Binafsi,kwa asilimia 95 , naamini Lissu atapata kura nyingi kuwazidi waitia nia wengine wanaowania kuteuliwa na chama kupeperusha bendera ya CHADEMA kwa nafasi ya uraisi ,na hili litadhihirika pale matokeo ya kura yatakapotangazwa.
Siku hiyo natarajia ukumbi utalipuka kwa shangwe na vigelegele ambavyo havitaishia tu ndani ya ukumbi bali shamrashamra hizo zitaendelea nje ya ukumbi na baadae kuhami mitandaoni.
Media za kimataifa nazo hazitakuwa nyuma katika kutangaza matokeo hayo huku Lissu akihojiwa aseme machache juu ya ushindi wake bila kusahau Mbowe kama mwenyekiti kwani ni lazima watataka maoni yake.
Ikitokea hiyo asilimia 5 ndio itatoa mshindi kwa maana ya Nyalandu,ukumbi utapoa ingawa wapo wachache watashangilia ila CCM ndio wataongoza kupokea kwa furaha matokeo hayo kuliko wana-CHADEMA wenyewe.
Kama ambavyo nimekuwa nikisema humu mara kadhaa,Lissu anabebwa na nyakati kwani hizi ni nyakati zake kama tusemavyo: "kila jambo na wakati wake" na wakati huu ni wa Lissu.
Tusubiri.