Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu, tuwe wa kweli tunapotoa maelezo ambayo wengine wanapata mafundisho, usije ukahukumiwa kwa kupotosha! Lugha 120 zilizotamkwa siku ya Pentekoste ni lugha za mataifa na makabila yaliyokuwapo pale Yerusalem. Kumbuka kuwa Yerusalem ulikuwa ni mji mkubwa na njia kuu ya kibiashara uliokutanisha watu wengi tofauti tofauti. Lugha zilizonenwa siku hiyo zilizowashangaza wengi ni lugha za makabila yao mfano kigiriki, kiarabu, kirumi, kiaramai, kiebrania, kikushi, kihindi, kichina, kiyemeni, n.k. hizo ni chache tu. Ndiyo maana wale waliowasikia walishangaa kuwa hawa ni wayahudi wamejifunza wapi na lini hizi lugha wanazozitamka? Kunena kwa lugha unakosema wewe (kama watoto wachanga) ni kunena wewe na Mungu wako, dhamira yako ndiyo inaongea. Ukinena na mtu mwingine au hata muumini mwenzako hamtaelewa nini mnaongea kwa sababu mnatamka maneno yasiyo rasmi. Kwa ufafanuzi, nenda karekodi hayo matamshi au yaandike na umpe mtu mwingine uone kama ataelewa kitu!Inawezekana hujui historia au Biblia unaisoma kama kitabu cha hadithi au umekaririshwa.
Tuanze taratibu.
Kanisa la kwanza lilianzia wapi na nini zilikuwa sifa zake?
Kanisa la kwanza lilianza waliambiwa wasubiri na siku Roho Mtakatifu alipowashukia (Siku ya Pentecost) na walinena kwa lugha wote watu 120 na walipotoka hapo Petro ndo alihubiri sermon ya kwanza na watu 3000 wakaokoka.
Mbona sijaongelea mambo ya Muyahudi au mwarabu hapa wewe uneyatoa wapi?
Je Kanisa Kanisa Katoliki wananena kwa lugha?
Wakihubiri watu wanaokolewa?
Historia ya Kanisa Katoliki iko hivi (Hapa najua utakasirika)
Warumi walikuwa na dini yao ya kipagani na kwa sababu dola ya Kirumi ndo ilikuwa inatawala wakati ule watu wengi walilazimika kuifuata ile imani ya kipagani na ndo maana walikuwa hawakubaliania na mafundisho ya Yesu.
Walimkataa Yesu mpaka ikafika wakamtafutia kesi ya uongo ili wamuue na wakafanikiwa lakini mbegu aliyokuwa ameipanda Yesu ilizidi kustawi.
Wakaona njia pekee ni kuwaua wale wanafunzi wa Yesu waliwaua sana Kasoro Yohana tu ndo alikufa kwa uzee lakini haikusaidia kuizima ile mbegu ya Yesu.
Walipoona ni haizuiliki wakaamua kuingiza upagani wao katika uKristo na kubadili kutoka Roman kuwa ROMAN CATHOLIC.
Catholic maana yake ni Universal (Kwa kila mtu) yaani Roman kwa kila mtu.
Lakini ule upagani hawakuuacha waliendelea nao na ndo wakaziingiza doctrine kinyemela kama za
Sala ya Bikira Maria, ibada za wafu mwezi Nov na nyingine nyingi.
Wajanja walipostuka wakajua tumepigwa na walipohoji ndo wakafukuzwa na wengine kuasi ndo ukaanza uprotestanti.
Lakini kanisa la kwanza la Yesu si Roman Catholic, hili ni la kipagani na liliingiza upagani wao ndani ya Kanisa la Yesu baada ya kushindwa kulizuia au kulifuta Kanisa aliloliacha Yesu
Ili kukupa ufafanuzi, kama hutaki niambie tuache mada hiyo!Mbona sijaongelea mambo ya Muyahudi au mwarabu hapa wewe uneyatoa wapi?
Catholic sio dhehebuUkristo umejengwa juu ya Kweli ya Neno la Mungu siyo juu ya dhehebu fulani!
haya maelezo yamejitosheleza sana... na ndio uhlisiaNdugu, tuwe wa kweli tunapotoa maelezo ambayo wengine wanapata mafundisho, usije ukahukumiwa kwa kupotosha! Lugha 120 zilizotamkwa siku ya Pentekoste ni lugha za mataifa na makabila yaliyokuwapo pale Yerusalem. Kumbuka kuwa Yerusalem ulikuwa ni mji mkubwa na njia kuu ya kibiashara uliokutanisha watu wengi tofauti tofauti. Lugha zilizonenwa siku hiyo zilizowashangaza wengi ni lugha za makabila yao mfano kigiriki, kiarabu, kirumi, kiaramai, kiebrania, kikushi, kihindi, kichina, kiyemeni, n.k. hizo ni chache tu. Ndiyo maana wale waliowasikia walishangaa kuwa hawa ni wayahudi wamejifunza wapi na lini hizi lugha wanazozitamka? Kunena kwa lugha unakosema wewe (kama watoto wachanga) ni kunena wewe na Mungu wako, dhamira yako ndiyo inaongea. Ukinena na mtu mwingine au hata muumini mwenzako hamtaelewa nini mnaongea kwa sababu mnatamka maneno yasiyo rasmi. Kwa ufafanuzi, nenda karekodi hayo matamshi au yaandike na umpe mtu mwingine uone kama ataelewa kitu!
