Ukumbi wa Arnautoglo safari ndefu ya Mwalimu Nyerere ilipoanzia

"Julius Kambarage Nyerere, mwalimu wa shule asiyefahamika sana kutoka Pugu alikuwa anagombea nafasi hiyo dhidi ya kijana maarufu wa Dar es Salaam na Kaimu Rais wa TAA na Katibu wake, mtoto wa mwanasiasa na mfanya biashara maarufu wakati wake, Kleist Sykes, Abdul akiwa Market Master Kariakoo Market."

Hivi kwanini ukimsema Nyerere ni lazima uonyeshe alikuwa duni tu ??
 
hapana hujalijibu ila umeongeza details ngoja nifafanue, abdul alitamani nyerere ashinde lkn aligombea na hakuwaweka wazi wafuasi kuwa msinipigie kura, kura zangu mpeni nyerere(kampeni) hapo huoni kuwa abdul angeshinda coz tayari alikuwa anajulikana zaidi ya nyerere? mkuu said zipo chaguzi nyingi ambazo wagombea walishinda uchaguzi bila kampeni bila shaka unafahamu. Sasa pia nilitaka kufahamu nyerere alipata kura ngapi na abdul alipata ngapi?
Blac,
Uamuzi uliopitika ni kuwa Nyerere ndiye anaefaa kuongoza harakati za kudai uhuru.
Kwa ajili hii basi ile inner circle ya TAA ya Hamza Mwapachu, Abdul na Ally Sykes,
Dossa Aziz
na John Rupia hili walikuwa wanalifahamu lakini haya mambo yalikuwa
siri kubwa wasingeweza kusema hadharani kuwawanataka kuunda chama cha siasa
kudai uhuru kwa hiyo mchagueni Nyerere kwa kuwa ndiye atakaekuwa kiongozi wetu.

Tewa Said Tewa hakuwa katika inner circle lakini Abdul alimweleza kuwa Nyerere
ndiye atakaechukua uongozi kutoka kwake.

Mazungumzo haya walifanya usiku kuamkia siku ya uchaguzi.

Bila shaka kwa wale ambao waliokuwa wakifahamiana kwa karibu zaidi walipeana
msimamo ule wa mtu kwa mtu.

Nasema haya kwa kuchukua jinsi Abdul alivyozungumza na Tewa.

Hili la idadi ya kura ni katika moja ya ''mysteries,'' katika historia ya TANU.
Ikutoshe tu kuwa hii historia ninayokupeni hapa hakuna mahali popote ilipoelezwa
ukitoa kitabu cha Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika.''

Nyerere mwenyewe hajapata kuleleza popote kama aliwahi kugombea nafasi ya
rais wa TAA na Abdul Sykes.

Ikiwa kama vile hapakuwa na uchaguzi baina ya Abdul na Nyerere hizo kura vipi
leo tutajua idadi yake?

Hakuna anaekumbuka idadi ya kura kwa wote ambao nilio wahoji.
Judith Listowel katika kitabu chake anasema Nyerere alipita kwa kura chache.
 
Marashi,
Ungeweza kuliuliza au kutoa fikra zako kiungwana.
Hivi ungenipa nafasi ya mimi kuchangia ninayoyajua.

Mzee Salamu, nipo nje ya mada, nilikua nakuuliza kuhusu mwandishi Amir T. Mohamed wa Zanzibar, naomba nipate historia yake kwa ufupi, asante
 
Kinachonifurahisha wakati huo kulikuwa hakuna udini ukabila wala ukanda.
Wakati ule waliyokuwa wanapigania uhuru walikuwa hawashughulishwi na dini zao au makabila yao au ukanda wao wao walikuwa wanapigania uhuru, tatizo ni baada ya uhuru.
Hata Afghanistan wale mujahidin waliyokuwa wakipigana na wasovieti walikuwa si magaidi lakini baada ya Afghanistani kushinda vile vita ndiyo kukazuka na majina ya kuitana magaidi.
 
Mwanzi1,

Suala la dini lilikuwapo lakini udini haukuwapo.

