Hizo propaganda hazisaidii!!! Anayedaiwa kumzidi nguvu mwenzake kwenye uwanja wa propaganda, kwenye uhalisia keshapokonywa majimbo manne tayari!!! Hana uwezo wa kujipigania bila kuombaomba silaha toka nchi za magharibi ambako wameshajipatia soko la silaha zao!! Atalipa deni la silaha hizo kwa zaidi ya miaka 100 ijayo!! Wasipompa silaha hana uwezo wa kupigana hata kwa wiki moja!! Huyo ndiye anapigiwa chapuo kuwa anashinda vita!! Karibu nusu ya nchi yake iko gizani kwa kukosa umeme na maji tiririka ni shida!! Huyo ndiye tunaambiwa anashinda!! Kila leo miji yake inapokea precision cruise missiles zinazoangamiza miundo mbinu muhimu huyo ndiye tunaambiwa anashinda vita!!! Na kuna mapopoya humu yanaamini propaganda hizo za magharibi!!
Mhhh! Ni yupi kati yao anayeomba waongee/wazungumze? Anayeomba waongee ujue amekamatiwa chini kisawasawa na ameshaona hana ujanja tena zaidi ya kuomba mazungumzo kwani ngoma imeshakuwa nzito kwake tofauti na matarajio yake.
Alianza hivi:-
1. Jisalimishe au kimbilia nchi ya uhifadhi(Exile) but Jamaa yupo na anavitembelea vikosi vyake kama kawa.
2. Ni OP ya masaa72 tu kazi itakuwa imeisha.Huu ni mwezi wa 9 bado hajaweza kukamilisha OP
3. Ole kwa nchi yeyote itakayomsaidia au kutoa silaha - nitatoa jibu sawia kwa hilo taifa. Leo hii west wanasaidia kwa hali na mali na bado hajatoa jibu sawia
4. Nitatumia nuklia. Hadi leo ameziatamia nuklia zake kama kuku anvyoatamia mayai hazitumii bado. Anabweka tu licha ya kuambiwa ni RUKSA kutumia halafu ataona majibu yake.
5. Ameshindwa kwenye medani za kivita sasa anapiga hovyo maeneo ambayo sio ya kivita e.g. mashule, mahospitali n.k.(Hazingatii taratibu za vita)
6. Ameishiwa askari na silaha na kwa sasa anahaha kuomba msaada kwa Iran, Belarus, NK na kukodi kundi la mamluki Wagner. Anakusanya yeyote mtaani Wazee, walevi,vibaka na Wafungwa (Me na Ke) kuwapeleka kama askari mstari wa mbele(Frontline)
7. Amejaribu kuwaomba wazee wa magharibi wamshawishi Ukraine akubali kwenda kwenye meza ya mazungumzo. Amepewa vigezo vikamshinda kutekeleza.
NB:......Yapo mengi yanayoashiria kwamba Jamaa katepeta, yuko hoi bin taaban mpaka ameshindwa kuwalipa wazee waliostaafu kazini posho zao. Wapo matajiri wanaojiua kutokana na kero na changamoto za kimaisha zilizopo nchini Urussi.