Ukristo Marekani umekosa Mwelekeo

Ukristo Marekani umekosa Mwelekeo

Unyenyekevu ni tabia.
Wapo Watu hawawajua waarabu, hawawajui waislamuna hawana hizo dini na ni wanyenyekevu.

Uislamu ni dini ya kiarabu iliyoanzishwa na MUHAMMAD,

Yesu hakuwa muislamu kama dini ila alikuwa ni mnyenyekevu kitabia. Kidini Yesu ni Myahudi
Yesu hakuwa "mnyenyekevu"?
 
Sasa kama ndo hivyo mbona waarabu wa Maka walikuwa wakimpinga mtume Muhammad kuueneza huo uislam ndani ya jamii ya waarabu kwa hoja ya kuwa unapingana na mila na mungu wao walio kuwa wanamuabudu kipindi hicho?

Nimekuambia kuwa kabla ya uislam na Ukrisito kuja jamii za wazungu na waarabu zilikuwepo kwa zaidi ya mamilioni ya miaka zikiwa na tamaduni zao hivyo sio sahihi kusema eti hizo dini eti hizo dini ni tamaduni za jamii fulani,kwa sababu hizo dini zimekuja na kuwakuta kama sisi ambavyo dini zili tukuta.

Na mpaka hizo jamii zinakuja kupokea dini hizi kumetumika gharama kubwa sana ya damu za watu na muda mwingi sana ,sasa kama hizi dini zilikuwa zinaendana na tamaduni zao kwann watu walikuwa wanakataa hizo dini mkapa ikarazimika kutumika ncha ya upanga ili wazi kubali?

Hata waarabu wa Africa kaskazini uislam wamekuja kuujua baada ya wao kutawaliwa na Ottoman walikuwa hawaujui.
Waarabu sio wa Mecca peke yao, Waarabu wako sehemu kubwa Uarabuni.
 
Hakuna dini ambayo haijawahi kupingwa na wenyeji wake.
Kuanzia Uyahudi, Ibrahim alipingwa na Jamii yake ndio akakimbia kutoka Ukaldayo mpaka Canaan(Palestine)
Ukristo ulipingwa na Warumi mpaka mfalme wa Kirumi constanino aliposilimu na kuingiza mila za Kirumi kwenye Ukristo ndio ukawa ukristo unaouoma hivi leo.

Muhamad alipingwa na Makuresh nusura wamuue lakini baadaye uislamu ukàkubalika hapo mashariki ya kati.

Dini kwa zamani ilikuwa inahusisha siasa na utawala.
Uislamu ungetumika kuunganisha jamii zote za mashariki ya kati ikiwemo Waarabu kwa sababu ndio imebeba utambulisho wa jamii hizo.

Ndio maana nikakuambia bila kutawaliwa (ukoloni) hizo dini ni tamaduni za jamii zingine. Hazina uhusiano na mila, desturi, tamaduni na miungu ya waafrika.
Kila jamii ina dini yake.
Sasa kama hizo dini zilikuwa zinaendana na tamaduni za wenyeji kwann walikuwa wana zipinga?
Alafu mkuu sio kweli kuwa dini zipo kwa sababu wa uwepo wakoloni ,kwa sababu kuna nchi zilitawaliwa na hazijafuata dini hizi mbili.
Dini kwa kiasi kikubwa zilienezwa na wafanya biashara na wamisionali.
 
Weka tafsiri yako upendayo, mradi usijidanganye nafsi yako tu.

Swali litakalo kuja ni unyenyekevu kwenye nini?
Kwa kuongezea ili uwe muislamu lazima uwe mnyenyekevu kwa Allah ambaye ni Mungu wa Waarabu (kabila la Wakurdi alilotokea Muhamad)

Sasa Yesu anamjua hata huyo Allah? Ili awe mnyenyekevu mbele zake? Yesu ni Myahudi alikuwa mnyenyekevu kwa Yàhweh, Mungu wa waisraeli.

Kuna Watu ni wanyenyekevu kwa Rais Samia. Na wapo ni wanyenyekevu kwako lakini sio wanyenyekevu kwa Allah.

