tafuta kwenye biblia yote, kama kuna neno katoliki. ukilipata urudi hapa tujadili. Ukweli ambao hauujui ni kwamba, Kanisa la kwanza, lile lililopo kitabu cha Matendo, halifanani hata nukta na katoliki. kanila la kwanza linafanana moja kwa moja na ulokole. halipo hata kwa wasabato, lipo kwa walokole. why?
1. Kanisa la kwanza lilihubiri wokovu, walokole wa sasa pia, ila katholic wanapinga wokovu, hawahubiri wokovu. wasabato pia.
2. kanisa la kwanza liliamini mtu akiokoka yapasa ajazwe Roho Mtakatifu, na anene kwa lugha. wakatoliki na wasabato wanasema hayo ni mapepo. hata padre hajawahi kunena, na kunena ni muhimu.
3. kanisa la kwanza waliongozwa na Roho Mtakatifu, walokole pia. ila wakatoliki na wasabato, wanaongozwa na akili zao pamoja na mapokeo.
kwa hayo matatu tu nakutoa knock out. Pia, nikitaja ulokole hapa simaanishi hao manabii na mitume wa uongo, hao sio walokole, ila wauza maji upako na mafuta. hao nao hawafanani kabisa na kanisa la kwanza, wapo fungu moja na wakatoliki, wasabato, walutheran (ukiondoa wanafellowship), waanglican, wajehova n.k. huu ndio ukweli mchungu. mwenye swali aulize.