Ukraine ipo tayari kwa lolote, wananchi wake wataingia vitani kupigana na majeshi ya Urusi

Ukraine ipo tayari kwa lolote, wananchi wake wataingia vitani kupigana na majeshi ya Urusi

Korofi ni NATO,, baada ya vita baridi walikubaliana NATO na warsaw pact zivunjwe ,, mrusi akatimiza,, marekani na wenzake wakaendelea na NATO huku wakinyakua nchi kuizunguka Russia,,
Russia wamestuka kusa wanazidi kuzungukwa tu, ndiposa wameweka jeshi tayari
Sasa Russia kwa nini apate tabu si awe tu mpole kisha atume maombi aruhusiwe kujiunga na Nato. If you can't beat them join them.
 
Sasa Russia kwa nini apate tabu si awe tu mpole kisha atume maombi aruhusiwe kujiunga na Nato. If you can't beat them join them.
Tabu ni kuwa Russia can beat them all
 
Urusi ni nani wa kuyaamulia mataifa mengine yaungane na nani au yasiungane na nani, huo ni upuuzi ambao hakuna anayeweza kuukubali.
Hata wamarekani hawawezi kukubali , Russia iweke kambi za jeshi cuba,, au mexico, etc
 
Urusi ni nani wa kuyaamulia mataifa mengine yaungane na nani au yasiungane na nani, huo ni upuuzi ambao hakuna anayeweza kuukubali.
kwani US nayeye ninani anapowaamulia wenzie hiki wafanye hiki wasifanye
UKRAINE hatakaa ajiunge na NATO kwausalama wa NATO na UKRAINE yenyewe
 
Ukraini imeamua sasa kufundisha wananchi wake na kuongeza jeshi la akiba hata na lisilo na akiba.kwa ajili lolote litakalo tokea na mzozo huu baina mbili kati ya ukraini na vikosi vya Urusi.

View attachment 2106112
nafikiri wanahitaji diplomasia tu, kwasabbu watajikuta wameingia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. unajua Urusi alichokifanya, kuna eneo kule Ukraine hasaa wanakopakana na urusi, kuna watu wengi sana ambao asili yao ni urusi, yaani ni warusi wanaoishi ukrane, ni kama watusi wanaoishi congo. na mara zote huwa wanaisapoti urusi against ukraine wakati wanaishi palepale ukraine. na urusi ndio anawatumia sana kama maspy wake. unaishi na raia ambaye asili yake sio nchi yako na anampenda adui kuliko wewe. na mara nyingi hao waukraine wenye asili ya urusi wakionewa tu na ukraine, russia huwa anasema anataka kuivamia ukraine ili kuikoa maisha ya raia wa ukraaine wenye asili ya russia. ni kipanzi ambacho kipo kwenye jicho la ukraine maisha yake yote. na kuna siku wakiamua watajimega tu na kuhamia urusi, that means watamega ardhi ya ukrain kuhamia urusi. hivyo akijifariji kupigana na urusi ajue ataanza kupigana na raia wake mweneywe ambao pia wamesamba ukrain yote.
 
kwani US nayeye ninani anapowaamulia wenzie hiki wafanye hiki wasifanye
UKRAINE hatakaa ajiunge na NATO kwausalama wa NATO na UKRAINE yenyewe
Ukraine lazima atajiunga na Nato na ni swala la muda tu. Wachovu Russia hawawezi kupigana vita, njaa itawaua kuliko vita yenyewe.
 
Failure state,unaota Mkuu kawaulize NATO na USA kuhusu hili.
Ili uitawale hii dunia kwa amani ni lazima ui eliminate Urusi,vinginevyo usuperpower wako ipo siku utaota mbawa tu.Ndio maana USA anafanya kila aliwezalo kumzungukan Urusi.
State zilizokuwa chini ya Russia ndo zina mkimbia kwa sababu ya vitisho.Russia anatakiwa ajikite kwenye uwezeshaji wa kiuchumi badal ya mabavu.Russia ni failure state sababu naona wanaludia makosa miaka ya umoja wa kisovieti.NOW wanatakiwa wajifunze kwa China
 
kaingilia mambo yandani ya nchi gani?
kuna watu wanaingilia mambo yandani yanchi zawatu kwamba hamuwaoni hamuwasikii ama ndio propaganda zimewawezaa
Kwamba ni sahihi kwa Russia kuipangia Ukrain jinsi ya kushirikia na washirika wake?
 
