Ukristo Marekani umekosa Mwelekeo

Yesu hakuwa "mnyenyekevu"?
 
Waarabu sio wa Mecca peke yao, Waarabu wako sehemu kubwa Uarabuni.
 
Sasa kama hizo dini zilikuwa zinaendana na tamaduni za wenyeji kwann walikuwa wana zipinga?
Alafu mkuu sio kweli kuwa dini zipo kwa sababu wa uwepo wakoloni ,kwa sababu kuna nchi zilitawaliwa na hazijafuata dini hizi mbili.
Dini kwa kiasi kikubwa zilienezwa na wafanya biashara na wamisionali.
 
Weka tafsiri yako upendayo, mradi usijidanganye nafsi yako tu.

Swali litakalo kuja ni unyenyekevu kwenye nini?
Kwa kuongezea ili uwe muislamu lazima uwe mnyenyekevu kwa Allah ambaye ni Mungu wa Waarabu (kabila la Wakurdi alilotokea Muhamad)

Sasa Yesu anamjua hata huyo Allah? Ili awe mnyenyekevu mbele zake? Yesu ni Myahudi alikuwa mnyenyekevu kwa Yàhweh, Mungu wa waisraeli.

Kuna Watu ni wanyenyekevu kwa Rais Samia. Na wapo ni wanyenyekevu kwako lakini sio wanyenyekevu kwa Allah.

Somo la Semantic NI pana
 
Hayo utajibu wewe ukiijuwa lugha ya Yesu
 
Sasa kama hizo dini zilikuwa zinaendana na tamaduni za wenyeji kwann walikuwa wana zipinga?

Wanazipinga kwa sababu ni dini mpya zilizoanzishwa na miongoni mwa Watu wao. Sababu kubwa ni maslahi ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa mfano, Yesu alipokuwa anahubiri kuhusu habari njema(Injili) dini yake ya kiyahudi ilimpinga kwa sababu ya maslahi ya kisiasa na kiuchumi. Ni ishu ya Wafuasi na Kupata nguvu ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa zamani Dini ilikuwa ndio Siasa. Unapoanzisha dini zamani ni kama sasa uanzishe chama cha siasa.

Muhamad alipinga kuabudu sanamu katika Kaaba Kwa Sababu tayari alikuwa na mafungamano na ukaribu na baadhi ya Wayahudi na Wakristo. Alikuwa muumini wa Mungu mmoja. Ambaye kwa wakati huo waarabu kabla ya uislamu Allah alikuwa Chief god yaani mungu mkuu ambaye sanamu yake haikuwako kati ya zile sanamu ya miungu 360 zilizokuwa zinaabudiwa pale kaaba
 
Aisee! Kwa hiyo jamaa yuko zake Mbande! Halafu anajifanya yuko Maryland! 😁
 
Hayo utajibu wewe ukiijuwa lugha ya Yesu

Hao wote tunaowataja sio Waafrika.
Wana dini zao, wanamiungu yao, wanamila na desturi zao.

Ila mimi na wewe ambao ni waafrika tunaacha yetu tunakimbilia yasiyotuhusu. Huo ndio Ukoloni mamboleo wenyewe.

Kitendo cha muafrika kujitambulisha kama muislamu au mkristo kinadhihirisha jinsi ambavyo akili yake ilivyokufa, alivyotawaliwa.

Kitabu chenye kipo wazi ni kitabu cha kiarabu, wahusika ni waarabu, Maeneo yanayotajwa ni ya waarabu, sikukuu zote niza waarabu, mil na desturi zote ni za waarabu.
Halikadhalika na biblia. Sasa mambo ya utumwa ndivyo yalivyo.
 
Ungeweka mifano ya hizo nchi mjadala uwe mpana zaidi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…