Ukraine yatakiwa kuzingatia maonyo ya Urusi haraka kabla kipigo kijacho

Ukraine yatakiwa kuzingatia maonyo ya Urusi haraka kabla kipigo kijacho

Mie nasema vita kaitafuta yeye rais wa ukrain! Asingekua mbishi tusingefika huku! Ifike sehem ajitambue... jambazi hadi kukuingilia nyumban kwako kuna jambo!
Unamaanisha Putin ni jambazi
 
Mie nasema vita kaitafuta yeye rais wa ukrain! Asingekua mbishi tusingefika huku! Ifike sehem ajitambue... jambazi hadi kukuingilia nyumban kwako kuna jambo!
".....jambazi hadi kukuingilia nyumban kwako kuna jambo!"
Haswaa. Na jambo lenyewe ni kwamba jambazi limeona au amepata ramani ya kitu chenye thamani ulichonacho nyumbani kwako naye anakitamani siku nyingi. Hiyo ndo akili ya Putin. ... Urussi(Putin) anatamani sana Ukraine iwe ni sehemu (mojawapo ya mikoa) ya Urussi.
 
Super pawer anazidi kuchakazwa na kudhalilishwa wewe umeklalia propaganda.., shauri yako,nenda ukamsaidie bwana wako uko field maana anatolewa kamasi balaa View attachment 2459698

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Hizo propaganda hazisaidii!!! Anayedaiwa kumzidi nguvu mwenzake kwenye uwanja wa propaganda, kwenye uhalisia keshapokonywa majimbo manne tayari!!! Hana uwezo wa kujipigania bila kuombaomba silaha toka nchi za magharibi ambako wameshajipatia soko la silaha zao!! Atalipa deni la silaha hizo kwa zaidi ya miaka 100 ijayo!! Wasipompa silaha hana uwezo wa kupigana hata kwa wiki moja!! Huyo ndiye anapigiwa chapuo kuwa anashinda vita!! Karibu nusu ya nchi yake iko gizani kwa kukosa umeme na maji tiririka ni shida!! Huyo ndiye tunaambiwa anashinda!! Kila leo miji yake inapokea precision cruise missiles zinazoangamiza miundo mbinu muhimu huyo ndiye tunaambiwa anashinda vita!!! Na kuna mapopoya humu yanaamini propaganda hizo za magharibi!!
 
Mhhh! Ni yupi kati yao anayeomba waongee/wazungumze? Anayeomba waongee ujue amekamatiwa chini kisawasawa na ameshaona hana ujanja tena zaidi ya kuomba mazungumzo kwani ngoma imeshakuwa nzito kwake tofauti na matarajio yake.
Alianza hivi:-
1. Jisalimishe au kimbilia nchi ya uhifadhi(Exile) but Jamaa yupo na anavitembelea vikosi vyake kama kawa.
2. Ni OP ya masaa72 tu kazi itakuwa imeisha.Huu ni mwezi wa 9 bado hajaweza kukamilisha OP
3. Ole kwa nchi yeyote itakayomsaidia au kutoa silaha - nitatoa jibu sawia kwa hilo taifa. Leo hii west wanasaidia kwa hali na mali na bado hajatoa jibu sawia
4. Nitatumia nuklia. Hadi leo ameziatamia nuklia zake kama kuku anvyoatamia mayai hazitumii bado. Anabweka tu licha ya kuambiwa ni RUKSA kutumia halafu ataona majibu yake.
5. Ameshindwa kwenye medani za kivita sasa anapiga hovyo maeneo ambayo sio ya kivita e.g. mashule, mahospitali n.k.(Hazingatii taratibu za vita)
6. Ameishiwa askari na silaha na kwa sasa anahaha kuomba msaada kwa Iran, Belarus, NK na kukodi kundi la mamluki Wagner. Anakusanya yeyote mtaani Wazee, walevi,vibaka na Wafungwa (Me na Ke) kuwapeleka kama askari mstari wa mbele(Frontline)
7. Amejaribu kuwaomba wazee wa magharibi wamshawishi Ukraine akubali kwenda kwenye meza ya mazungumzo. Amepewa vigezo vikamshinda kutekeleza.
NB:......Yapo mengi yanayoashiria kwamba Jamaa katepeta, yuko hoi bin taaban mpaka ameshindwa kuwalipa wazee waliostaafu kazini posho zao. Wapo matajiri wanaojiua kutokana na kero na changamoto za kimaisha zilizopo nchini Urussi.
 
Imeshazoeleka sasa kwamba Putin na genge lake ni watu wa mikwara kila kunapokucha.
Hakuna jipya hapo.
Laiti magharibi wakitaka hii vita iishe hata mwezi wa pili au 3 inawezekana kabisa. Majimbo yakotokwa sio kwamba hawawezi peleka silaha ili kuyakomboa ila wao walishasema, nia yao ni kuona vita vinachukua muda mrefu zaidi.
 
Ndio. Baadhi ya Vitu vingi vilivyomkasirisha Putin ni pamoja na kufedheheka mbele ya Mataifa kwani ameshindwa kuiteka Ukraine kwa zaidi ya miezi 9 ilhali alijitapa ni 72hrs.
Uchumi wake umedorora mno kutokana na vizuizi/vikwazo vya kimataifa n.k.
Putin amefika mahali ameanza kuwa omba-omba kwa Iran, Belarus na N.Korea yan anachopigania kwa sasa ni kulinda walau Status quo yake.
Heshima aloijenga kwa miaka mingi ameiporosha kirahisi
 
Ukifuatilia kwa vizuri hii si mikwara.Urusi inataka imalize kazi kabla hizo Patriot hazijafika.
Waukraine wakitaka kulazimisha ushindi kwa faida ya NATO wataishiwa na kila kitu.
Huweizi maliza kazi kwa makombora ya msafa marefu pekee. Jeshi LA waenda kwa miguu linamuumiza Putin
 
Back
Top Bottom