Katika majadiliano ya Nansio Mwapachu alimwambia Abdul kuwa Nyerere
mbali ya sifa nyingine zilizomfanya yeye awe anafaa zaidi kuongoza harakati
za uhuru, yeye kama Mkristo hii itaondoa hofu kwa Waingereza.

Wakoloni hawataiangalia TANU kama chama cha Waislam kinachotaka kuleta
vita kama ile ya Maji Maji mwaka wa 1905.
 
Wakati ule waliyokuwa wanapigania uhuru walikuwa hawashughulishwi na dini zao au makabila yao au ukanda wao wao walikuwa wanapigania uhuru, tatizo ni baada ya uhuru.
Hata Afghanistan wale mujahidin waliyokuwa wakipigana na wasovieti walikuwa si magaidi lakini baada ya Afghanistani kushinda vile vita ndiyo kukazuka na majina ya kuitana magaidi.
Vumilika,
Uhuru wa Tanganyika ulikuja na changamoto nyingi ambazo kwa
bahati mbaya katika jamii ziliwakumba Waislam peke yao.

Hili litahitaji uzi wake maalum.
 
Blac,
Uamuzi uliopitika ni kuwa Nyerere ndiye anaefaa kuongoza harakati za kudai uhuru.
Kwa ajili hii basi ile inner circle ya TAA ya Hamza Mwapachu, Abdul na Ally Sykes,
Dossa Aziz
na John Rupia hili walikuwa wanalifahamu lakini haya mambo yalikuwa
siri kubwa wasingeweza kusema hadharani kuwawanataka kuunda chama cha siasa
kudai uhuru kwa hiyo mchagueni Nyerere kwa kuwa ndiye atakaekuwa kiongozi wetu.

Tewa Said Tewa hakuwa katika inner circle lakini Abdul alimweleza kuwa Nyerere
ndiye atakaechukua uongozi kutoka kwake.

Mazungumzo haya walifanya usiku kuamkia siku ya uchaguzi.

Bila shaka kwa wale ambao waliokuwa wakifahamiana kwa karibu zaidi walipeana
msimamo ule wa mtu kwa mtu.

Nasema haya kwa kuchukua jinsi Abdul alivyozungumza na Tewa.

Hili la idadi ya kura ni katika moja ya ''mysteries,'' katika historia ya TANU.
Ikutoshe tu kuwa hii historia ninayokupeni hapa hakuna mahali popote ilipoelezwa
ukitoa kitabu cha Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika.''

Nyerere mwenyewe hajapata kuleleza popote kama aliwahi kugombea nafasi ya
rais wa TAA na Abdul Sykes.

Ikiwa kama vile hapakuwa na uchaguzi baina ya Abdul na Nyerere hizo kura vipi
leo tutajua idadi yake?

Hakuna anaekumbuka idadi ya kura kwa wote ambao nilio wahoji.
Judith Listowel katika kitabu chake anasema Nyerere alipita kwa kura chache.
umeeleweka vizuri hiyo sentensi alipita kwa kura chache nilidhani labda kura zilikuwa zinaeleweka kwa idadi.
 
Mohamed Said

Kuna hotuba moja ya Nyerere, alihutubia kuhusu heshima ya serikali na umuhimu wa serikali kukemea rushwa, alisema kuhusu Waziri aliyeiaibisha serikali kwa rushwa akawajibishwa. Alitaja pia tukio moja la Mgiriki ambaye alijitapa kwamba kaiweka serikali nzima ya Nyerere mfukoni mwake.

Nyerere alikasirika sana kwa kauli ile, akamfunga yule Mgiriki. Mgiriki alikuwa very well connected, akafanya mpango mpaka Kenyatta akamsihi Nyerere amuachie, Nyerere akakataa, akafanya mpango mpaka Askofu Makarios amuombe Nyerere amuachie Mgiriki yule, Nyerere, kwa kumuwekea heshima Aaskofu Makarios, akamuachia yule Mgiriki kwa sharti la kwamba asirudi tena Tanzania.

Nilikuwa najiuliza sana ilikuwaje mpaka Nyerere akamuheshimu vile Askofu Makarios. Nikafikiri labda ni kwa sababu Nyerere aliombwa sana, au anaheshimu viongozi wa dini wa kimataifa.

