Ukristo na Uislamu ni Dini mbili zisizofanana kabisa

Mimi nimesoma tu mstari mmoja unao beba hii mada yote nikaachia hapo, pale ulipo andika kuwa
"Kuna MUNGU (Almighty GOD) kwenye Biblia na kuna Allah kwenye Koran"

Naomba utambue kuwa, wanao amini Almighty God ni Waislam kwani wao ndio wana amini kuwa kuna Mungu mmoja tu, asiye na mshirika na mwenye Mamlaka yoye. Allah ni jina lenye maana hiyo, yaani Mungu Mmoja, Asiye na mshirika, Asiye fanana na kitu chochote na Mwenye Mamlaka yote.

Ukisema Mungu Baba, Mungu Mwana na roho mtakatifu.... huyo sio Almighty God? labda kama huelewi maana ya maneno Almighty God!

Kuhusu masimulizi ya habari za Mitume yasikuchanganye kwani yale ni masimulizi tu; ndio sababu hata kwenye Biblia kila mtume amesimulia kivyake na ndio sababu tunapata makanisa mapya kila siku, huyu akifuata mafundisho ya Marko, huyu Paul nk nk nk
 
GOD na ALLAH ni majina mawili tofauti ujue...

Hizo MUNGU BABA, MUNGU MWANA, na ROHO MTAKATIFU zusikuchanganye... MUNGU BABA ndio the Almighty GOD, yeye hapokei maagizo, Mungu mwana actually ni YESU, na roho mtakatifu ni roho inayokuongoza wewe kwenye maisha ya kila siku hususani kwenye kutenda mema. YESU na Roho mtakatifu wote wanapokea maagizo kutoka kwa MUNGU BABA au MUNGU MKUU au kwa kimombo THE ALMIGHTY GOD.

Kwenye uislamu hakuna THE ALMIGHTY GOD, GOD The Son, HOLY SPIRIT... Huu utatu mtakatifu haupo katika uislamu, na ndio maana tunasema hizi ni DINI mbili tofauti kabisa zisizofanana.... Wakristo hawana ALLAH kwenye mafundisho yao
 

Tatizo lako lugha ya malkia inakupita kushoto
"Almighty God" maana yake ni nini?
 
Kuhusu masimulizi ya habari za Mitume yasikuchanganye kwani yale ni masimulizi tu; ndio sababu hata kwenye Biblia kila mtume amesimulia kivyake na ndio sababu tunapata makanisa mapya kila siku, huyu akifuata mafundisho ya Marko, huyu Paul nk nk nk
Ukizungumzia kuhusu makanisa mapya, nami nitakuuliza kuhusu ushirika mbalimbali wa kiisilamu; mbona kwenye uislamu kuna SUNNI, SHIA, IBADI ambao ulizaliwa OMAN... Bado na kwenye SHIA kuna makundi kama Waismaili na Wazaidi
 
Tatizo lako lugha ya malkia inakupita kushoto
"Almighty God" maana yake ni nini?
Tatizo sio lugha tatizo ni majina... Almighty GOD maana yake ni MUNGU MWENYEZI au muweza wa Yote.

ALLAH maana yake ni nini? Maana sisi kwetu kwenye biblia hakuna neno Allah, hata kwenye kiebrania au kigiriki lugha za mwanzo za mitume hakuna neno ALLAH
 
"Almighty" maana yake ni nini?
 
Kila mtu akaabudu anakoamini,huwezi kusema ww ulipo ni sahihi alipo mwenzio sio sahihi hilo tumuachie MUNGU mwenyewe.
Tusihukumiane sisi kwa sisi,mwenye hukumu na kauli ya mwisho kwa wanadamu wote ni MUNGU PEKEE
 
Ukizungumzia kuhusu makanisa mapya, nami nitakuuliza kuhusu ushirika mbalimbali wa kiisilamu; mbona kwenye uislamu kuna SUNNI, SHIA, IBADI ambao ulizaliwa OMAN... Bado na kwenye SHIA kuna makundi kama Waismaili na Wazaidi
Kwenye uislam wanatofautiana kwa yale mambo wanaita ya sunna (ukiyafanya ni vizuri ila usipo yafanya hayana madhara/ hupati dhambi) Na maanisha kwenye kuendesha sala/Ibada "Sunni na Shia kila kitu ni sawa kabisa. Mtu wa Sunni anaweza kuingia Shia akasa bila changamoto yoyote!
Waislam wakiwa ugenini huuliza msikiti, hawaulizi msikini wa Shia/Sunni.....

