Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Baada ya Urusi kupiga miundo mbinu ya maji na umeme huko Kiev. Maengineer na Mafundi wa Ukraine wanefanikiwa kurudisha umeme na Maji katika mji mzima wa Kiev.
Hayo yamesemwa na Mayor wa jiji la Kiev.
Wakati huohuo Ukraine imesema imefanikiwa kudondosha Drone 8 za Urusi ilizopewa na Iran(Shahed-136) jana zilizokuwa zimetumwa zikapige miundo mbinu ya Kiraia
Hii inafuatia baada ya Ukraine kuongeza ulinzi wa anga kutokana na mitambo mbalimbali ya Ulinzi wa Anga iliyopata kutoka kwa washirika wake wa Magharibi. Ujerumani imeipa Ukraine mtambo wake wa Gepard unaodungua ndege na drone na pia Marekani imeipa Ukraine mitambo ya ulinzi wa anga ya NASAM miwili na imesema itapeleka mingine nane.
Kwa upande wa uwanja wa vita, Urusi imeondoa mamlaka yake ya kiutawala kutoka Mji wa Kherson na kuuhamishia kusini karibu na Crimea, na wakati huohuo imekuwa ikiendesha operesheni ya kuondoa raia huko Kherson baada ya pressure ya kijeshi kutoka Ukraine kuwa kubwa.