Lakini leo nimeelewa vizuri zaidi angle ya Wagiriki walioisaidai TANU tangu kabla ya Uhuru kina Arnatouglo na Aaskofu Makarios ilivyojenga heshima kwao kutoka kwa Nyerere.
 
"Julius Kambarage Nyerere, mwalimu wa shule asiyefahamika sana kutoka Pugu alikuwa anagombea nafasi hiyo dhidi ya kijana maarufu wa Dar es Salaam na Kaimu Rais wa TAA na Katibu wake, mtoto wa mwanasiasa na mfanya biashara maarufu wakati wake, Kleist Sykes, Abdul akiwa Market Master Kariakoo Market."

Hivi kwanini ukimsema Nyerere ni lazima uonyeshe alikuwa duni tu ??
Yamakagashi umesoma sentensi hiyo kuwa inamdunisha Mwalimu? Ni huku kusema hakuwa anafamika? Wapi kwengine unaona nimemdunisha Mwalimu. Mimi sijahisi kama hiyo ni lugha ya dharau lakini hebu nifafanulie.
 
Mkuu heshima kwako, sina mpango wa kuuliza hilo kwasababu kama kuna sababu ungeziweka tu kwenye bandiko lako ila fahamu tu nathamini na kuheshimu mchango wako kwenye historia ya nchi yetu.
Daudi,
Ndiyo sikuandika na wewe ulipenda niandike na ukauliza.

Tatizo hukuuliza kwa adabu umeghadhibika na umekuja na jeuri.

Mimi kuepusha shari na pia kukufunza ndiyo nakakuambia ukiuliza kwa adabu nitakupa jibu.

Hata hivyo nadhani ushalipata jibu kutokana na majibu yangu kwa wengine.

Hauko peke yako wanaoghadhibishwa na historia hii.
Historia inawataabisha wengi na wengependa kama tungebaki na ile historia yetu rasmi.
 
Daudi,
Ndiyo sikuandika ba wewe ulipenda niandike na ukauliza.

Tatizo hukuuliza kwa adabu umeghadhibika na umekuja na jeuri.

Mimi kuepusha shari na pia kukufunza ndiyo nakakuambia ukiuliza kwa adabu nitakupa jibu.

Hata hivyo nadhani ushalipata jibu kutokana na majibu yangu kwa wengine.

Hauko peke yako wanaoghadhibishwa na historia hii.
Historia imewashamgaza wengi na wengependa kama tungebaki na historia yetu rasmi.
Mkuu sighadhibishwi kabisa na maswala kama haya, mimi nimecheka tu kwasababu hicho kwangu ni kituko.
Nisamehe bure kama umehisi kuwa nimekukosea adabu.
 
Blac,
Uamuzi uliopitika ni kuwa Nyerere ndiye anaefaa kuongoza harakati za kudai uhuru.
Kwa ajili hii basi ile inner circle ya TAA ya Hamza Mwapachu, Abdul na Ally Sykes,
Dossa Aziz
na John Rupia hili walikuwa wanalifahamu lakini haya mambo yalikuwa
siri kubwa wasingeweza kusema hadharani kuwawanataka kuunda chama cha siasa
kudai uhuru kwa hiyo mchagueni Nyerere kwa kuwa ndiye atakaekuwa kiongozi wetu.

Tewa Said Tewa hakuwa katika inner circle lakini Abdul alimweleza kuwa Nyerere
ndiye atakaechukua uongozi kutoka kwake.

Mazungumzo haya walifanya usiku kuamkia siku ya uchaguzi.

Bila shaka kwa wale ambao waliokuwa wakifahamiana kwa karibu zaidi walipeana
msimamo ule wa mtu kwa mtu.

Nasema haya kwa kuchukua jinsi Abdul alivyozungumza na Tewa.

Hili la idadi ya kura ni katika moja ya ''mysteries,'' katika historia ya TANU.
Ikutoshe tu kuwa hii historia ninayokupeni hapa hakuna mahali popote ilipoelezwa
ukitoa kitabu cha Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika.''

Nyerere mwenyewe hajapata kuleleza popote kama aliwahi kugombea nafasi ya
rais wa TAA na Abdul Sykes.

