Ukraine yaiomba Ujerumani silaha za kujilinda dhidi ya Urusi

Ukraine yaiomba Ujerumani silaha za kujilinda dhidi ya Urusi

Kweli kejeli....mzee mzima anatandika kombora hapo kofia inakua ya fashoon tu
Helmet husaidia kuzuia sprinters, shrapnels na kudondokewa na vitu uko kwenye trench na kwingine. Risasi sio lengo kuu la helmet ingawa inazipunguza au kuzuia impact, ila Marekani sahivi helmet zao mpya zinazuia standard bullet.

Zile helmet sio kila nchi inafyatua. Nchi kibao haziwezi toa modern helmet. Ila Ukraine wanaotoa vifaru vyao kama T-84 Oplot na makombora yao sio wakupewa helmet. Ujerumani ina silaha nzito kama kifaru cha Leopard 2 kazi ya Krauss-Maffei hii hata ukiweka Abrams cha Mmarekani sikichagui. Kuna guns na howitzers zenye range kubwa kutoka kwa Rheinmetall. Kuna diesel submarines zenye AIP System kama Dolphin anazouziwa Israel.

Tatizo silaha za Ulaya nyingi hutengenezwa kwa joint projects. Watashiriki kina Spain, Italy, UK, Germany. Mara nyingi France hutengeneza silaha zake na kampuni zake kama Dassault na Naval Group, UK sometimes hutengeza zake pia. Hata makampuni ya silaha ya Ulaya yanalazimika kuungana kuwa consortium kupata tenda. Kina BAE Systems, Airbus, MBDA, Fincantieri, Thales, etc wanashirikiana. Ili upate silaha mpaka wakubali nchi zote. Ndio maana nchi kama Argentina yenye bifu na UK inanunua silaha kwa France au Sweden
 
Ukraine imetuma ombirasmi kwa serikali ya Ujerumani kwa ajili ya msaada wa "silaha za kujihami", kwa mujibu wa ripoti ya gazeti.

Katika barua iliyonukuliwa na Gazeti la Ujerumani la Süddeutsche Zeitung, ubalozi wa Ukraine umeiomba Berlin kutoa jibu la haraka, kutokana na hali tete ya kiusalama na kitisho cha uvamizi wa Urusi.

Moscow imepeleka maelfu ya wanajeshi kwenye mpaka wa Ukraine, na kusababisha hofu kwamba inapanga kumvamia jirani yake huyo mdogo. Jumuiya ya kujihami ya mataifa ya magharibi NATO, pia imeonya juu ya idadi kubwa ya wanajeshi wa Urusi wanaopelekwa nchini Belarus.

Urusi inakanusha kupanga uvamizi. Imedai uhakikisho kadhaa wa kiusalama kutoka mataifa ya magharibi, ikiwemo kwamba Ukraine kamwe haitajiunga na NATO na kwamba muungano huo wa kijeshi uondoe vikosi vyake kutoka eneo la Ulaya Mashariki.

Katika kujibu matakwa ya Urusi, NATO na Marekani zimesema madai yote mawili hayana mashiko na badala yake zimependekeza mazungumzo zaidi kuhusu makombora na kupunguza kwa wanajeshi.

Katika barua iliyonukuliwa na Süddeutsche Zeitung, Ukraine inatoa maombo kadhaa makhsusi ya vifaa vya kujilinda, ikiwemo mifumo ya makombora ya masafa ya kati ya kudungua ndege, bunduki za kudungua ndege zisizotumia rubani, kamera za uchunguzi, mifumo ya ufuatiliaji ya kielektroniki, vifaa vya kuona usiku na risasi.

Kyiv inatafuta "msaada wa mara moja katika upatikanaji wa haraka wa mifumo ya silaha za aina ya kujihami," inasema barua hiyo, kwa mujibu wa Gazeti la Süddeutsche Zeitung.
Wajerumani ndio kiboko ya Warusi
 
Kwani maamuzi ya nchi moja kujiunga na kingine si maamuzi ya nchi husika? Inakuaje Ukraine izuiliewe na Urusi kujiunga na NATO?
Ukraine wao watie sahihi tu, hayo Mambo mengine yatafuata baadae .....unyonge ni ujinga
NATO ndio wanajivuta vuta kuisainisha ukraine iwe member...
Moja ya masharti ya kujiunga NATO , member mpya anatakiwa asiwe na migogoro ya ndani, kama civil war kwani NATO hawataki kujikuta wamenasa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe , itakua kashifa NATO itumike na serikali ya ukraine, kupigan vita na wa ukraine,
Ukraine ina separatists kule donabas
 
Mjerumani anawabania jamaaa hadi NATO wenzie wameanza kujiuliza jamaa wana ajenda gani maana wameombwa silaha muda sana ila wanajizungusha tu ..................isije baadae ikafanywa suprise matata
Ujerumani inazingatia Katiba yake!
 
Back
Top Bottom