Ukuu wa Dollar ya Marekani umefika mwisho?

Ukuu wa Dollar ya Marekani umefika mwisho?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Short story. Nguvu ya Marekani ipo kwenye dollar yake anbayo ndiyo "sarafu ya dunia." Moja ya sababu inayofanya dollar iendelee kuwa sarafu ya dunia ni kutumika kwake kufanyia biashara ya mafuta. Biashara yenye pesa nyingi zaidi duniani.

Mwaka 1974 Marekani na Saudi Arabia(Akiwa mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta) kutumia dollar pekee kama sarafu ya kuuzia mafuta. Badala yake SA atauziwa silaha na kupewa ulinzi. Mkataba huo ulikuwa wa miaka 50. Mwaka huu mwezi wa sita mkataba huo umeisha na Mwanamfalme wa SA bado hajaonyesha nia yoyote ya kusign upya, na hata amekataa mualiko wa kwenda kwenye mkutano wa G7.

Je dollar itaanguka au US atamdhibiti SA kama anbavyo aliwadhibiti wengine waliojaribu kuchallenge dollar yake?
 
Hadi leo mtoa mada ujafahamu kwanini Dollar ina nguvu? Ukiwa mzalishaji mkubwa wa vitu na teknolojia watu watakuja kununua kwako kwa njia rahisi uliyosema.
Sasa chukulia SA atauza mafuta kwa pesa yake, swali ni kuwa yeye atanunua vingapi kwa pesa ya wengine?
 
Ni wangapi wanatafuta hiyo pesa ya SA kwenda kukitumia huko SA then uilingananishe na wanaotafuta pesa ya Marekani kwa ajili ya kukitumia.
Dollar kuanguka leo au kesho sidhani.
 
Moja ya sababu inayofanya dollar iendelee kuwa sarafu ya dunia ni kutumika kwake kufanyia biashara ya mafuta
Swali : Dola itaanguka???

Jibu: Ndiyo itaanguka, lakini ni ngumu kutokea kwa sasa!

Sababu ni nini? Uchumi wa dunia umetengenezwa na kushikamanishwa kupitia dola, kuanguka kwa dola ni kuanguka kwa uchumi wa dunia.

Siku dunia ikiamua kuacha kutumia dola kama sarafu kwenye hifadhi zake kwenye nyanja mbalimbali basi huo ndiyo mwisho wa dola!

Unaona kuna nchi inayojaribu kufanya hivyo kwa sasa??
 
Hadi leo mtoa mada ujafahamu kwanini Dollar ina nguvu? Ukiwa mzalishaji mkubwa wa vitu na teknolojia watu watakuja kununua kwako kwa njia rahisi uliyosema.
Sasa chukulia SA atauza mafuta kwa pesa yake, swali ni kuwa yeye atanunua vingapi kwa pesa ya wengine?
Marekani ilianza kupata trade deficit miaka ya 1970 huko. Si muuzaji wala mtengenezaji mkubwa wa vitu. Kinachofanya dollar iwe na nguvu ni hilo dili la kuifanya itumike kununulia mafuta. Ndiyo maana ya kuitwa Petrodollar.
 
Ni wangapi wanatafuta hiyo pesa ya SA kwenda kukitumia huko SA then uilingananishe na wanaotafuta pesa ya Marekani kwa ajili ya kukitumia.
Dollar kuanguka leo au kesho sidhani.
Kilichopo ni kuwa Saudi Arabia imekubaliana na Marekani kuuza mafuta yake kwa Dollar. Ndiyo maana huoni watu wakitafuta pesa yao kwenda kununua mafuta. Lakini leo wakisema wanauza mafuta yao kwa Riyal unafikiri ni wangapi wataanza kuisaka hiyo pesa?
 
Hadi leo mtoa mada ujafahamu kwanini Dollar ina nguvu? Ukiwa mzalishaji mkubwa wa vitu na teknolojia watu watakuja kununua kwako kwa njia rahisi uliyosema.
Sasa chukulia SA atauza mafuta kwa pesa yake, swali ni kuwa yeye atanunua vingapi kwa pesa ya wengine?
Mtoa mada kachagua kipengele kimoja tu kidogo kati ya vingi vinavyofanya dola ya USA iwe na nguvu. N combination of factors na siyo mafuta pekee. Ni wazi kuwa hakuna kitu kinachodumu hasa dola lenye nguvu (nchi) kwa sababu historia inatufundisha hivyo. Lakini sioni hayo aliyoyayasema yakitokea sasa hivi tena kwa haraka namna hiyo.
 
Swali : Dola itaanguka???

Jibu: Ndiyo itaanguka, lakini ni ngumu kutokea kwa sasa!

Sababu ni nini? Uchumi wa dunia umetengenezwa na kushikamanishwa kupitia dola, kuanguka kwa dola ni kuanguka kwa uchumi wa dunia.

Siku dunia ikiamua kuacha kutumia dola kama sarafu kwenye hifadhi zake kwenye nyanja mbalimbali basi huo ndiyo mwisho wa dola!

Unaona kuna nchi inayojaribu kufanya hivyo kwa sasa??
Nchi nyingi zinaanza kufanya makubaliano ili zifanye biashara kwa kutumia sarafu zao. BRICS wanapambana kushusha utawala wa dola. Saudi Arabia wanasita kusaini mkataba wa Petro dollar. Kuna harakati nyingi sana za watu kutaka kuachana na dollar. Kitendo cha akiba ya dollar za Russia kuwa frozen kimewafanya watu wengi waanze harakati za kuikimbia dollar.
 
Nchi nyingi zinaanza kufanya makubaliano
Sifahamu uelewa wako kuhusu uchumi wa dunia, inaonekana unataka kubishana, nimesema hapo juu, dola itaanguka kwani hakuna kitu kisichokuwa na mwisho hapa duniani.

Ila kwa sasa na kwa baadaye ni ngumu kutokea huu ni ukweli mchungu, huwezi kusema dunia itaachana na dola hata kwa miaka 50 ijayo, au wewe kwa kutumia akili yako unaliona hilo??

Walijaribu Mjapani, Mwingereza, Mchina na EU walikutana na ugumu coz ya uchumi wa kushikamanishwa na dola.

Kasome kwa nini world reserve currency iwe dola na siyo sarafu nyingine pamoja na manyanyaso yote dunia inayoyapata.

Ukweli mchungu: Dunia inahiitaji sana dola kwa sasa kuliko dola inavyohiitaji dunia!

Nb: Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, itakuja kuanguka ni suala la wakati na tunahitaji kuvumilia!
 
Back
Top Bottom