Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,926
- 15,634
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine amesema kuwa mfumo wa Ulinzi wa anga wa Israel maarufu kwa jina la Iron Dome hauwezi kuhimili kuzuia makombora ya Urusi nchini Ukraine.
Waziri huyo aliyeshuhudia na kutesti nguvu ya makombora ya Urusi anasema kuwa mfumo huo wa Iron Dome umeundwa kwa ajili ya kuzuia makombora yaendayo kwa kasi ndogo, yarukayo kimo cha chini na yasiyo na nguvu kubwa (yenye nguvu hafifu) ambayo kimsingi makombora hayo hutengenezwa gereji. Iron Dome haina uwezo wa kukinga anga dhidi ya makombora ya kruizi na balistiki yanayomiminwa na Urusi yenye kasi kubwa na nguvu (impact) kubwa zaidi, yatengenezwayo kwenye viwanda maalumu kwa teknolojia ya juu zaidi, hata mengine yakawekewa 'decoys' za kuidanganya/kuikwepa mifumo ya ulinzi wa anga imara zaidi ya hiyo Iron Dome.
Ngoja nisubiri Povu toka kwa Waisrael wa Kibaigwa, uzuri wa bahati habari hii imeletwa na The Jerusalem Post.
====