Ikiwa kama vile hapakuwa na uchaguzi baina ya Abdul na Nyerere hizo kura vipi
leo tutajua idadi yake?

Hakuna anaekumbuka idadi ya kura kwa wote ambao nilio wahoji.
Judith Listowel katika kitabu chake anasema Nyerere alipita kwa kura chache.
mkuu mtu aliyepata kura chache alishinda vipi uchaguzi huo dhidi ya mwenye kura nyingi??

Ni kwanini isisemwe kuwa walitofautiana kwa kura chache??
 
Nakusudia ushindi mdogo na hata hivyo ulivyosema ni sawa pia.
 
Mkuu sighadhibishwi kabisa na maswala kama haya, mimi nimecheka tu kwasababu hicho kwangu ni kituko.
Nisamehe bure kama umehisi kuwa nimekukosea adabu.
Daudi,
Kwa namna ulivyokuja katika mjadala bila kujali kuwa unasomwa na wengi
kituko ni wewe.

Halafu unashangaa ati hujui kama umekosa ustaarabu.

Sijapata kuwa kituko katika maisha yangu yote na katika historia hii nimeandika
mengi na sijawahi kuambiwa kuwa nachekesha.

Tunabishana kwenye mengi na hatukubaliani ila kuwa kituko ilo sijapatapo kuwa.

Ikiwa haya ninayoandika kwako ni kituko inabidi ujitazame kama huu mjadala ni
makamo yako.

Nitakufahamisha jambo.
Wewe ulipatapo popote kuisoma au kusikia historia hii?

''Uamuzi uliopitika ni kuwa Nyerere ndiye anaefaa kuongoza harakati za kudai uhuru.
Kwa ajili hii basi ile ''inner circle;'' ya TAA ya Hamza Mwapachu, Abdul na Ally Sykes,
Dossa Aziz
na John Rupia hili walikuwa wanalifahamu lakini haya mambo yalikuwa
siri kubwa wasingeweza kusema hadharani kuwa wanataka kuunda chama cha siasa
kudai uhuru kwa hiyo mchagueni Nyerere kwa kuwa ndiye atakaekuwa kiongozi wetu.''

Hujapata wewe hata siku moja kusikia historia hii.
Unadhani mimi nimeitunga?

Nilitegemea wewe ushangazwe iweje hii historia haikuandikwa?

Au unachomwa kwa kuwa hukutegemea watu hawa kufanya makubwa kama haya?

Kwa kawaida kitabu kina umri wa kuishi kama viumbe vilivyo hai kisha kitabu hufa.

Kwanza sikutegemea kitabu changu kitavutia hisia za watu kiasi hiki kilichopo sasa.
Kitabu kipo huu mwaka wa 20 na tunakwenda toleo la nne.

Kitabu cha Sykes bado hai.

Juzi Pascal kanipongeza kuwa uzi aliofungua unaonihusu mimi post zilizoletwa ni
2000 na wafatiliaji ni 20000.

Unadhani hawa wanakuja hapa Majlis kusoma na kujadili vichekesho?

Ndipo hapo nimekutahadharisha ikiwa wewe unaniona mimi kichekesho basi jua
una tatizo.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kulikuwa na kozi inasomeshwa, ''Government and
Politics in East Africa,'' nami niliisoma.

Naamini kabisa kuwa walimu wangu wale walionisomesha kozi ile leo wakisoma
kitabu cha Sykes, watabadili mengi katika historia ya utaifa wa Watanganyika.
 
Umeyasikia popote majina hayo hapo chini ukitoa machache:

"Uchaguzi ule wa 1953 uliwaingiza katika uongozi Waafrika wengi kutoka nje ya Tanganyika khasa Kenya. Viongozi wa TAA walikuwa hawa wafuatao: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Makatibu wa muhtasari; Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah (Mnyasa), Z. James, (Mkenya), Dome Okochi (Mkenya), C. Ongalo (Mkenya) na Patrick Aoko (Mkenya). Dennis Phombeah na Ally Sykes walialikwa na Kenneth Kaunda rais wa African National Congress (ANC)kwenye mkutano wa vyama vya siasa Kusini ya Sahara uliokuwa unafanyika Lusaka, Northern Rhodesia na walifunga safari kwenda. Yaliyowakuta Salisbury, Southern Rhodesia wakati wako transit hapo iko siku In Shaa Allah nitaeleza hapa mkasa uliowakuta baada ya kukamatwa Salsbury na kupigwa PI."
 
