Ukristo: Mungu hajakataza kuoa mke zaidi ya moja, dhana ya mwili moja si kuwa na mke moja, hata ukilala na malaya ninyi tayari ni mwili moja

kuoa mke zaidi ya mmoja kuna masharti na mazingira ambayo yanaruhusu kufanya hivyo tena mke aliyetangulia lazima akubali kwa ridhaa bila kulazimishwa ila tatizo naona wengi wanatoa sababu nyepesi zinazoongozwa na tamaa za kuoa mke zaidi ya mmoja hii ni kwa wote mkristo/muislamu mfano mke amezeeka ambapo anashindwa kumuhudumia mumewe na mume bado ana nguvu basi mke anaweza kumshauri mumewe aoe mke mwingine wa kumsaidia
 
Hata Shetani ana wajumbe Haji yeye kama yeye , Mungu naye ana wajumbe ambao ni binadamu ndo aliwatumia kuandika Kwa uongozi wake , ndio ni kweli hakuna kitabu kilichoshushwa kutoka Mbinguni , Iko hv kama huamin biblia basi we endelea na mpango wako , wanaoiamini pia wataendelea kuamini ....

Swala la Imani huwez mpangia mtu , katika masuala ya kiimani mi naamini biblia na sababu ninayo, Ila siamini katika mfumo wa madhehebu ambayo totatlly yapo kunyonyana ...na kwenye biblia hayapo
 
Sorry nimeongea Kwa muktadha wa biblia boss , kuna mambo mengine biblia imeongea Kwa lugua ya picha ..... Kama tutajadiliana kupitia biblia naamini tutaelewana lakini kama tukiamua tutumie facts zinazoonekana Kwa macho , Mila na desturi sidhani kama tutafika ,
 
Ok,ila tuheshimu kwamba sio kila mtu jamvini anafata biblia,hivyo basi ni vizuri kuitumia ila kupanua wigo wa matumizi pia ya common sense.

Ila sjaona kugusia swali nlilokuuliza ni lini watu watakuwa responsible for their actions and behaviours?
 
Huyu mmoja anavyonipelekesha na imagine ningekua na wawili sijui ningekuwaje.
 
Mungu aliumba mwanaume na mwanamke, sio mwanaume na Wanawake ingekuwa hivyo unavyotaka angeumba mwanaume na wanawake wanne tofauti, Ibrahimu hakuna na wanawake wengi, Bali alikuwa na Sarah pekee, baada ya Sarah kufariki akaoa mwanamke mwingine, Yakobo maandiko yanasema alimpenda Rachel na sio Leah hiyo ilikuwa ni matokeo ya roho ya uongo na Mungu aligundua hilo akamfunga Recho tumbo.

Hoja ya wanaume kunyimwa unyumba na wake zao ni kweli lipo linatokana na wanawake kukosa utii mbele za Mungu na mbele ya waume zao, na wanawake hutumia hiyo kama silaha ya kuwaadhibu wanaume Ndio kosa linapoanzia shetani anapata upenyo wa kusambaratisha kumbuka shetani hapend umoja, Ndio maana analeta suala ya wake wanne linaloonekana ni jema lakini kiuhalisia hakuwezi kukawa na umoja Kwa wanawake wanaoshea mwanaume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…