John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Ukraine imetuma ombirasmi kwa serikali ya Ujerumani kwa ajili ya msaada wa "silaha za kujihami", kwa mujibu wa ripoti ya gazeti.
Katika barua iliyonukuliwa na Gazeti la Ujerumani la Süddeutsche Zeitung, ubalozi wa Ukraine umeiomba Berlin kutoa jibu la haraka, kutokana na hali tete ya kiusalama na kitisho cha uvamizi wa Urusi.
Moscow imepeleka maelfu ya wanajeshi kwenye mpaka wa Ukraine, na kusababisha hofu kwamba inapanga kumvamia jirani yake huyo mdogo. Jumuiya ya kujihami ya mataifa ya magharibi NATO, pia imeonya juu ya idadi kubwa ya wanajeshi wa Urusi wanaopelekwa nchini Belarus.
Urusi inakanusha kupanga uvamizi. Imedai uhakikisho kadhaa wa kiusalama kutoka mataifa ya magharibi, ikiwemo kwamba Ukraine kamwe haitajiunga na NATO na kwamba muungano huo wa kijeshi uondoe vikosi vyake kutoka eneo la Ulaya Mashariki.
Katika kujibu matakwa ya Urusi, NATO na Marekani zimesema madai yote mawili hayana mashiko na badala yake zimependekeza mazungumzo zaidi kuhusu makombora na kupunguza kwa wanajeshi.
Katika barua iliyonukuliwa na Süddeutsche Zeitung, Ukraine inatoa maombo kadhaa makhsusi ya vifaa vya kujilinda, ikiwemo mifumo ya makombora ya masafa ya kati ya kudungua ndege, bunduki za kudungua ndege zisizotumia rubani, kamera za uchunguzi, mifumo ya ufuatiliaji ya kielektroniki, vifaa vya kuona usiku na risasi.
Kyiv inatafuta "msaada wa mara moja katika upatikanaji wa haraka wa mifumo ya silaha za aina ya kujihami," inasema barua hiyo, kwa mujibu wa Gazeti la Süddeutsche Zeitung.