Huwezi kujibu wewe muongo, ngoja tukusaidie!
"Wattakhadhuu ayati warusulih khuzuwa"
Hiyo ni aya katika sehemu ya Qur'an Mungu anasema:
"Wao aya zetu na mitume yetu wakachukulia mzaha mzaha"
Na aya ilipoanzia inasema hawa watu malipo yao ni moto wa Jehannam.
Sasa ili Mtume kutuzuia huko ili tusichukulie aya za Mungu na mitume zake mzaha mzaha akatuonya, akasema:
"Mtu atakayesema kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu akatumia rai yake, Mapema makazi yake ajiandae motoni."
Ili wewe Sheikh
ndengisivilii usichukulie aya za Mungu mzaha mzaha kwa sababu ukijitafsiria mwenyewe utakuwa unafanya mzaha mzaha.
Ili usiingie motoni jehennamu inakubidi aya za Mungu uzitafsiri kwa nyenzo zake. Ukitafsiri mwenyewe utazifanyia mzaha mzaha.
Nyenzo za tafsiri ya Qur'an ni tatu:
1)Qur'an bi Qur'an
2)Qur'an bi Sunna
3)Qur'an bi Swahaba
Kuhusu wapi wameamrisha swala 5 angalia Qur'an surat -Nisa’ 4:103 tafseer ya ibn Abbas.
Zipo aya nyingi ila kwa hili anzio hapo!