VN Warehouse Limited
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 1,139
- 1,156
Habari wana JF,
Kuna kipimo ambacho wafanyabiashara wengi hawakiangalii wanapopima ukuaji wa biashara zao.
Wengi huangalia:
•Mauzo yameongezeka?
•Stock inaisha?
•Faida ipo?
Lakini kuna swali moja la msingi sana:
Ni wateja wangapi wanaokuja kwako ambao hawakuwahi kukujua kabla ya kuanzisha biashara?
Mara nyingi tunaanza biashara tukisaidiwa na:
•Marafiki
•Ndugu
•Watu wa kanisani/msikitini
•Watu wa mtaani
Wafanyakazi wenzetu wa zamani
Hawa huja kuku-support.
Wanakuja kwa sababu wanakujua, sio kwa sababu brand yako inawavuta.
Na hilo si jambo baya - ni hatua ya mwanzo.
Lakini tatizo linaanza pale ambapo baada ya miezi au miaka kadhaa, wateja wako wakubwa bado ni wale wale uliokuwa unawafahamu kabla hujaanza.
Hapo tambua bado haujajenga soko - umejenga mtandao wa mahusiano.
Mfano 1:
Umefungua duka la vifaa vya ujenzi.
Mwezi wa kwanza unauza sana kwa sababu marafiki zako wa WhatsApp wame-share, ndugu zako wamekuja kununua, watu wa karibu wameleta mafundi wao.
Lakini baada ya mwaka mmoja, ukiangalia wateja wako 70% ni watu wale wale.
Hapo bado hujapenya soko.
Umejenga circle, hujajenga brand.
Mfano 2:
Una saluni.
Wateja wengi ni marafiki zako na dada zako uliosoma nao.
Lakini hakuna mteja anayekutafuta kupitia Google, Instagram au kupita tu kwa sababu ameona huduma yako.
Hapo bado unategemea jina lako binafsi, sio biashara yako.
Mfano 3:
Unafanya supply ya vifaa kwa kampuni.
Kama mikataba yako mingi inatoka kwa watu waliokujua zamani, je kesho wakiondoka au kuhamishwa, biashara yako itabaki imara?
Biashara iliyokua kweli ni ile ambayo:
•Watu wanakuja kwa sababu ya huduma, sio kwa sababu ya urafiki
•Watu wanakulipa kwa sababu ya ubora, sio kwa sababu ya kukuonea huruma
•Watu wanakutafuta hata kama hawajawahi kukutana na wewe
Mteja wa kweli ni yule anayekutafuta kwa sababu ana hitaji - na anakuona wewe kama suluhisho.
Kama leo ukiamua kufunga simu na kutowatafuta marafiki zako, je mauzo yataendelea?
Hiiko ndicho kipimo cha ukuaji.
Kama wateja wengi bado ni wale wa zamani, basi kazi yako mpya ni:
•Kujenga brand
•Kuboresha huduma
•Kuweka mfumo wa masoko
•Kuonekana mtandaoni
•Kuweka standards zinazoleta wateja wapya
Biashara haiwi kubwa kwa sababu una network kubwa.
Inakuwa kubwa pale inapoanza kuvutia watu usiowajua.
Support ya mwanzo ni mtaji mzuri.
Lakini ukuaji wa kweli unatoka kwenye soko lisilokujua.
Jiulize leo:
Je biashara yangu inakua, au bado inaishi kwa support ya mahusiano?