Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Nimawasalimia wana JF wote.
Leo nimeona niweze kuelezea mambo muhimu sana ya nchi niliyoweza kuyapata miaka ya 90s.
Miaka hiyo nilitokea kumpenda mtoto mmoja wa kike jina lake akiitwa Misoji. Kusema kweli mwanamke huyo sitamsahau katika maisha yangu. Yeye ndiye aliyenifundisha mambo mengi sana kuhusu Ulimwengu wa Nuru na ulimwengu wa Giza. Japo kuwa nilikuwa muumini mzuri na nilikuwa nasoma vitabu vya dini na kukariri maandiko. Baada ya kukutana na Misoji niliweza kujifunza mambo mengi sana.
Siku moja baada ya kukutana na Misoji aliniuliza swali, Nikikuonesha vitu vizito vya dunia hii utakuwa na uwezo wa kustahimili? Ili kuonesha uanaume wangu nilisema Mpenzi hakuna kitu chochote utanionesha nikatetemeka.
Basi Misoji kwa jicho la upole na mahaba akatikisa kichwa na kusema basi naomba ukae siku mbili kwa kutafakari kisha baada ya hapo tuje kuonana saa sita usiku kwenye mbuyu uliokuwa unajulikwana kwa jina la Lyabatogwa. Bila kufikria sana nikasema sawa mpenzi wangu.
Siku hizo mbili nilizingojea kwa hamu sana, maana nilikuwa bado sijaonja tunda lake. Nilikuwa fika najua siku hiyo ndiyo siku muhimu sana ya kwenda kupata moto moto. Saa ilipofika nilijisogeza mpaka kwenye mbuyu ule. Eneo hilo lilikuwa limetulia sana na nilikuwa pekee yangu yapata kama dakika thelasini. Baadaye baridi ikaanza kuniyemelea kidogo kidogo, huku mbu wa hapa na pale wakijivinjari kwenye mwili wangu.
Muda kidogo kwa nyuma yangu nilisikia sauti ya Misoji ikiniita jina langu, Hanga! Hanga! Hanga! upo tayari, Niligeuka na kukutana na Misoji akiwa ameambatana na wasichana wengine wawili. Niliitikia ndio nipo tayari.
Basi yule msichana mmoja akauliza je, Misoji unauhakika huyu atafaa kweli? Misoji akasema ndio ninaouhakika kabisa. Basi! sikuelewa walikuwa na maana gani.
Walichora ardhini dura huku pembeni wakaweka vitu vyenye rangi nyeupe. Wakaniambia ingia kwenye hii duara. Huku nacheka cheka, huku moyoni ninajisemea hivi vitoto vya kike vinaleta michezo ya kitoto ngoja niingie kwenye duara nivifurahishe. Sikuchelewa nikaingia katikati ya duara. Baadaye wakaniweka katikati wakiwa wamesimama kwenye kingo za duara. Kila mmoja aliwasha moto na kushirikilia kupitia vijiti walivyokuwa wamevishikiria.
Wakaanza kuongea maneno. Kwakweli lugha ile sikuifahamu walikuwa wanaongea lugha gani.
Waliendelea kuonge maneno hayo kama dakika kumi hivi. Nilianza kusikia sauti za watu wakiongea, sauti za kiume na sauti za kike. Kila mmoja anasema "huyu amekuja huku ataweza?", Wengine wanasema tumpe muda na tumfanyie mafunzo maana ndio leo kafika.
Ghafla kuna mwanga mkali ulitokea mbele yangu mithili ya mlango ukifunguliwa na ndani ya mlango huo kuna taa kali. Baadae Misoji aliniambia twende. Tuliongozana na wasichana hao watatu kuingia kupitia lango hilo.
Nilipigwa bumbuwazi baada ya kuingia na kuona kuwa ni mji uliojengeka sana, nilianza kushaanga magari yanapishana, watu wengi wakinunua na kuuza. Watu wamevalia mavazi yenye thamani kubwa. Nikamuuliza Misoji, hapa ni wapi? Alisema sasa tumeingia dunia iliyochini ya Ardhi, hapa ulipo ni nchi inayoitwa Gamboshi. "Niliposikia neno Gamboshi nilianza kutetemeka nikajua fika sasa hawa wasichana wamenichukua niwe msukule". Nilijikaza kisabuni, huku ndani nateketea taratibu.
Tukakutana na mama mmoja aliyekuwa anatusubiri akasema Misoji njooni huku mwenyekiti wa hapa anataka kijana huyu aandikishwe.
Nimeitwa mara moja na boss. nitaendelea......