KERO Ukosefu wa huduma muhimu ya maji na intaneti hosteli za UDSM za wanafunzi wa Masters na PhD ni mateso makubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Pesa zinaliwa
 
Mwanafunzi wa PhD analalamikia upatikanaji wa internet! Wasomi mnasomaga Nini Kama mpaka level hiyo Bado hamuwrzi hata kubuni mbinu mbadala ya internet
 
Na kweli wewe mshamba haswa. Nchi gani duniani ambako hakuna hostel za wanafunzi wa post-graduate? au ukisikia hostel unakuwa na picha gani kichwani?
Nilikwenda kusoma mahali. Kulikuwa na graduate students village. Nikawa najisemea dah nakwenda kukaa bwenini. Kuingia ni two bedrooms halafu viko full furnished utafikiri hotelini. Kila kitu kipo ndo nikajua hawa watu wapo siriazi na mambo yao aisee.

Hivi kwa nini sisi hata mambo madogo tu hatuwezi? Inakuwaje vigumu kuhakikisha kwamba kuna maji ya kutosha katika hosteli za graduate students? Hapo ukute fungu lilishatolewa mtu akapita nalo.

Halafu wanafunzi wa PhD wanalalamika vyoo kunuka huku wakisingizia ukosefu wa maji. Ukienda kuangalia si ajabu ukakuta kumejazwa magazeti na makorokocho mengine. Na hawa ni wanafunzi wa PhD!

Sisi kusema kweli bado! πŸšΆπŸΏβ€β™‚οΈπŸšΆπŸΏβ€β™‚οΈπŸšΆπŸΏβ€β™‚οΈ
 
Shalom ya vyoo kwa UDSM ni kubwa sana…..

Kuna vyoo Vipo pale Nkrumah,SR’s,Theaters etc. kiukweli hali ya vile vyoo ni mbaya sana

Kuna muda unaenda chooni unakuta vinyesi vya watu wazima,wamejisaidia halafu wakashindwa kuflash kwa sababu maji hakuna na vyoo vinatoa harufu kali sana Kama vyoo vya soko

UDSM vyoo ni vya pale maktaba mpya(japo na vyenyewe vinakwenda kuharibika soon kutokana na uangalizi hafifu)na kule Confucius institute pekee
 
Hilo la competency ya wahitimu wetu pengine halina uhusiano kabisa na kuwepo kwa intaneti. Linaweza kuwa limesababishwa na mitaala yetu na namna tunavyowaandaa na kuwatunza walimu wetu kwa ngazi zote. Aliyeleta hii mada ana hoja ya msingi sana na ambayo haikwepeki kabisa, uwepo wa huduma za internet za uhakika na ambazo watu wataweza kuzimudu.
Kwa taasisi za elimu ya juu na taasisi zingine zote bila ya kusahau umma kwa ujumla wake, huduma ya intaneti ni ya lazima na ya muhimu sana, vinginevyo tuendelee kupiga ramli chonganishi tu.
 
PhD na Master m akaa chuo. Hapana kapangeni mjifunze Maisha.
 
Mpaka mwenye PhD hawezi kujieleza
 
Sijaelewa vzr mkuu,, unalalamika kwa sababu hakuna huduma tajwa au kwa kuwa hiyo huduma wanaokosa ni wanafunzii wa uzamivu na uzamiri
 
Hayo labda ndo matumizi yako ukipata internet.
Kwa Dunia ya sasa hata hostel za undergraduate zilifaa ziwe na internet.
Kuitumia kujijenga au kujibomoa ni maamuzi ya mtu binafsi.
 
PhD anakaa hostel!?mbona mnadeka sana PhD
PhD na masters inatakiwa unakaa mahali kwenye ka apartment hata ka laki na nusu mahali ila hostel tena hapa mjini hapana.
Anyway ushauri wako wa kuchimba kisima ni mzuri
sasa unataka akakae baa? Tatizo la watz ndio hivyo, akipata kimaster chake anajiona hawezi kukaa hostel. Nchi zilizoendelea hayo mambo yapo, hujatembea ndio maana unasema .
 
Watakuwa wa st J hao, wa MUM wapo vizuri
 
PhD bado unalia shida ya makazi na unataka internet ya bure? kazi ipo hapo jalalani..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…