Ukuaji wa lugha ya Kiswahili: Neno Mbashara

ijoz

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
731
Reaction score
715
Sikuwahi kufahamu kuwa katika kiswahili kuna neno linaitwa mubashara, likimaanisha "matangazo ya moja kwa moja yaani live".

Jana kwa mara ya kwanza nilivyoona hilo neno chini ya nembo ya ITV nilidhani ni kifupisho cha maneno fulani.

Hivyo tuendelee kujifunza lugha yetu adhimu:

Mbashara (si mubashara) = Live
Sharubati = Juice
Tufaa = Apple
Nywila = Password

 
mubashara ni neno lakiarabu lenye maana ya (moja kwa moja,wazi,bila sutra)
Wananchi walijitokeza kwa wingi kuangalia 'mubashara' mechi ya wakimataifa...
wananchi walijitokeza kwa wingi kuangalia mechi ya kimataifa mubashara
 
mubashara ni neno lakiarabu lenye maana ya (moja kwa moja,wazi,bila sutra)
wananchi walijitokeza kwa wingi kuangalia mechi ya kimataifa mubashara
Haswaaa ustadhijuma...ni mushabara mwanzo mwisho hakuna kificho.
 
Bila shaka. Pia ni muhimu tuache usisisi katika lugha yetu adhimu.

Kimfaacho Mtu chake.
 
Mubashara ni neno la kiarabu lenye maana moja kwa moja au Live
 
Reactions: EHK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…