Ukraine waamua kuachia mji wa Severodonetsk baada ya kichapo kikali

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Vikosi vya Ukraine vilivyoko Severodonetsk vimetakiwa kuondoka, kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa eneo hilo.

Mji huo ndio kitovu cha uvamizi wa Urusi huku Moscow ikijaribu kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa za mashariki mwa Ukraine.

"Kusalia katika nafasi ambazo zimeshambuliwa kwa miezi mingi haina maana," gavana wa mkoa wa Luhansk Serhiy Haidai alisema.

Vikosi vya Urusi vimepiga hatua katika siku za hivi karibuni na vinakaribia kuzunguka jiji hilo, na mji wake pacha wa Lysychansk.

"Wamepokea maagizo ya kurejea kwenye nafasi mpya... na kutoka huko waendelee na shughuli zao," Bw Haidai aliambia televisheni ya Ukraine.

"Hakuna maana ya kukaa katika nafasi ambazo zimeharibiwa kwa miezi kadhaa kwa sababu ya kubaki," alisema.

Miundombinu yote ya jiji imeharibiwa kabisa, Bw Haidai aliongeza, na zaidi ya 90% ya nyumba zikiwa zimepigwa makombora na 80% kuharibiwa vibaya.

Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ulioanza mnamo Februari, umekuwa ukilenga Severodonetsk na mji wake pacha wa Lysychansk kwa wiki kadhaa.

Ni nafasi za mwisho zilizosalia za Kiukreni katika eneo la Luhansk, moja ya mikoa miwili inayounda Donbas ya mashariki.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amedai kwa uwongo kwamba wazungumzaji wa Kirusi katika Donbas wamekuwa wahanga wa mauaji ya halaiki - mojawapo ya sababu kuu anazotumia kuivamia Ukraine.

Siku ya Alhamisi, vikosi vya Urusi vilichukua udhibiti wa maeneo zaidi kusini mwa Severodonetsk na Lysychansk, na kuzua hofu kwamba vikosi vya Ukraine vitazingirwa huko hivi karibuni
 
Urusi sasa kutwaa miji magofu isiyo na shughuli zozote za kiuchumi sababu kabomoa miundombinu, mashule, mahospitali, makazi ya watu, kalipua reli, viwanja vya ndege nk

Hajateka mji kateka magofu kuteka mji unakuwa na watu, viwanda na shughuli za kiuchumi zikiendelea

Mrusi anateka dead cities
 
Urusi sasa kutwaa miji magofu isiyo na shughuli zozote za kiuchumi sababu kabomoa miundombinu, mashule,mahospitali ,makazi ya watu ,kalipua reli ,viwanja vya ndege nk

Hajateka mji kateka magofu kuteka mji unakuwa na watu ,viwanda na shughuli za kiuchumi zikiendelea

Mrusi anateka dead cities
Urusi walikuambia wanafuata shule Ukraine?

Acheni porojo nyie wamarekani wa Tandahimba. Kichapo mnachopokea sio cha kitoto!
 
Hakuna shule wala hospitali wala masoko wala mahoteli kwenye hiyo miji

Mrusi kabomoa vyote na makombora

Hii vita ni ya kwanza duniani kwa nchi kuteka magofu na kuyakalia

Hata Sisi tulipopigana na Uganda tulipoteka miji ilikuwa miji hai yenye uchumi.na biashara ,mashule,hospitali no

Mrusi bwege anateka miji magofu
 
Mrusi alikuambia anataka shule za Ukraine?

Hebu jibu kwanza hapo alafu tuendelee!
 
Urusi sasa kutwaa miji magofu isiyo na shughuli zozote za kiuchumi sababu kabomoa miundombinu, mashule,mahospitali ,makazi ya watu ,kalipua reli ,viwanja vya ndege nk

Hajateka mji kateka magofu kuteka mji unakuwa na watu ,viwanda na shughuli za kiuchumi zikiendelea

Mrusi anateka dead cities
Kaeni kwakutulia
Nasikia PUT IN anaumwa yupo ai sii yuu huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna shule wala hospitali wala masoko wala mahoteli kwenye hiyo miji

Mrusi kabomoa vyote na makombora

Hii vita ni ya kwanza duniani kwa nchi kuteka magofu na kuyakalia

Hata Sisi tulipopigana na Uganda tulipoteka miji ilikuwa miji hai yenye uchumi.na biashara ,mashule,hospitali no

Mrusi bwege anateka miji magofu
Mkuu hapa Putin anatuma ujumbe kwa Poland na akina Britain jinsi miji yao itakavyokuwa endapo wakizidisha choko choko
 
Vikosi vya Ukraine vilivyoko Severodonetsk vimetakiwa kuondoka, kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa eneo hilo.

Mji huo ndio kitovu cha uvamizi wa Urusi huku Moscow ikijaribu kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa za mashariki mwa Ukraine.

"Kusalia katika nafasi ambazo zimeshambuliwa kwa miezi mingi haina maana," gavana wa mkoa wa Luhansk Serhiy Haidai alisema.

Vikosi vya Urusi vimepiga hatua katika siku za hivi karibuni na vinakaribia kuzunguka jiji hilo, na mji wake pacha wa Lysychansk.

"Wamepokea maagizo ya kurejea kwenye nafasi mpya... na kutoka huko waendelee na shughuli zao," Bw Haidai aliambia televisheni ya Ukraine.

"Hakuna maana ya kukaa katika nafasi ambazo zimeharibiwa kwa miezi kadhaa kwa sababu ya kubaki," alisema.

Miundombinu yote ya jiji imeharibiwa kabisa, Bw Haidai aliongeza, na zaidi ya 90% ya nyumba zikiwa zimepigwa makombora na 80% kuharibiwa vibaya.

Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ulioanza mnamo Februari, umekuwa ukilenga Severodonetsk na mji wake pacha wa Lysychansk kwa wiki kadhaa.

Ni nafasi za mwisho zilizosalia za Kiukreni katika eneo la Luhansk, moja ya mikoa miwili inayounda Donbas ya mashariki.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amedai kwa uwongo kwamba wazungumzaji wa Kirusi katika Donbas wamekuwa wahanga wa mauaji ya halaiki - mojawapo ya sababu kuu anazotumia kuivamia Ukraine.

Siku ya Alhamisi, vikosi vya Urusi vilichukua udhibiti wa maeneo zaidi kusini mwa Severodonetsk na Lysychansk, na kuzua hofu kwamba vikosi vya Ukraine vitazingirwa huko hivi karibuni
Kudadeki hatimaye NATO wameondoa majeshi. Wamekubali kushindwa. Sasa tunaelekea kyiv
 
Urusi sasa kutwaa miji magofu isiyo na shughuli zozote za kiuchumi sababu kabomoa miundombinu, mashule,mahospitali ,makazi ya watu ,kalipua reli ,viwanja vya ndege nk

Hajateka mji kateka magofu kuteka mji unakuwa na watu ,viwanda na shughuli za kiuchumi zikiendelea

Mrusi anateka dead cities

Alisikika kilaza mmoja wa Nangurukuru.🤣🤣🤣
Kinachoangaliwa ni ardhi yenye rotuba,bandari,kutanuka kwenda kaskazini, kuangusha Dola ya marekani na madini ya chuma yanayopatikana kwenye hayo maeneo,na sio majengo ww mjinga!
 
Back
Top Bottom