Ukristo ni dini ya kipagani, ni dini ya kuabudu jua

Hio siku sahihi ya saba ni ipi hali kalenda zimebadilika hii ya SAsa sio ile ya kwenye Biblia kule Hakuna neno jumamosi, Alhamisi, nk
 
Umenena kaka. Watu wanaruhusu kushikiwa akili zao
 
Tuanze na hiyo kupumzika...wewe huwa unapumzika hiyo siku ya saba?
Usikimbie swali kijanja. Tubaki kwenye hoja yako. Umesema Mungu ameagiza kuabudu siku ya 7.

Nimekuuliza swali.
Ni wapi kwenye amri ya 4 Mungu ameagiza KUABUDU siku ya Saba?

Kwenye hiyo Kutoka uliyonukuu, ni wapi Mungu ameagiza Kuabudu?

Nijibu hilo swali.
 
Mkuu,

Hoja yako inaijibu hoja ya mleta mada moja kwa moja. Jua ni ishara ya kuangaza,hakuna mkristo anaabudu jua,hata wasiokuwa wakristo mnalifahamu hili.

Pia kukusu jina la kristo siyo la ukweli au yehoshwa kuitwa YESU hiyo nayo siyo hoja. Waislamu humwita Yesu Kama Issa lakini haiondoi tafsiri kuwa ndiye yule yule,au wareno kumwita Bebeto,ni Yesu yule yule.

Sasa mesiha au masihi kwa kigiriki ni kristos ambapo bado maana haijapotea maana Ni mtu yule yule mmoja akiyekija katika misheni ileile. Na wafuasi wake wakaitwa wa-mesihi au tuseme wa-kristo,kumaanisha watu wa yule mtu aliyeitwa kristo/masihi.

Haya mambo ya dini na imani hekima inahitajika Sana kuyajadili.
 
Utashindana na imani zote duniani! Ila hutokuja kuishinda imani ya Kikatoliki.
 
Nasadiki kwa Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume", period

Na ndiyo dini ya ukweli ya Ukristu ambayo ilianzishwa na Mtume Petro alipokabidhiwa kondoo awachunge na Bwana Yesu Kristu (Mathayo 16:18). Wengine wote ni waprotestanti na wapinga kristo.

Wasabato siyo DHEHEBU LA KIKRISTU bali ni CULT iliyoanza baada ya Nabii wa Uwongo kushindwa utabiri wake juu ya mwisho wa Dunia kuwa ni mwaka 1844
 
Wewe kwa Imani yako inakupunguzia nini hao hata wakiabudu Upepo ?

Sijui kwanini watu wanakosa ustaarabu wa kufanya yao na kuacha wengine wafanye ya kwao; Hizi kelele zenu mara nyingine ni Kero na usumbufu kwa wasio na mlengo wowote

By the way Jua ndio centre of Life ulimwenguni ungekuwepo miaka mamilioni kadhaa yanayokuja na Nishati ya Jua (Hydrogen) itakapoisha ndio ungegundua umuhimu wa Jua; Bila Jua hakuna Solar System ambayo dunia ni part ya hio system
 
Utashindana na imani zote duniani! Ila hutokuja kuishinda imani ya Kikatoliki.
Nilishamshinda huyo ibilisi kitambo

Kwenye ufunuo kanisa katoliki linajulikana kama mama wa makahaba
 
Tapeli na jambazi wote ni wezi tu.

Hilo li dini lako na la mwenzko unaemponda yote hovyo tu. Hayo yaliletwa Afrika kuwapumbaza waswahili ili mjione bora dhidi ya wenzenu
 
Petro hakuanzisha dini inayoitwa Ukatoliki.
Hiyo dini ilianza na watawala wa rumi ambao waliamua kuingiza upagani kwenye ukristo ili waitawale dunia kidini.
 
Petro hakuanzisha dini inayoitwa Ukatoliki.
Hiyo dini ilianza na watawala wa rumi ambao waliamua kuingiza upagani kwenye ukristo ili waitawale dunia kidini.
Siyo kweli, unabisha kwa vile unataka kufurahisha nafsi yako. Warumi walipinga kanisa kwa karne 3 hadi Mfalme Costantine alipokubali.

Siku ya Pentecoste ndiyo mwanzo wa kanisa Luka 24:50-53 pale walipoanza kunena kwa lugha
 

Siku ya JUMAPILI, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya juma, SIKU YA BWANA aliyoshinda mauti na kufufuka [UFUNUO1:10] Tunaitenga maalum kumwabudu Bwana kwa sababu:-​

a) Ni sikukuu ya malimbuko ya mavuno ambayo ilifanywa katika Agano la Kale, SIKU YA PILI baada ya Sabato; Ikiwa ni utabiri wa Kristo ambao ni LIMBUKO lao waliolala [WALAWI23:9-14;1WAKORINTHO15:20].​

b) Ni siku ya ushindi ya Bwana wetu Yesu aliyofufuka, na kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwa Yesu [YOHANA 20:1,19,26 WARUMI 10:9].​

c) Siku ya kuja Roho Mtakatifu, Mwangalizi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika kanisa, ilikuwa siku ya Pentekoste ambayo ni Jumapili, siku ya pili baada ya sabato [MATENDO 2:1]​

d) Siku ya Pentekoste, Jumapili ndiyo siku ya kwanza ambayo kanisa la kwanza lilianza mahubiri na watu 3,000 wakaokoka na kuanza kusanyiko la kwanza la Ibada kanisani [MATENDO 2].​

e) Wakristo wa kanisa la kwanza walikusanyika Jumapili [MATENDO 20:6-12;1WAKORINTHO 16:1-2].
Sababu hizi, zinadhihirisha pia wazi wazi kwamba kuabudu Jumapili hakukuanzishwa na mfalme CONSTANTINE wala kanisa Katoliki.​

Biblia inatupa uhuru wote katika kuchagua siku ya kumwadhimisha Bwana [WARUMI14:5-6]. Vilevile ni muhimu kufahamu kuwa siku zote ni siku za kujifunza Neno [MATENDO 17:11;2:46].​

KUSHIKA SIKU, SIYO NJIA YA KUOKOKA​

Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili, sio njia ya kuokoka. Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote [WARUMI 10:​

 
Amri inayokataza kuabudu sanamu haijafutwa. Ndio amri ya kwanza kabisa ya Mungu kwa mujibu wa kanisa katoliki. Japo haijataja sanamu direct ila imekataza kuabudu miungu of which obviously sanamu is included.

Huwe siwezi kuargue sana juu ya mifumo ya ibaada, kwasababu haya kwetu ni mapokeo tuu. Na shida ya mapokeo ni kwamba yeyote akiwa vuzuri tuu katika kuyadefend anaweza kuonekana anasema ukweli, hataka kama anadanganya. Ndio maana hata biblia kila mtu uwa anaitafsiri kivyake na wate wanaonekana wanamake sense. Mapokeo.

Katika suala la kuabudu jua, alama zinaonesha ni kama kweli wakatoliki tunaabudu jua (Kutokana na evidance zako mleta mada). Lakini mbona katika ibaada za kikatoliki hakuna sehemu Jua linatajwa? Vipi kama mimi nitakuja na hoja kwamba Jua linatumika kama ishara ya Nuru, Utanipinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…