Ukraine sasa iko katika vita kamili vya kujikomboa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hali ya vita vya Ukraine sasa iko wazi kwa kila mshirika.

NATO na Ukraine kwa upande mmoja na Russia kwa upande mwingine.

Uwanja wa vita rasmi unaeleweka kwa wote kuwa ni Ukraine.

Russia kama Nduli Amini, sasa anatakiwa kufurushwa kutoka katika ardhi zote za Ukraine zikiwamo Donbas, Lohansk na Crimea.

IMG_20220407_202246_619.jpg

Kimsingi kimenuka na ndiyo sababu Russia amesitisha safari kuelekea Kyiv na pia kujiondoa kote kwingine ili kujizatiti kwenye angalau majimbo matatu hayo.

Ukraine War: 'Russian soldiers held us as human shields'

Mwinda kageuka kuwa mwindwa. Udhwalimu haukuwahi kushinda na sasa ajipange kulimia meno.

Vinavyoitwa aina ya vita vikuu vya III vya dunia vinanukia hapa.

Ole wao kina nyasi, mafahali wawili hawa watakapokuwa wanapoonyeshana ubabe.

Hivi ni vita visivyokuwa na mwisho ulio katika siku za karibuni.
 
Hali ya vita vya Ukraine sasa iko wazi kwa kila mshirika.

NATO na Ukraine kwa upande mmoja na Russia kwa upande mwingine.

Uwanja wa vita rasmi unaeleweka rasmi kwa wote kuwa ni Ukraine.

Russia kama Nduli Amini, sasa anatakiwa kufurushwa kutoka katika ardhi zote za Ukraine zikiwamo Donbas, Lohansk na Crimea.

Kimsingi kimenuka na ndiyo sababu Russia amesitisha safari kuelekea Kyiv na pia kujiondoa kote kwingine ili kujizatiti kwenye majimbo matatu hayo.

Ukraine War: 'Russian soldiers held us as human shields'

Mwinda kageuka kuwa mwindwa. Udhwalimu haukuwahi kushinda na sasa ajipange kulimia meno.

Vinavyoitwa aina ya vita vikuu vya III vya dunia vinanukia hapa.

Ole wao kina nyasi, mafahali wawili hawa watakapokuwa wanapoonyeshana ubabe.

Hivi ni vita visivyokuwa na mwisho ulio katika siku za karibuni.
Madikiteta most of time hawatumii akili
 
Ukraine anabahati mbaya sana. Atapondwapondwa mpaka nukta ya mwisho. Hakuna kitu kitasalia. Lawama zote ziende kwa Zelensky, alitakiwa kukaa pamoja na Putin wayamalize.
Kwamba ungemshauri Nyerere kukaa chini na Amini wayamalize?

Anachofanya Ukraine hapa ni kurejesha ardhi yake dhidi ya mvamizi. Kwenye hilo Ukraine wako tayari kufa achilia mbali nchi kuharibika:

IMG_20220405_124518_576.jpg
 
We ni mpumbavu
Mara ngap amemtaka huyo Putin kichaa wazungumze huyo mshenzi amekataa

Mpumbavu tuu huyo
Dunia ya sasa haitak vita

Matusi yote hayo ya nini??.

Russia na NATO & the US--- wanajuana kwa undani zaidi kuliko sisi tunavyowajua, Historia ya uhasama wao inaanzia tangu vita kuu ya pili, vita baridi, kuvunjika kwa Soviet na WARSAW, WARSAW ni counterpart ya NATO kabla ya kuvunjika kwa Soviet.

Mzozo huu chimbuko lake ni uhasama wa kihistoria uliokuwa unafukuta chini kwa chini na hatimaye kuibuka hivi karibuni.

Tuombe Mungu kwani harufu ya WW lll ndio inanukia kwani silaha zinazoingizwa Ukraine kutoka NATO na USA zitachochea vita kuwa kubwa na athari mbaya na hivyo kuanzisha WW lll, Putin hawezi kukubali kushindwa kirahisi atatumia Hypersonic zenye uwezo wa kubeba Nuke heads, hapo dunia itakuwa Finito.
 
Ukraine haijapambana peke yake, ina NATO yote nyuma ya pazia ila atachapwa sana patabaki jivu pale na mcheza comedy wao kawaharibia nchi.

Ulipo mgogoro kila kitu ni wazi.

NATO kajiingiza ila vita ndani ya Ukraine. Haipo siri tena:

"Vita vikuu vya dunia kupiganiwa Ukraine."

Putin kaonyesha kulielewa somo mapema. Amekimbia mbio sana mithili ya aliyefumaniwa kuwahi Donbas, Lohansk na Crimea.

Hayupo anayetaka vita. Ukraine kapelekewa vita. Ukraine yuko katika kujikomboa na gharama yake ameikubali.

Habari ndiyo hiyo.
 
Matusi yote hayo ya nini??.

Russia na NATO & the US--- wanajuana kwa undani zaidi kuliko sisi tunavyowajua, Historia ya uhasama wao inaanzia tangu vita kuu ya pili, vita baridi, kuvunjika kwa Soviet na WARSAW, WARSAW ni counterpart ya NATO kabla ya kuvunjika kwa Soviet.

Mzozo huu chimbuko lake ni uhasama wa kihistoria uliokuwa unafukuta chini kwa chini na hatimaye kuibuka hivi karibuni.

Tuombe Mungu kwani harufu ya WW lll ndio inanukia kwani silaha zinazoingizwa Ukraine kutoka NATO na USA zitachochea vita kuwa kubwa na athari mbaya na hivyo kuanzisha WW lll, Putin hawezi kukubali kushindwa kirahisi atatumia Hypersonic zenye uwezo wa kubeba Nuke heads, hapo dunia itakuwa Finito.
USA kama yeye mbabe wa Dunia arushe hata risasi Moja katika Ardhi ya Russia halafu washirika wake wakae pembeni vita ipigwe Kati yake na Russia tuone mbabe Nani?...
 
Ulipo mgogoro kila kitu ni wazi.

NATO kajiingiza ila vita ndani ya Ukraine. Haipo siri tena:

"Vita vikuu vya dunia kupiganiwa Ukraine."

Putin kaonyesha kulielewa somo kukimbia mbio sana mithili ya aliyefumaniwa kuwahi Donbas, Lohansk na Crimea.

Hayupo anayetaka vita. Ukraine kapelekewa vita. Ukraine yuko katika kujikomboa na gharama yake ameikubali.

Habari ndiyo hiyo.
Mzee Kiduku wa North Korea tunaomba utuongezee silaha sisi Warusi huku Ukraine
 
USA kama yeye mbabe wa Dunia arushe hata risasi Moja katika Ardhi ya Russia halafu washirika wake wakae pembeni vita ipigwe Kati yake na Russia tuone mbabe Nani?...

Umeelewa kilichomkimbiza Mrusi kutokea Kyiv? Si Putin alishatoa siku 3 kwa Zelensky kutoka madarakani?

Ni hivi, parameters zote za vita ziko wazi, kila kitu kinajulikana na pande zote zimeridhia.

"Uwanja wa vita ni Ukraine."

Kwani wewe unaongelea vita ipi tena ya kurusha risasi au kombora wapi kusikohusika ndugu?
 
Back
Top Bottom