Ukweli kuhusu crypto currency mtu hawezi kukuambia

Ukweli kuhusu crypto currency mtu hawezi kukuambia

Pain killer

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
14,361
Reaction score
21,680
Habari wakuu,

Hapa juzi elimu kuhusu crypto currency imekuwa inatrend Hadi bungeni huko, wabunge wameanza kuwa wanazungumzia hili swala, yule mbunge kafika mahali kabisa kasema serikali ingenunua Bitcoin za billion moja 2010 saizi tungekuwa na hela za kutosha.

Kwanza kabisa nipende kuseam kuwa crypto currency (sarafu za kidigital) ni kweli ipo na dunia inaelekea huko, kama usipojifunza saizi 2035 huko utajifunza whether you like or note, usifikili 2035 ni mbali. Kwani ndio itakuwa medium of exchange baada ya kutumia paper money kwa muda mrefu, kumbuka Kuna evolution of money ,tulitoka bater trade - metalic money -coin money - paper money soon tunaenda kwenye sarafu za kidigital.

Kwenye crypto currency Kuna vitu viwili.

  • KUTRADE CRYPTO CURRENCY
  • KUHOLD CRYPTO CURRENCY

Kama utaamua kutrade crypto currency Basi kaa ukijua upo kwenye list ya kupoteza pesa zako kwanin hutanunua coin zenye project utanunua shit coin na meme coin ambazo muda wowote zitapanda na kushuka Kama kimbunga, utajikuta unadeal na airdrop za kutosha. Hapa unaweza kumake pesa kwa haraka ,vile vile unaweza kupoteza pesa haraka haraka. Hii haiepukiki lazima tu utapoteza Kama utaamua kutdrade.

- Kama utaamua kuhold coin hapa una asilimia 99.99% ya kutokupoteza pesa yako, hii ni endapo utaamua kusoma na kuhold coin zenye project ndefu na imara huku ukitegemea kukaaa nazo zaidi ya miaka 5-10, hapa namaanisha unanunua coin unaiweka bila kuigusa, kama unavoweza nunua mahindi na kuyaweka kwenye store huku ukisubili Bei yake ipande.

Note: KWENYE CRYPTO HAKUNA MAFANIKIO YA MUDA MCHACHE ,MAFANAIKIO YA COIN YEYOTE UNAKUJA KUYAONA BAADA YA MIAKA 5-10, UKIHOLD COIN KWA JUMLA YA MIAKA 10 KWENYE WALLET YAKO KAA UKIJUA HIO COIN ITAKUBADILISHA MAISHA YAKO NA HUTOJUTA. TAITIZO NI KWAMBA WATU HAWAWEZI KUFANYA HIVYO.

- Usije ukafikili Crypto currency ni kazi, hapa utakufa na stress, hii sio kazi, hii ni sawa na uwekezaji, badala uchukue pesa yako uiweke bank uje uichukue baada ya miaka 5 ndio wanashauri ununua coin, kwan hio coin utakayo nunua baada ya miaka hiyo mitano itakuwa imepanda bei, kununua coin ni sawa umenunua mazao umeweka ndan umesubili yapande ndio uuze.

- Coin yeyote ambayo madeveloper Wana project nzuri, hio coin huwa inapanda kila mwaka usipoteza muda kuwaza kuwa coin haipandi inaweza ikapanda na kushuka wiki kadhaa miaze kachaa, lakin haiwezi kupita miaka miwili coin ipo pale pale.

Watu wengi wanashindwa kuhold coin kwa ajiri ya mafanikio ya mbele, na kujikuta wakitrade, uza na kununua ,wanaona coin inpump wananunua coin haina hata market cap, total supply haipo, circulating supply ni 0.00 lakin anajilipua tu. Kuna coin ambazo ni scam, yaani unanunua coin unaona inapanda badae ukiswap unakuta hakuna hela, haina value na anakuwa amepoteza pesa. Hivi vyote ni vimbwanga ambavyo wanakutana navyo watu wanaotrade. Kama umehold unakuwa zako pemben unaendelea na maisha yako.

Usije ukafikili hii ni biashara Kama huna kazi[emoji28] ,Kwan daily utashinda unafungua trust wallet, binance, kuaangalia coin zako huu ni uwekeza Kama nilivosema Kama unataka utajiri wekeza then endelea na Mambo yako yaan nunua coin then endelea na shughuri zako za kila siku.

JINSI UNAWEZA KUTAPELIWA

- Kwa wakala, sheria za crypto currency kama unataka kununua coin unamtumia kwanza pesa wakala, then wewe ndio anakutumia coin hapa hapa baadhi ya watu huko kwenye magroup ya wasap na telegram wamepigwa sana na kuichukia crypto japo kwa Sasa hili tatizo limeshatatuliwa, mfn binance kuna mawakala kabisa wamesajiliwa wanafanya hizo kazi.

- Kununua scam coin, kuna coin ambazo ni scam unaweza nunua na kujikuta umepoteza pesa, hizi coin zinakuwa kabisa kwenye wallet na usipokuwa Makin unapigwa vizuri, so kupitia kusoma kwanza yote haya utayaepuka, so inatakiwa unakuwa Makin.

Crypto is real, tuendeleaa kujifunza

Uzi tayari



/URL]
 
Ongezea hii
- Kuna scam website nyingi, wanakutaka ujisajiri na kununua crypto na kutrade kwao, Utaweza kununua, ila ku_withdraw sahau, hapo tayari umeshapigwa.
Yaah hii pia inawakuta wengi Sana

Lazima tusome kwanza kuelewa Mambo
 
Dadeeeki Bitcoin washenzi sana ngoma iko 155,000,000 dah
Nomaa
Screenshot_20211110-134753.jpg
 
Coin gani ni stable ? Na platform ipi safe ya kununua na kuweza kuwithdraw anytime bila marinji rinji
Kuna coin ambazo zimeshakuwa imara tayari kwenye soko Kama ...

