Ukristo umejengwa juu ya msingi wa Roman Catholic. Ipo Dominant kwa zaidi ya miaka 2000

ukristo umeanza 30 AD

imani strong ina dominate na ndo maana watu wamejikuta wameacha na wamehamia kwenye ukristo kwanini ya mababu haikuenda kusambaa ulaya ?
We kula ugali ukanyee haya mambo ya dini waachie waliokuletea
 
Kwani wewe shida yako ni nini? UKATOLIKI TU? Kwa hiyo wewe unaabudu miti na milima ambayo iliumbwa kabla yako, maana mwanadamu aliymbwa siku ya 6, kwa maelezo" Na tumfanye mtu kwa mfano wetu." "AKATAWALE VITU VYOTE." Umelala, amka!
Achana na hizo stori endeleaa kula ugali na kufanya kazi
 
Tunazungumza dini au siasa? Maana hata Muhammad alikuwa na mambo mawili, kutawala dola ya kiislam na kueneza Qur'an. Yesu alikataa utawala wa kidunia na alikubali ufalme wa mbinguni!
Quran, bibilia vyote upuuzi mtupu
 
je ni dini gani iliyoanza sawa na Catholic, zote zimekuja miaka mingi sana baadae mingi sana alafu zikachomoza kutokea huko huko, iliyo anza kivyake ni uislamu na yenyewe pia ilikua baadae sana almost miaka 60 baadae
Achana na stori za dini utapoteza muda wewe
 
Wewe tafuta mitume wa kiafrika uwasome achana na hao wa kuletewa
 
haya
 
Kuna kitu huwa najiuliza kwanini Pasaka ikipangwa na Roman Catholic, na makanisa mengine yanatumia siku hiyo hiyo. Kwanini Lutheran wasiwe na siku yao na wengine
system nzima ya Ukristo bado Catholic ana control ni ngumu kwao kujiwekea yao, Catholic ina organize hiyo siku ki dunia ila makanisa mengine ni ngumu kufanya hivyo pia wakiwa na yao haitakua na uzito uliozoeleka keaiyo ni ngumu hata kuanza
 
historia nzima ya Ukristo imeshikiliwa na kanisa katoliki hilo halipingiki
 
Wewe tafuta mitume wa kiafrika uwasome achana na hao wa kuletewa
Hata hao Mitume wa Kiafrika wanafanya kazi ya kumhubiri huyo huyo Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai na atakayekuja kuhukumu wazima na wafu! Pole sana!
 
Hata hao Mitume wa Kiafrika wanafanya kazi ya kumhubiri huyo huyo Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai na atakayekuja kuhukumu wazima na wafu! Pole sana!
Simaanishi hawa wapayukaji Mimi namanisha miungu wa kiafrika walikuwepo huko zamani na watu waka survive bila hizi dini za ukristo na uislamu
 
Simaanishi hawa wapayukaji Mimi namanisha miungu wa kiafrika walikuwepo huko zamani na watu waka survive bila hizi dini za ukristo na uislamu
Kabla hujajua kujenga ulikuwa unaishi kwenye mapango, maana yake ulikuwa unajua kujihifadhi ili kuwa salama kwa wanyama, baridi na faragha nyingine. Baadaye ukaona mtu anatoka kwenye nyumba (bila kujali ni ya tope, mawe au miti), ukamuiga kujenga ukaboresha faragha yako na hifadhi yako. Wewe ulijua kuwa kuna Mungu toka zamani lakini hukujua namna bora na kumuabudu na akakujulisha kupitia mtu mwingine. Tujifunze kuwa maisha bora mi mchakato wa mabadiliko ya mazingira na elimu ya ufahamu wa kujitafutia maisha maisha bora zaidi na zaidi. Ulitaka tuendelee kuishi vichakani kama Wahadzabe? Tumejifunza mangapi kutoka kwa hao Wazungu na bado tunawategemea?
 