Somo la Semantic NI pana
 
Swali litakalo kuja ni unyenyekevu kwenye nini?
Kwa kuongezea ili uwe muislamu lazima uwe mnyenyekevu kwa Allah ambaye ni Mungu wa Waarabu (kabila la Wakurdi alilotokea Muhamad)

Sasa Yesu anamjua hata huyo Allah? Ili awe mnyenyekevu mbele zake? Yesu ni Myahudi alikuwa mnyenyekevu kwa Yàhweh, Mungu wa waisraeli.

Kuna Watu ni wanyenyekevu kwa Rais Samia. Na wapo ni wanyenyekevu kwako lakini sio wanyenyekevu kwa Allah.

Somo la Semantic NI pana
Hayo utajibu wewe ukiijuwa lugha ya Yesu
 
Sasa kama hizo dini zilikuwa zinaendana na tamaduni za wenyeji kwann walikuwa wana zipinga?

Wanazipinga kwa sababu ni dini mpya zilizoanzishwa na miongoni mwa Watu wao. Sababu kubwa ni maslahi ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa mfano, Yesu alipokuwa anahubiri kuhusu habari njema(Injili) dini yake ya kiyahudi ilimpinga kwa sababu ya maslahi ya kisiasa na kiuchumi. Ni ishu ya Wafuasi na Kupata nguvu ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa zamani Dini ilikuwa ndio Siasa. Unapoanzisha dini zamani ni kama sasa uanzishe chama cha siasa.

Muhamad alipinga kuabudu sanamu katika Kaaba Kwa Sababu tayari alikuwa na mafungamano na ukaribu na baadhi ya Wayahudi na Wakristo. Alikuwa muumini wa Mungu mmoja. Ambaye kwa wakati huo waarabu kabla ya uislamu Allah alikuwa Chief god yaani mungu mkuu ambaye sanamu yake haikuwako kati ya zile sanamu ya miungu 360 zilizokuwa zinaabudiwa pale kaaba
 
Mimi kinanishangaza mtu muislam ku-pretend kuwa Mkristo ili kujenga hoja zisizokuwa na mashiko.

Uliyeleta hii mada umejifanya unaishi America kumbe upo zako hapo Mbande ila ulichoandika hapa umehadithiwa na jamaa yako aliyewahi kuishi huko lakini ukaona uongeze na verse kwamba ulikuwa unasali Kanisa fulani ili uaminike.

Zipo njia nyingi za kueneza imani yako watu wakaielewa siyo lazima uwe muongo muongo mjanja mjanja mwisho hata imani yako inaonekana ya kijanja janja.
Aisee! Kwa hiyo jamaa yuko zake Mbande! Halafu anajifanya yuko Maryland! 😁
 
Hayo utajibu wewe ukiijuwa lugha ya Yesu

Hao wote tunaowataja sio Waafrika.
Wana dini zao, wanamiungu yao, wanamila na desturi zao.

Ila mimi na wewe ambao ni waafrika tunaacha yetu tunakimbilia yasiyotuhusu. Huo ndio Ukoloni mamboleo wenyewe.

Kitendo cha muafrika kujitambulisha kama muislamu au mkristo kinadhihirisha jinsi ambavyo akili yake ilivyokufa, alivyotawaliwa.

Kitabu chenye kipo wazi ni kitabu cha kiarabu, wahusika ni waarabu, Maeneo yanayotajwa ni ya waarabu, sikukuu zote niza waarabu, mil na desturi zote ni za waarabu.
Halikadhalika na biblia. Sasa mambo ya utumwa ndivyo yalivyo.
 
Sasa kama hizo dini zilikuwa zinaendana na tamaduni za wenyeji kwann walikuwa wana zipinga?
Alafu mkuu sio kweli kuwa dini zipo kwa sababu wa uwepo wakoloni ,kwa sababu kuna nchi zilitawaliwa na hazijafuata dini hizi mbili.
Dini kwa kiasi kikubwa zilienezwa na wafanya biashara na wamisionali.
Ungeweka mifano ya hizo nchi mjadala uwe mpana zaidi mkuu
 
Back
Top Bottom