Ukweli gani mgumu umekubaliana nao baada ya kuwa mtu mzima?

Ukweli gani mgumu umekubaliana nao baada ya kuwa mtu mzima?

1. Maisha ya mtu yanapangwa na mtu mwenyewe... Kinachowezekana kwa mwingine si lazima kiwezekane kwako hata kama mnafanya au kupitia jambo linalofanana.

2. Hakuna bora kuliko mwingine. Anayepangilia mambo yake vizuri hufaidika mapema.

3. Umri haumzeeshi mtu au kumkomaza mtu, bali mapito yake na harakati zake.

3. Drug abuse haina shida ila shida ipo kwenye kusudio (akili) la mtu mtumiaji.
 
1. Dunia Haina huruma kwa mwanamke asiyekuwa na kipato chake
2. Kosea pote usikosee kuoa/kuolewa haijalishi ni Muslim/Christian
3. Kuna watu watakuja na wataondoka na hutakuwa na uwezo wa kuwauzia (marafiki, business partners)
4. Kukaa kimya ni Bora zaidi kuliko kujieleza ( ukija ukasema 1+1 = 200 natakiwa kukuunga mkono ili maisha yaendelee)
Michael Rainey Jr Yes GIF by Power Book II Ghost.gif
 
Noma sana wakuu!
Sio kuhusu mimi tena, ni wale jamaa niliokuwa nawatafuta miaka kadhaa nyuma. Kuhusu mimi itakuja tena baadae huko.
Unazungumzia nini hapo juu 👆👆👆
Nikiwa 20s nikadhani safari ya maisha ni ndefu sana, kumbe nilijidanganya, maisha mafupi sana, nakubali sasa nimekuwa mzee wa umri na kumbe sina mda nitawaachia wengine waendelee na hii dunia.
Kweli, mimi na wewe inawezekana tumeshaishi kwa muda mrefu zaidi hapa duniani kuliko muda tuliobakiza.
Watu wanakuja na kuondoka, marafiki wa 20s huenda usivuke nao hadi 40s, sisi tulio 60s tunatengeneza marafiki wa kuzeeka pamoja.
💯
Ngono na tamaa ya ngono ni vitu vya kupita tu, unafikia kipindi havina maana tena kwenye maisha.
Ni kweli kabisa!
 
Back
Top Bottom