Sasa Russia kwa nini apate tabu si awe tu mpole kisha atume maombi aruhusiwe kujiunga na Nato. If you can't beat them join them.
Ona demand za putin hakuna nchi yenye watu timamu wana weza kubali
Screenshot_20220205-101648_YouTube.jpg
 
Kati ya hao wa ulaya nani aliemtuliza Hitler?
Upepo wa WW II ulibadilika tu pale Marekani alipojiunga rasmi na vita na hili liko documented kabisa.

NB: Warusi takriban milioni 27 walikufa kutokana na vita hivyo.
 
Huyu Russia mbona majirani zake karibu wote wa Ulaya Magharibi wamejiunga na NATO tayari na hajafanya chochote sasa huyo Ukraine ndio anataka kumuonea.

Russia ni sharti aelewe kwamba ushirika wa leo watu wanaangalia maslahi hivyo hawezi kulazimisha mtu awe mshirika wake wakati na yeye ni mtu wa njaa tu, hilo haliwezekani.
 
Upepo wa WW II ulibadilika tu pale Marekani alipojiunga rasmi na vita na hili liko documented kabisa.

NB: Warusi takriban milioni 27 walikufa kutokana na vita hivyo.
Marekani yupo ulaya? Soma vizuri na Mmarekani aliwapa wote msaada hadi hao uingereza na wenzake mbona bado walichezea vichapo? Au msaada kwa urusi ulikua ni tofauti?
 
Marekani yupo ulaya? Soma vizuri na Mmarekani aliwapa wote msaada hadi hao uingereza na wenzake mbona bado walichezea vichapo? Au msaada kwa urusi ulikua ni tofauti?
Walichezea vichapo kutoka kwa nani, mbona hueleweki..?
 
Bado hoja ni dhaifi Huwez kupigia mstali Marekani au Russia et wanaweza amua future ya poland au Ukrain hao Wote hawana mamlaka mkuu.Russia anatakiwa akubali tu she falure state
Watu wanajadili Mambo ki ushabiki tu, ukishindwa kumshawishi nchi ikuunge au iwe upande wako....usimshikie silaa
 
Huyu Russia mbona majirani zake karibu wote wa Ulaya Magharibi wamejiunga na NATO tayari na hajafanya chochote sasa huyo Ukraine ndio anataka kumuonea.

Russia ni sharti aelewe kwamba ushirika wa leo watu wanaangalia maslahi hivyo hawezi kulazimisha mtu awe mshirika wake wakati na yeye ni mtu wa njaa tu, hilo haliwezekani.
Watu wanaangalia usalama wa nchi zao huwezi kuona mtu unayejua adui yako anakusogelea kashika silaha ww unasubiri mpk akuchome ndio uchukue hatua itakuwa ushachelewa umeumia unatakiwa uzuie mapema ndio maana hata USA miaka hyo USSR alivyopeleka makombora yake Cuba USA alipambana sana yaondolewe unafikiri kwann alikuwa na wasiwasi wakati makombora yapo nchi jirani sasa mnachoshangaa Russia kukataa NATO kusogea karibu yake ni sababu nia yao nikuweka makombora hapo jirani yake,

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Huyu Russia mbona majirani zake karibu wote wa Ulaya Magharibi wamejiunga na NATO tayari na hajafanya chochote sasa huyo Ukraine ndio anataka kumuonea.

Russia ni sharti aelewe kwamba ushirika wa leo watu wanaangalia maslahi hivyo hawezi kulazimisha mtu awe mshirika wake wakati na yeye ni mtu wa njaa tu, hilo haliwezekani.
Ukraine hawezi kuungwa NATO kamwe
 
K
Walichezea vichapo kutoka kwa nani, mbona hueleweki..?
Kutoka kwa mjerumani............mrusi ndo alieweza kuzama berlin kumaliza utopolo wa hitler.......mbona hao wengine waliopewa misaada na Marekani walikua bado wanapapaswa na mjerumani?
 
Back
Top Bottom