Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Katika hali inayoonesha vita vinaelekea kubaya zaidi Urusi imeitaka Ukraine kuzingatia maonyo yake haraka kabla awamu ijayo ya mashambulizi haijaanza. Onyo hilo limetolewa na waziri wa mambo ya nje wa Urusi mapema jana.
Katika onyo hilo Sergei Lavrov ameitaka Ukraine kuyatambua majimbo mapya ya Urusi na kuacha kupeleka askari wake huko.
Onyo hilo limekuja siku moja baada ya raisi Putin kunakiliwa akisema yuko tayari kwa mazungumzo na Ukraine tafsriri ya aaina ya mazungumzo ambayo ndio sasa imepatikana kutoka kwa waziri wake wa mambo ya nje
Wakati huo huo onyo hilo limekuja baada ya ziara ya Putin huko Belarus na ziara nyengine ya kushtukizia ya raisi wa Belarus huko Urujsi. Ziara hizo zimeambatana na harakati kubwa ya kupelekwa zana nzito za kivita kwenye mpaka wa Belarus na Ukraine zikiwemo ndege zenye uwezo wa kubeba makombora ya nyuklia.
wiki iliyopita raisi Zelensky naye alifanya ziara ya muda mfupi huko Mareknai ambako aliahidiwa kupatiwa makombora ya patriot ambayo ni maalum kwa kuyadungua makombora mengine yanayoelekea kutua kwenye yake.Makombora hayo yatachukua mpaka miezi 6 ijayo kuwasili humo muda sawa na unaohitajika kwa kutoa mafunzo kwa askari wa Ukraine watakayotakiwa kuyatumia.