JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Zaidi ya miili 900 ya wananchi wa kawaida imebainika kuwepo katika Jiji la Kyiv ambao ni Mji Mkuu wa Ukraine baada ya kuondoka kwa majeshi ya #Russia, mingi kati ya hiyo ikiwa imeshambuliwa kwa risasi. Polisi wamesema kuwa hiyo ni ishara kuwa wengi waliuawa kirahisi.
Idadi hiyo ya kutatanisha iliibuka muda mfupi baada ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi kuahidi kuongeza mashambulizi ya makombora dhidi ya Kyiv kujibu madai ya mashambulizi ya #Ukraine katika eneo la Urusi.
Rais wa Ukraine, Volodymyr #Zelenskyy alishutumu wanajeshi wa Urusi wanaokalia baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Kherson na Zaporizhzhia kwa kuwatisha raia na kuwinda mtu yeyote ambaye ni mwajiriwa wa jeshi au Serikali ya Ukraine
Source: Indiatoday