Kuhusu upagani siyo warumi tu waliokuwa wapagani, dunia nzima ya wakati huo ilikuwa inaabudi vinyago, mizimu, wanyama, milima, miti, mito, n.k. na wengine walikuwa hawana habari ya kuabudu chochote. Baba yake Ibrahim pia alikuwa mpagani na aliabudu sanamu. Wakati wa Yesu chini ya utawala wa warumi wayahudi wote walikuwa wanamuabudu Yehova kama Torati ya Musa ilivyowaamuru na hawakuzuiwa na utawala wa warumi. Shida ni kuwa wayahudi hawakupenda kutawaliwa, walitaka wajitawale wenyewe kupitia ahadi ya kupata Masihi na ndiyo Yesu anapotokea na kuwaambia kuwa mimi nimekuja kuwakomboa wana wa Israel lakini ufalme wangu siyo wa hapa ulimwenguni. Wayahudi wanagawanyika makundi, wapo wanaomkubali, wapo wanaomkataa na wengine wasiokuwa na msimamo. Kwa sababu Yerusalem ilichafuka mara baada ya kumuua Yesu, mitume wake na wafuasi walijificha na kufanya mambo yao kwa uficho wakiwaogopa wayahudi wenzao waliokuwa wakitaka kuwaangamiza kabisa ili mafundisho ya Yesu yapotee kabisa. Kwa kuwa Yesu alikwisha waambia kuwa nendeni ulimwenguni kote mkahubiri habari hii niliyowafundisha ndiyo maana maeneo yaliyokuwa ya kwanza ni yale yaliyofikika kwa urahisi yaani Asia Ndogo. Lakini, waliposhikwa baadhi ya mitume walisafirishwa kwenda Roma, Italia makao makuu ya Dola ya Kirumi ili washitkiwe na kuhukumiwa huko. Wakati wakiwa huko ndipo walipata nafasi ya kuwahubiria wayahudi wenzao na baadhi ya warumi na hata viongozi wengine walisikiliza mahubiri yao. Wayahudi wa Roma ndiyo waloanzisha ufuasi wa Yesu Kristo na kuweka makao huko kwa sababu Yerusalem kulikuwa hakuna amani tena. Ili Injili iende kwa watu wote basi makao makuu yakawekwa hapo. Maana ya neno Katoliki linapotoshwa sana, Katoliki (Catholic) ni 'kwa wote' pata tafsiri kwenye kamusi ya Kigiriki siyo kusikiliza propaganda!
Hujui history ya kanisani kweli ila ni nje ya mada, nimesema msingi wa ukristo wote ni Catholic, imesimama kua dominant kwa zaidi ya miaka 2000
em nieleze hiyo history,Hujui history ya kanisa
Mkuu ni nini kama siyo dhehebu?Catholic sio dhehebu
Asiyejua maana haambiwi maana! Hili ni somo na kwa wengine pia. Dhehebu au Madhehebu ni mtindo au namna au rasmi katika dini fulani ya kumuabudu Mungu. Mfano kusujudu, kupiga goti au magoti, namna ya kufunga mikono, n.k. na pia hata namna ya uendeshaji sala au swala, mazingira na majengo ya ibada na namna ya kuyatafsiri maandiko na uwepo wa misimamo hivyo vyote vinaonyesha tofauti ya dhehebu moja na jingine.Mkuu ni nini kama siyo dhehebu?
Katoliki ni dhehebu la mafundisho ya Yesu waliyoagizwa mitume kuyahubiri kwa watu wote na wafanye vile vile kama walivyoshuhudia wao wenyewe na ilivyoandikwa katika vitabu, siyo kama INAVYOTAFSIRIWA na baadhi ya madhehebu. Mvinyo ni pombe, wanatafsiri kuwa ni togwa. Mabinti wa Lutu walilala na baba yao (Lutu), je walimlewesha togwa?Mkuu ni nini kama siyo dhehebu?
kanisa la mitume originally kutoka kwa mitume madhehebu ni makanisa yaliyochomozaMkuu ni nini kama siyo dhehebu?
Hao waroma unaowasema ni kina nani? Fafanua, hueleweki.Jamani waroma, mnafanya vizuri duniani elimu, afaya, nk. Lakini hayana uhusiano wowote na Mungu. Bila kuongozwa na Roho Mtakatifu utaenda kuishi Kwa shetani mjue! Hilo mnalijua vizuri, kuwa na mapesa na kumiliki ardhi kubwa hakusaidii chochote mtafuteni Mungu!
wapo kapu moja ndugu, wote motoni. kwa sababu wapo tofauti kabisa na kanisa la kwanza lile la kitabu cha MATENDO YA MITUME.we siku nyingine usurudie kufananisha Catholic na wasabato sawa
Unajua maana ya biasness kwenye maandiko. Mfano ukisoma andiko la msabato hakunamahali atalisemea vema kanisa la RC, ukikutana na mwislam hatolisemea vema Ukristu.Search
1. Penis steeple.
2. Circe or Kirk.
Anzia hapo.
Hayo maneno yote yanalenga neno Kanisa based on etymology na symbolism yanashambulia ukatoliki wapi ?Hayo maandiko umefanya selection TU ya waliolisema vibaya RC. Lakini Ukristu ni ukatoliki hakuna wa kukipinga Hilo na itaendelea kuwa hivyo. Hii ni Kwa sababu ndio waanzilishi, ndio walipitia madhila makubwa duniani na kuendelea kuwepo hadi Leo.
Ukatoliki sio Ukristo,upo mbali mbali kabisa ,Ukiamini kuwa Ukatoliki ni upagani basi ujue kuwa madhehebu yote yanayotokana na Ukatoliki ni wapagani.Anglikana,Luthery,Assemblies..
Biblia inamuita Roma kahaba mkuu ,na hao wanaofata mafundisho yake wanaitwa mabinti zakeMengi yanaupagani wa Kikatoliki. Kama kuabudu mioto(Mishumaa), Sherehe za kipagani(Christmas), Kutumia sanamu nk nk.