Ukurasa wa Serikali 'Tanzania Government' uliotumika kutangaza kutafutwa Kigogo2014, wafutwa

Sasa hivi umeongea vyema.

Haya sasa tuanze.

Page ya kwanza yenye blue tick ina hiyo email ya es@plancom.go.tz

Picha ya page iliyoondolewa blue tick kabla ya kufutwa haina hiyo email, ina website peke yake.

Kwa unavyoamini, mtu anayeweza kufungua hiyo page hawezi google ili kupata email ya ikulu? Aipachike tu hapo ili iwe more convincing?

Serikali ilitakiwa kuikana hii page. Nafikiri hawajaikana mpaka muda huu.
 
Mkuu badala ya kutuona sisi watanzania ni mambumbu mimi naoana ungejikita kutupa elimu ya kutofautisha Fake account na Genuine acc kwenye mitandao, Tutashukuru mkuu
Elimu unajipa mwenyewe. Hakuna mtu atakayekufuata kukupa elimu. Hii hii internet imejaa elimu kibao. Usikimbilie ku-follow mambo ya kijinga kama ya akina Diamond etc. Soma mambo ya maana.
 
wewe ulikuwa unalazimisha hiyo page imefunguliwa na ikulu nimekuwekea email address iliyofungua hiyo account unasema imepachikwa...Sasa unadhani kuna haja ya mimi kuendelea kupoteza muda wangu kwa mtu anaepambania umbeya uwe ukweli? wewe si umesema unaijua mitandao wewe why unauliza vitu ambavyo vipo very clear.

Haya mimi nakuacha na mahaba yako kwa upande wako uliouchagua.
 
Elimu unajipa mwenyewe. Hakuna mtu atakayekufuata kukupa elimu. Hii hii internet imejaa elimu kibao. Usikimbilie ku-follow mambo ya kijinga kama ya akina Diamond etc. Soma mambo ya maana.
Sawa mkuu sasa mbona ule ukurasa ulikuwa na Blue Badge? Je ili tujue ukurasa ni halali si tunangalia Blue badge ilikuwaje ile page ikawa verified?
 
Duh hatari.

Email inayotumika kufungulia akaunti siyo lazima iwe displayed kwenye profile. Email itakayokua displayed ni ile unayotaka members waione wakitaka kuwasiliana na wewe.

Ni kama humu tu. Tunatumia email kufungua Id lakini sehemu ya contacts tunaweza weka email nyingine ambayo tunataka memba wengine waione.

So hiyo email inaweza kua ilitumika kufungua page ama la ila ni email unayotakiwa tumia kuwasiliana nao.
 
Inaonekana teknolojia ya mawasiliano imekuacha mbali Sana! Lichunguze tangazo lile na utaiona tick ya rangi ya bluu yenye maana ya kuwa account Ile ni ya serikali ya Tanzania na imekuwa verified kwenye mtando husika! Upo bandugu? Next time tambua hadhira unayoiandikia kuwa Ina utaalamu kuliko wako hivyo hawadanganyiki kirahisi!
 
Naunga mkono hoja
 
Mkuu upo sahihi na hiko ndicho mama alichowauliza hao wanao hangaika na kigogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…