Nakubaliana nawe. Ukristo na uislam vimejengwa
Nakubaliana nawe. Si Ukristo tu uliozaliwa na kujengwa
Nakubaliana nawe. Siyo ukristo tu. Hata uislam pia. Jikumbushe namna ulivyoiba au tuseme kudukua agano la kale na kuongeza ngano kidogo na kujipa na kujipatia ufuasi na uhalali. Kimsingi, bila ukristo na ngano zake za Adam na Ibrahim (Abrahamic religions0, hakuna uislam. Kadhalika, ukiangalia uarabu na uislam, utaona hili wazi wazi.
 
tafuta kwenye biblia yote, kama kuna neno katoliki. ukilipata urudi hapa tujadili. Ukweli ambao hauujui ni kwamba, Kanisa la kwanza, lile lililopo kitabu cha Matendo, halifanani hata nukta na katoliki. kanila la kwanza linafanana moja kwa moja na ulokole. halipo hata kwa wasabato, lipo kwa walokole. why?
1. Kanisa la kwanza lilihubiri wokovu, walokole wa sasa pia, ila katholic wanapinga wokovu, hawahubiri wokovu. wasabato pia.

2. kanisa la kwanza liliamini mtu akiokoka yapasa ajazwe Roho Mtakatifu, na anene kwa lugha. wakatoliki na wasabato wanasema hayo ni mapepo. hata padre hajawahi kunena, na kunena ni muhimu.

3. kanisa la kwanza waliongozwa na Roho Mtakatifu, walokole pia. ila wakatoliki na wasabato, wanaongozwa na akili zao pamoja na mapokeo.

kwa hayo matatu tu nakutoa knock out. Pia, nikitaja ulokole hapa simaanishi hao manabii na mitume wa uongo, hao sio walokole, ila wauza maji upako na mafuta. hao nao hawafanani kabisa na kanisa la kwanza, wapo fungu moja na wakatoliki, wasabato, walutheran (ukiondoa wanafellowship), waanglican, wajehova n.k. huu ndio ukweli mchungu. mwenye swali aulize.
 
Acha kushikiwa akili wewe waafrika walikua na teknolojia Yao tangu mwanzo na waliishi bila kutegemea mzungu na nikwambie tu kama siyo kitawaliwa na wazungu Leo hii watu weusi tungekua na nguvu kubwa sana hapa duniani.
 
ndio ni hiyo ni kweli kitu ambacho wakristo wanatofautiana na wakristo ni kumuamini Kristo

kitu hakiwezi kufanana kwa zaidi ya asilimia 50 na kingine na kikawa hakikuchukua kitu kutoka sehemu hiyo,


uislam pia umekuja miaka mingi baada ya ukristo. nao ni abrahamic religion!
 
Hiyo catholic ni mpinga kristo.
Baada ya kuzuia Injili kwa upanga bila mafanikio mpinga kristo akavaa joho la dini ambayo ni Catholic baadaye akaja kwa dini nyingine ya Uislamu.
The same devil but in two face.
The real way is to receive Christ and be baptized in deep water then be filled with Holy spirit.
 
na ndo madhehebu yote ya ukristo yalipo chipukia
 
we siku nyingine usurudie kufananisha Catholic na wasabato sawa
 
Acha kushikiwa akili wewe waafrika walikua na teknolojia Yao tangu mwanzo na waliishi bila kutegemea mzungu na nikwambie tu kama siyo kitawaliwa na wazungu Leo hii watu weusi tungekua na nguvu kubwa sana hapa duniani.
Tatizo ni kuwa unazunguka halafu unarudi tena pale pale. Waafrika kama walikuwa na teknolojia yao hapo mwanzo, hiyo teknolojia mbona haikuwasaidia wasitawaliwe? Hata mwarabu (bedui) wa kule jangwani Arabia alikuwa na teknolojia ya kuishi jangwani lakini leo hii kuna maghorofa, je amlaumu myahudi?
 
Mbona sijaongelea mambo ya Muyahudi au mwarabu hapa wewe uneyatoa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…