Etherium ,Bitcoin ,Solana ,bnb ...

Kwa mtu anayeanza Hana kiasi cha pesa kikubwa siwezi kumshauli kuhold hizo coin ,Kwan Bei yake iko juu ....ila Kama una pesa za kutosha unaweza nunua ....

Coin zenye project unazijua unavosoma na kufuatilia Mambo ..mfan Tron ,doge coin ,Shiba Inu , UMI , n.k .....hizi ni coin ambazo project yake ni kubwa na hazitakuja kupotea kwenye ulimwengu wa crypto na Bei zake ni kawaida Sana .....

Mfn

1tron=$0.1134..

1shiba Inu =$0.0000546..

Hizo ni coin ambazo kufika 2030 Bei zake zitakuwa zimepanda ,sitaki kusema zitakuwa ngapi ,ila zikiwa juu...

Hizo coin haizshuki sanaa ,Wala huwa hazipandi kwa fujo,ziko slow
But sure ....
 
umesahau kwamba lazima uwe na iyo 'paper money' ili upate iyo unayoita 'sarafu ya kidijitali'

anyway andiko zuri
Mkuu simaaishi hizo pepar money zitatoweka hapana ...

Ndio maana Hadi Leo Kuna barter trade huko vijijin ,yaana watu wanauziana bidhaa kwa bidhaa ,lakin pesa bado zipo Kama mfumo wa kubadilishana....

So note na coin zitaendelea kuwepo but hizi sarafu za kidigital zitakuwa juu zaidi ,kwanin upitwe na fursa Kama hii wakati uwezo unao wa kujua Mambo ...
 
Ongezea hii
- Kuna scam website nyingi, wanakutaka ujisajiri na kununua crypto na kutrade kwao, Utaweza kununua, ila ku_withdraw sahau, hapo tayari umeshapigwa.
Ni kweli, kama waliyoingizwa mkenge Simba sports club wakamchukuwa kocha mwenye cv fake, kisa zipo kwenye website ambayo mtu yoyote anaweza kuingiza details anazozitaka kama Wikipedia.
 
Hapa me hapanihusu.nisharizika kula supu asubuhi,mchana matunda na maji makubwa jion mayai na uji.sometimes wali au ugali au mtori nyama...ya Nini niteseke tena?
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mwaka 2017 Tron (TRX) ilianzishwa Bei yake ikiwa

1tron =$0.0015 .....

Kwa wakati huo Kama kuna mtu aliamua kununua Tron za $100 ,hii ni sawa na laki mbili na nusu .....

Maana yake angekuwa na Tron ngapi unajua

1 Tron = $0.0015
?=$100

Maana yake angekuwa na tron 66,666.67 hivi ....

Unajua Bei ya Sasa ya Tron ni ngapi ,leo 2021 ......1tro = $0.10825

Hio ni miaka 4 imepita ....

So akisema auze Leo tron zake atakuwa na

1tron = $0.10825
66,666.67tro. = ???

So hapo atakuwa na $ 7216.67

Hizo unajua ni sawa na shilling ngapi ? Ni 18 million ....

Sasa unajiuliza kanunua Tron za laki mbili na nusu Leo anatron za million 18 ndani ya miaka 4 .....

Kama utaamua kuhold coin na kuendelea na Mambo yako kwa muda mrefu kaa ukijua huko mbeleni hata mwalimu ambaye amestafu amepewa pension zake huko nssf atakuamkia shikamoo kaka [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].... ......

Hapo nimaaua kuacha Bitcoin Kwan mwaka 2010 wengi huenda hatukuwa na smart phone ,nimeamua kuchukua mwaka 2017 ambao wengi humu tulikuwa tunatambua Mambo kabisa

HOLd Hold hold ..... crypto is real
 
Mwaka 2017 Tron (TRX) ilianzishwa Bei yake ikiwa

1tron =$0.0015 .....

Kwa wakati huo Kama kuna mtu aliamua kununua Tron za $100 ,hii ni sawa na laki mbili na nusu .....

Maana yake angekuwa na Tron ngapi unajua

1 Tron = $0.0015
?=$100

Maana yake angekuwa na tron 66,666.67 hivi ....

Unajua Bei ya Sasa ya Tron ni ngapi ,leo 2021 ......1tro = $0.10825

Hio ni miaka 4 imepita ....

So akisema auze Leo tron zake atakuwa na

1tron = $0.10825
66,666.67tro. = ???

So hapo atakuwa na $ 7216.67

Hizo unajua ni sawa na shilling ngapi ? Ni 18 million ....

Sasa unajiuliza kanunua Tron za laki mbili na nusu Leo anatron za million 18 ndani ya miaka 4 .....

Kama utaamua kuhold coin na kuendelea na Mambo yako kwa muda mrefu kaa ukijua huko mbeleni hata mwalimu ambaye amestafu amepewa pension zake huko nssf atakuamkia shikamoo kaka [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].... ......

Hapo nimaaua kuacha Bitcoin Kwan mwaka 2010 wengi huenda hatukuwa na smart phone ,nimeamua kuchukua mwaka 2017 ambao wengi humu tulikuwa tunatambua Mambo kabisa

HOLd Hold hold ..... crypto is real
Ina maana mkuu kwa mimi ambaye nataka kuanza,nianze na sarafu ipi hapo?kwa mtaji kidogo tuu wa laki tano labda.
 
Back
Top Bottom