Tofauti kabisa na huko kwengine, wanatumia Biblia moja ila kila kundi lina msimamao wake;
Kuna wana amini Agano la kale, na kuna wengine hawaliamini, kwa kusema Yesu alibadilisha kila kitu nk ....
 
Na mtu wa IBADI naye anaruhusiwa?

Sasa kama kila kitu ni sawa, kwa nini mgawanyike
 
Umesema kweli kabisa.

Ila kuna kitu kimoja hizi dini mbili zinafanana kabisa. Shetani wa Kikristu na Shetani wa Waislam ni mmoja na wala huwezi kuta wanalumbana kuhusu shetani ni dini gani kati ya hizo 2.

Cha ajabu Mungu wao ni tofauti🤣
 
Na mtu wa IBADI naye anaruhusiwa?

Sasa kama kila kitu ni sawa, kwa nini mgawanyike
Kutokana na mapokeo wanatofautiana kwa sunna, vitu vidogo vidogo visivyokuwa na madhara kwenye Ibada; Hawa wanavaa suruali fupi, wengine hawanyoi ndevu, kufunga mikono wakiswali nk nk havibadilishi swala....
Umeulizia Ibad "Ibad Islam is similar to Sunni Islam in belief and ritual, with some slight differences in some secondary issues"
Umeona hapo, Ibadi wanaendana kabisa na Sunni kwenye kufanya Ibada ila kuna mambo mengine flan flan wanatofautiana....
 
Kwa kuongezea Yesu wa Bible alipigiliwa pale msalabani ila kwenye kitabu kingine ilifanyika ubadilishwaji wa ki aina akapigililiwa mtu mwingine, na Yesu wa kwenye Bible alipopigiliwa msalabani na baada ya kufa alipita kuwasalilimia akina Petro na Yohana, la kuzingatia hapa hakusema kuna mabikra 72 huko, kumbuka alisema kabla hajafa kwamba anaenda kuwaandalia mahali.🙂
 
Una uhakika gani kuwa hao waliondika biblia walichokiandika ni sahihi?

Mfuatano na mpatano wa mawazo.
Wewe ni nini kinacho kusadikisha kuwa kuruwan alipewa Muhammad. Pia kwa nini imani ya kiislam inategemea sana tamaduni, mila na desturi za kiarabu?
 

Hayo madhehebu katika uislam ni matokeo ya utofauti wa kiitikadi. Siyo jambo dogo. Inahusisha mambo ya msingi. Ndiyo maana Shiah, Sunni, Ahmadiyyah nk hawapikiki chungu kimoja. Kuna wengine wanawaona wengine ni makafiri. Juzi juzi tumesikia mapigano kati yao yaliyopelekea vifo vya watu.
 
Tatizo ni kuwa wengi tunaamini Mungu mmoja mwenye uwezo wa kila kitu, lakini halafu tunamvua huo uwezo tunamuacha mtupu! Kwa mfano, tunaposema Mungu ameumba kila kitu, je ameumba kwa mikono? Kuumba ni kufinyanga, nani alimuona Mungu akiwa na mikono? Lakini pia tunaposema Mungu atahukumu siku ya mwisho, je ataonekana kwa macho akitoa hiyo hukumu? Au ni nani alimsikia Mungu akiongea? Anaongea lugha gani? Lazima tuone maandiko yanatoa fununu gani za uwepo wa Mungu, na bahati nzuri dini kuu zote zinatoa mwanga. Agano la Kale au Torati inatamka katika uumbaji Mungu anasema Mwanzo 1:27
 
Din ya mnyezimungu
 
Unasema kiumbe kabla ya kuumbwa kilikuwa kinaishi wapi!
Kitaishije na hakipo au sijakuelewa?

Halafu mi kusema hivo vitabu ni vya kujitungia haimaanishi Mungu hayupo.

Hivo vitabu vina madhaifu kibao, Mungu hana haja ya kuandika vitabu,.
Mungu andike kitabu cha nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…