The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
Takriban watu watatu wameuawa na wengine kumi na wanne wamejeruhiwa leo Ijumaa hii, Juni 27, katika shambulio la anga la Urusi kwenye mji wa Samar, katika mkoa wa Dnipropetrovsk - katikati-mashariki - gavana wa mkoa ametangaza.
Watu watatu wamepoteza maisha yao katika shambulio la adui. Watu kumi na wanne wamejeruhiwa," Sergei Lysak amesema kwenye Telegram, akiongeza kwamba idadi kamili ya vifo kutokana na shambulio hilo "imethibitishwa."
Hapo awali, afisa huyo alizungumza kuhusu "shambulio la kombora" dhidi ya Samar, ambalo lilisababisha "moto."
Shambulio hili baya la hivi punde la jeshi la Urusi linakuja siku mbili baada ya Rais Volodymyr Zelensky kusisitiza tena kwa Donald Trump, kando ya mkutano wa kilele wa NATO huko Hague, kwamba yuko "tayari" kununua mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot ya Marekani, muhimu kwa kuzuia mashambulizi ya anga ya Urusi.
Lakini kiongozi huyo wa Marekani aligeukia swali hilo kwa waandishi wa habari, akisema kwamba "angeona kama tunaweza kutoa baadhi ya mifumo hiyo," lakini kwamba Marekani "ilihitaji pia" mifumo hii sahihi sana.
Siku ya Jumanne, shambulio la Urusi huko Samar, jiji lenye wakaazi 70,000 kabla ya uvamizi wa Urusi, liligharimu maisha ya watu wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa, kulingana na Sergei Lysak.
Kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine, mashambulizi ya awali ya Urusi karibu na Samar yalipiga miundombinu ya kijeshi.
Samar ambayo inapatikana kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa mkoa wa Dnipro, iko chini ya kilomita 150 kutoka upande wa mashariki, ambapo jeshi la Urusi linasonga mbele dhidi ya vikosi vya Ukraine ambavyo viko katika hali nzito.
Wanajeshi wa Urusi sasa wanatishia kuingia katika jimbo la Dnipropetrovsk, hatua ambayo itakuwa ya kwanza tangu uvamizi huo uanze Februari 2022.