakazi wa Tabora na wa Iringa Milimani. Nawe ndio msomi wa Master's au PhD kama usemavyo unashindwa kuwasilisha hoja zako bila kashfa. Endeleeni kunya kwenye vifungashio hapo UDSM na hatutaleta maji sasa.

Unasoma Master's au PhD alafu unalilia internent. Unashindwa kununua bundle hata la jero utafute material mtandaoni. Wenzako tulisoma na kufanya research zetu kwa kutumia four figure we unadowload kila kitu mtandaoni.

Kilaza mkubwa.
Sasa broo una akili kweli yaan masters na phd holder bando la jero unajielewa kweli au ndo mnajitoa ufahamu unajua kusoma online wew unaweza soma 30hrs kwa bando la jero au ukishiba magimbi unaanza kashfa
 
Nimekaa hapo nilipokuwa nafanya masters yangu,uongozi wa hicho chuo ni zero kabisa.
Sijui hicho chuo kinashindwa nini kuandikia kwenye bajeti wapatiwe fedha za kuchimba visima katika hostel za Wanafunzi.
Masters ya uongozi nayo ni degree?
 
Back
Top Bottom