bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,213
- 2,938
UMEKUWA UKILIPA KODI MAISHA YAKO YOTE. JE, UNAJUA NANI ALIYEVUMBUA MFUMO HUU NA KWANINI?
Kabla ya kuwepo kwa fedha, benki, serikali, au katiba... tayari kulikuwa na mtu aliyesimama mlangoni kwako akipiga hesabu ya kile unachopaswa kumpa.
Kodi ya kwanza kabisa duniani ilikusanywa miaka 5,000 iliyopita huko Mesopotamia. Hakukuwa na pesa! Watu walilipa kwa ngano, mbuzi, na kibarua.
Mkulima akivuna, mtu aliyeshika kibao cha udongo alifika na kuandika kiasi anachodaiwa na hekalu. Kibao hicho cha udongo ndiye babu wa fomu yoyote ya kodi unayojaza leo.
Mbinu yao ilikuwa ya kijasusi sana. Hawakusema "Tupe ngano kwa sababu tuna nguvu."
Walisema: "Tupe ngano yako, na njaa ikitokea, tutakulisha."
Hofu iliyovikwa wema. Mtego wa kibiashara wa kale zaidi katika historia ya mwanadamu.
Wafalme wa Misri walisafiri nchi nzima kukagua mifugo, mafuta, na mazao ili kukata kodi. Lakini Misri waliongeza kitu kipya: Mamlaka ya Mungu.
Farao alionekana kama mungu. Ukigoma kulipa kodi, hukuwa unamgomea mfalme ulikuwa unamgomea Mungu mwenyewe!
Matokeo yake? Piramidi kuu za Giza zikajengwa. Majengo ya kifahari zaidi duniani yakasimamishwa juu ya migongo ya watu ambao hawakuwa na hiari.
Je, kodi unayolipa leo unaiona kama 'ada ya maendeleo' au ni 'unyonyaji uliohalalishwa'?
Dola ya Roma iligundua mbinu hatari zaidi: Hawa walikuwa mabepari binafsi waliolipa serikali fedha mapema ili wapewe haki ya kukusanya kodi. Chochote walichokusanya juu ya hapo, kilikuwa chao.
Matokeo yake? Walimnyonya kila mtu kwa nguvu zote. Mkusanya kodi akawa mtu anayeogopwa na kuchukiwa zaidi. Ndio maana hata kwenye Maandiko Matakatifu, kula meza moja na mkusanya kodi ilikuwa balaa kubwa, rejea watu walivyo mlalamikia Yesu, kwenda kwa Zakayo.
Historia ya miaka 5,000 inafichua kitu kimoja: Kodi haijawahi kuwa kuhusu barabara tu.
Jamii inayodaiwa kodi kila mwaka ni jamii inayolazimika kuendelea kufanya kazi, kuingiza kipato, na kubaki ndani ya mfumo ambao serikali inaudhibiti. Huwezi kujitoa. Huwezi kutoweka.
Serikali haihitaji kumfunga raia pingu za chuma ili kumtawala. Inachotakiwa kufanya ni kuhakikisha tu kwamba anadaiwa kila siku.
Mesopotamia walipochukua ngano yako, walihifadhi ghalani na kukulisha wakati wa njaa. Mfumo ulirudisha kile ulichotoa.
Leo? Raia wa kawaida anakatwa kodi ya mshahara, VAT, kodi ya ardhi, mafuta, simu na bando. Lakini makampuni makubwa yenye mawakili na akaunti za nje ya nchi hayalipi kitu. Katika nchi nyingi zinazoendelea, kodi inachukuliwa kulipa madeni ya taasisi za kigeni badala ya kujenga hospitali.
wajibu wa kulipa ulibaki pale pale. Lakini faida ya uwiano ikatoweka kimya kimya.
Benjamin Franklin alisema: "Duniani hakuna kitu cha uhakika kando na kifo na kodi."
Alikuwa sahihi. Lakini hakuuliza swali la msingi zaidi: Uhakika huo unamfaidisha nani?
Majibu ya swali hilo yamekuwa tofauti kwa miaka 5,000 inategemea tu ulikuwa umesimama upande gani wa kile kibao cha udongo.
Baadhi ya watu wanasema kodi ni gharama halali ya kuwa na ustaarabu na usalama. Wengine wanasema mfumo wa sasa umerudi kule kule Roma unyonyaji wa wenye nguvu dhidi ya wasio na nguvu.
Unadhani nchi unayoishi sasa ipo upande gani kati ya hii miwili?
Lengo la mada sio kukukataza kulipa kodi, bali kutoa elimu.