Putin naona anataka achukue kwanza majimbo yote ya mashariki yaliyoanzisha vuguvugu za kujitenga mwaka 2014 alafu ndo aendelee na vitu vingine.wasi wasi baadae kuna uwezekano wa kukatokea nchi 2.(ukraine ya warusi na ukraine ya wamagharibi).
Majimbo zaidi ya 9(CRIMEA,DONESK,LUHANSK,ODESSA,ZAPORIZHIA,KHARKIV,MYKOLAYIV,KHERSON NA DNIPROPETROVSK) yalishudiwa maandamano ya kutaka kijitenga na ukraine, ila ni majimbo ma 3 kati ya majimbo 9 yalifanikiwa kuweza kujiondoa(CRIMEA,DONESK NA LUHANSK)
Warusi baada ya kuingia wamechukua majimbo ma 2 la ZAPORIZHIA na KHERSON kwa nguvu na kubakiza majimbo ma 4 yaliyoanzisha vuguvugu za kujitenga kwaka 2014.
*ODESSA
*KHARKIV
* Mykolayiv Oblast
*DNIPROPETROVSK
(KHARKIV)
Kharkiv kwa sasa kunaonekana ndo jimbo lenye mashambulizi makali ya warusi kuliko jimbo lolote lile ndani ya ardhi ya Ukraine.vikosi vya anga na vya ardhini vinafanya mashambulizi muda wote,kuanguka kwa mji huu wa kiviwanda itakuwa pigo sana kwa serikali ya ukraine.
(ODESSA)
Odessa ndo jimbo pekee lenye bandari lililobaki kwenye mikono ya majeshi ya ukraine,kuferi kwa jimbo hili ni wazi ukraine atoweza kupokea au kutuma mzigo wowote ule kwa njia ya majini.siku 2 za ivi karibuni warusi wameongeza mashambulizi makali sana ya anga.ni wazi wanajiandaa kutaka kuvamia jimbo la Odessa.
(Mykolayin)
Mykolayin siku za nyuma imekuwa nayo kitovu cha kupokea mashambulizi kutoka angani na ardhini.vikosi vya urusi vinafanya mashambulizi mazito ili waweze kuingia kwenye mkoa huu.
(Dnipropetrovsk)
Dnipropetrovsk imekuwa makimbilio kwa wa ukraine wanaotoka sehemu zenye mapigano makali,ila kuongezeka kwa mashambulizi ya ivi karibuni kwenye mkoa huu inatoa ishara kuwa warusi wanajiandaa kutaka kuvamia.
View attachment 2174115