UKUMBI WA ARNAUTOGLO SAFARI NDEFU YA MWALIMU NYERERE ILIPOANZIA

View attachment 1141636

George Arnautoglo alikuwa Mgiriki tajiri na ndiye aliyejenga jumba hilo akalitoa kwa matumizi ya Waafrika wa Tanganyika.

George Arnautoglo alikuwa hawapendi Waingereza kwa kuwa walikuwa wameikalia nchi yake Greece ambako Padri Makarios alikuwa akiongoza mapambano ya kudai uhuru.

Arnautoglo alipata kutoa fedha kwa siri kuwapa TANU zisaidie harakati za kudai uhuru na fedha hizi alimpa Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa mmoja wa viongozi wa juu wa TANU.

Kwenye Ukumbi huu wa Arnautoglo tarehe 17 April 1953 ulifanyika uchaguzi wa mwaka wa TAA kumchagua Rais na viongozi wengine.

Julius Kambarage Nyerere, mwalimu wa shule asiyefahamika sana kutoka Pugu alikuwa anagombea nafasi hiyo dhidi ya kijana maarufu wa Dar es Salaam na Kaimu Rais wa TAA na Katibu wake, mtoto wa mwanasiasa na mfanya biashara maarufu wakati wake, Kleist Sykes, Abdul akiwa Market Master Kariakoo Market.

Nyerere Tanzania's Political Forum. Tafadhali hakikisha hoja unayoiweka hapa ni ya kisiasa kweli!

Vipi Nyerere aliweza kumshinda Abdul Sykes siku ile ni kisa cha kusisimua katika historia ya Tanganyika na historia ya Mwalimu Nyerere.

Hapa kwenye jengo hili na siku ile ndipo Julius Nyerere alipoanza safari yake ndefu ya siasa na uongozi.

Hapa Nyerere alikuwa siku ile kavuka kiunzi kikubwa katika maisha yake ya siasa.

Meneja wa Ukumbi huu wa Arnautoglo ambae na yeye alishiriki katika kupiga kura ya kunyoosha mikono alikuwa kijana wa Kinyasa kutoka Nyasaland (Malawi) Dennis Pombeah.

Phombeah akiendesha pikipiki yake aina ya BSA alizunguka mji mzima kumfanyia Nyerere kampeni.

Abdul na wenzake katika TAA hawakufanya kampeni yoyote kwani walitaka Nyerere ashinde.

Imenichukua zaidi ya miaka 10 kutafuta picha ya Dennis Phombeah na mwisho nimeipata picha yake.

View attachment 1141637
Dennis Phombeah
Phombeah kama meneja wa Arnautoglo Hall kafanya mengi katika kuisaidia TAA hadi TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika historia ambayo si wengi wanaifahamu.

Lakini Dennis Pombeah alikuwa rafiki kipenzi wa Oscar Kambona...

View attachment 1141638
Picha: Ukumbi wa Arnautoglo, Dennis Phomeah Menaja wa Arnautoglo na picha ya tatu kulia Nangwanda Lawi Sijaona, Abdulwahid Kleist Sykes, Julius Kambarage Nyerere na Waziri Dossa Aziz katika Ukumbi wa Arnautoglo kwenye dhifa ya kumuaga Rais wa TANU Julius Nyerere safari ya pili UNO 1957
Kwa hiyo hapa unataka kusema huyo Abdul Sykes, al-wataan wa Kariakoo alishindwa sababu hakufanya kampeni, na Nyerere, Mwalimu fulani tu wa Pugu, alishinda sababu alifanya kampeni? Halafu hapohapo unadai Abdul Sykwes alikuwa anataka Nyerere ashinde? Kwanza tuambie vote tally ilikuwaje, siyo kutuletea hadithi za "alishinda kwa kura chache sana". Ni dhahiri jinsi ambavyo una pindisha mambo kwa kuipendelea hiyo famila tukufu kwako wewe ya SYKES.
 
Back
Top Bottom